Bora wewe unachambua tatizo. Na ndiyo maana serikali ya Awamu ya sita katika kukabiliana na umaskini imeendelea kuboresha mikopo nafuu na juzi tumepokea fedha kwa ajili ya kwenda kutoa mikopo ya Wafanyabiashara ndogo ndogo kupitia NMB mtu mmoja mmoja na siyo kikundi. Watoa komenti wengi unaona kabisa wanapitwa na taarifa nyingi ila wanatoa komenti kama vile labda wanafahamu mikakati yote. Na mikakati yenyewe tukitoa taarifa views hata mia hazifiki. 😀
Ila lete Sasa habari ya taharuki, nusu sasa Uzi wamesoma 1K
Ni jambo jema Mama kama mko na dhamira kweli ya dhati kuuondoa umasikini, iwe dhamira kweli na sio namna ya kutafuta kura na kushinda uchaguzi.
Kumaliza umasikini sio tu kutoa mikopo bali nakupunguza gharama za maisha pia, kuangalia maeneo yoote yanayopandisha gharama za maisha na kutafuta namna ya kudumu ili mwananchi apate unafuu.
Kuondoa umasikini ni pamoja na kuhakikisha watanzania wengi wanakwenda shule na kupata elimu bora itakayowawezesha kujiajiri na kuajirika ndani na nje ya mipaka yetu.
Kuondoa umasikini ni pamoja na kulinda ajira za wazawa na kuhakikisha wigo mpana wa uwekezaji unawekwa na serikali itengeneze fursa nyingi kwa watu wake Kwa kuboresha vichocheo vyote kama demokrasia, kodi rafiki, sera nzuri za uwekezaji, upatikanaji wa nishati ya uhakika na nafuu.
Kwenye kipengele cha elimu bora ndio tunawashape vijana kimaadili kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu lakini pia vichwa vyao vinakuwa smart na kutokuwa manipulated na utandawazi.
Tatizo la utandawazi lipo na litaendelea kuwepo, tunapaswa nasi kuongeza kasi kukabiliana nalo ili lisitudhidi na kuwa ndio maisha yetu, mwisho wake tunakuwa Taifa la kijinga ambalo linaweza kuchukuliwa mateka ndani ya ardhi yake.
Kwenye vikao vyenu vile Cabinet bila shaka Mama unapaswa kuhighlights hii ya mmomonyoko wa maadili ni red flag ambayo inaweza kupelekea Taifa kuanguka maana hatuna tena jamii serious zaidi ya wapenda mizaha na wafanya mizaha.
Asante