Tabora United kachukueni pointi zenu 3 kwa Kagoma, mchezo ni batili.

Tabora United kachukueni pointi zenu 3 kwa Kagoma, mchezo ni batili.

Kwa Fei si alishi nda tena mara tatu,mkaleta mpira wenu wa hekima na Busara,leo mpira wetu kwenye usajili umekuwa wa hovyo, mara Lawi,mara Dube,Fei,Kagoma mara Awesu.

Hii hekima na busara huku mkiacha uweledi ndio unaucost mpira wa bongo,hasa kwenye usajili.
Kwa Fei kulikuwa na kesi ya kushinda?Fei alikuwa na mkataba na Yanga na alikosea kutaka kuuvunja kienyeji.Kuna kipi cha kushinda hapo?Mwanasheria asijejua buyer ni nani na seller ni nani kwenye mkataba sio wa kumuamini.Huo mkataba haukidhi hadhi ya kuitwa mkataba kwa kukosewa anayeuza na anayenunua.
 
Pengine watu hamjui kuwa kusaini mkataba sio kusajiliwa. Mchezaji anayemilikiwa na timu anasajiliwa kwenye mfumo baada ya timu yake kutuma code kwa timu inayomsajili. Ikiingizwa hiyo code hakuna timu nyingine duniani itakayoweza kumsajili. Kagoma hakusajiliwa na Yanga ndio maana wanahangaika, bali alisaini mkataba wa kuja kusajiliwa. Angekuwa amesajiliwa na Yanga basi Simba wangekwama kumsajili, maana ni ishu ya electroniki. Ni kama wewe hapa ukitaka kujiita kwa ID iliyomo humu tayari, utashindwa tu, kama huamini jaribu kubadili ID ujiite Kalpana
Kwa kutumia haya maelezo tuambie ilikuaje Awesu akarudishwa KMC?
 
Kwa Fei kulikuwa na kesi ya kushinda?Fei alikuwa na mkataba na Yanga na alikosea kutaka kuuvunja kienyeji.Kuna kipi cha kushinda hapo?Mwanasheria asijejua buyer ni nani na seller ni nani kwenye mkataba sio wa kumuamini.Huo mkataba haukidhi hadhi ya kuitwa mkataba kwa kukosewa anayeuza na anayenunua.
Basi nenda ukawe mwanasheria wewe, ulikua wapi mlipo shindwa kesi na KMC?
 
Tuambie sakata la Dube na Azam liliisha vipi. Dube alikuwa na mkataba na Azam hadi lini?
Dube aliilipa Azam na wakamalizana akawa huru wakati wa dirisha, wala hakuhitaji transfer tena. Kagoma aliuzwa na Singida hivyo lazima transfer ifanyike. Kama Yanga hawakupewa release letter na code ya kufanya uhamisho, waipeleke Singida FG polisi, na sio TFF
 
Pengine watu hamjui kuwa kusaini mkataba sio kusajiliwa. Mchezaji anayemilikiwa na timu anasajiliwa kwenye mfumo baada ya timu yake kutuma code kwa timu inayomsajili. Ikiingizwa hiyo code hakuna timu nyingine duniani itakayoweza kumsajili. Kagoma hakusajiliwa na Yanga ndio maana wanahangaika, bali alisaini mkataba wa kuja kusajiliwa. Angekuwa amesajiliwa na Yanga basi Simba wangekwama kumsajili, maana ni ishu ya electroniki. Ni kama wewe hapa ukitaka kujiita kwa ID iliyomo humu tayari, utashindwa tu, kama huamini jaribu kubadili ID ujiite Kalpana
Kama ingekuwa hivyo kusingekuwepo na kanuni kuhusu kosa la double signing, maana atakaewahi kutoa code TFF ndiye angekuwa mshindi. Kagoma alikuwa na mkataba wa maandishi na Yanga ambao haukusajiliwa TFF, sawa na Dube alivyokuwa na mkataba mrefu na Azam ambao ulikuwa haukusajiliwa TFF.
 
