Hoja yako nzuri sana ila vigumu kupata ajira zote hizo kwa wakati mmoja. Kumbuka, kama ni ajira nasi tunaomba wizara ya utumishi ambao huajiri kulingana na wage bill na mahitaji ya sekta zote. Hiyo zinazopatikana ndiyo hizo zinaenda. Na kumbuka, wizara haziajiri Bali ajira ziko halmashauri. Muwe mnakumbuka hili jambo. Hivyo, sisi ni watunga sera na miongozo ya kisera. Hivyo, kwa sasa ndiyo maana kuna madawati ya ulinzi wa watoto shuleni, waalimu nao wamesomea kozi za uangalizi wa watoto, wazazi nao nyumbani wanao wajibu na kwenye kata, Kijiji, mitaa kuna kamati za ulinzi wa watoto. Wote Hawa wakibaini tatizo wanapeleka rufaa kwa ustawi wa jamii. Ni kama afya tu kuwa, ukiona mgonjwa unampeleka wapi au taarifa unapeleka wapi? Je mbona mtoto akiugua nyumbani tunabaini, vipi akiwa na tabia mbaya tusibaini? Hatuwajibiki?