Dube aliilipa Azam na wakamalizana akawa huru wakati wa dirisha, wala hakuhitaji transfer tena. Kagoma aliuzwa na Singida hivyo lazima transfer ifanyike. Kama Yanga hawakupewa release letter na code ya kufanya uhamisho, waipeleke Singida FG polisi, na sio TFF
Dube alikuwa na mkata ulioko TFF uliokuwa unaisha 2024, lakini Azam walimsainisha mkataba usiokuweko TFF kama huu wa Yanga ambao hauko TFF pia. Ikamlazimu alipe auvunje, hata Kagoma lazima alipe auvunje mkataba wake na yanga ili aende Simba. Simba walikuwa na mkataba mpya na Israh Mwenda ambao haukusainiwa TFF pia, mwenda ilibidi auvunje ili aende Singida Black stars.
 
dilirisha la usajili lilikuwa halijafungwa, wangemsajili tu. Kwani ukiwa na mke ambae umeshamtolea mahari kwa wazazi wake na mchumba umeshampa kifunga uchumba akapokea, kama akiolewa na mke mwingine wazazi na mchumba hawana cha kujibu?
Kwenye swala la Kagoma, Simba kama Club haiadhibiki anayeadhibika hapo ni mchezaji kwa kufanya utapeli. Simba ni wahanga kama walivyo Yanga na waliweza kuingia naye mkataba na hatimaye kumsajili sababu mchezaji hakuwa amesajiriwa na klabu yoyote ndiyo maana TFF wakampatia kibali cha kuchezea Simba.
Hivyo basi, wanaostahili adhabu hapo ni mchezaji na club aliyotoka sababu kitendo walichokifanya ni utapeli. Watatakiwa kurudisha hela ya Yanga pia watakubaliana na Simba kama warudishiwe hela zao au Simba itamvumilia hadi adhabu itakapoisha. Hasara watakayoiingia Simba kama mchezaji atafungiwa ni kuikosa huduma ya mchezaji huyo pamoja na kulipia kila kitu, lakini kamwe haitanyang'anywa points zake.
 
Basi nenda ukawe mwanasheria wewe, ulikua wapi mlipo shindwa kesi na KMC?
Halafu mwisho ikawaje Awesu bado yupo KMC?
Mwanasheria asiyejua tofauti kati ya seller na buyer sio mwanasheria.Huo kwanza sio mkataba umekosewa kisheria.
 
Dube aliilipa Azam na wakamalizana akawa huru wakati wa dirisha, wala hakuhitaji transfer tena. Kagoma aliuzwa na Singida hivyo lazima transfer ifanyike. Kama Yanga hawakupewa release letter na code ya kufanya uhamisho, waipeleke Singida FG polisi, na sio TFF
Double Signing sio kosa la jinai kwamba klabu impeleke Kagoma Polisi, Double Signing nikosa ambalo kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji imepewa mamlaka na adhabu ya kutoa kwa kosa kama ilo likitokea.

Ikiwa kagoma ata kana zile Signature kama si zake basi kamati itapeleka swala ilo polisi wenye mamlakaza uchunguzi ili wazi hakiki kama ni za Kagoma au si zake.
Baada ya kupokea majibu ndipo Kamati itatoa adhabu.

Kama Yanga wataona Kagoma ana kataa zile Signature wao kama taasisi wanaweza kumfungulia kesi ya utapeli ndugu Kagoma baada ya kuwasiliana na Tff kwakua litakua kosa la Jinai.
 
Wachangiaji wengi humu hawajui maana ya pre-contract kati ya mchezaji na club inayompa huo mkataba.

Someni kanuni na sheria acheni uvivu. point zinapatikana uwanjani shekh, hakunaga kitonga.
 
Kaka unadanganya umma, kama ingekuwa hivyo TFF isingekuja na kanuni ya mchezaji kusaini timu zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Hiyo kanuni isingekuwepo kwenye bodi ya ligi.
Hapana nilikuwa namuuliza huyo jamaa, itakuwaje mchezaji akasajili zaidi ya timu 10. Sio sawa kaka hujanielewa tu.
 
Ndivyo mnavofarijiana? Leseni ya TFF ikishatoka maana yake kila kitu kipo clear. Komaeni na Kagoma pamoja na Singida, sio Simba maana atandelea kucheza hadi TFF watakaposimamisha leseni waliyoitoa
Kama nakuelewa hivi ila tatizo langu ni moja tu. Sijaelewa kwa nini Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji imemzuia Yusuph Kagoma kuitumikia Simba katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC, hali wakijua kuwa ana leseni ya TFF.
 
Back
Top Bottom