TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

TACAIDS: Wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya UKIMWI wamejitoa

Status
Not open for further replies.
Huu ugonjwa watakaobaki nao hapa duniani ni matajiri peke yao wale akina siye hatuna chetu maana dawa ya ARV ni ghali sana kuinunua kwa pesa ya kudunduliza na hivi tunaye muuaji magogoni hawezi kishindwa kutamka "kwani mimi ndio nimekuambukiza UKIMWI "
 
Mkuu unajua dozi ya ARV kwa mwezi i agharimu kiasi gani?? Hata CCM hawako pamoja na wewe kwenye suala hili
Nyie si mnajiita ni dona country na hamjawahi kushindwa vita yoyote duniani? Pambaneni na hali zenu. I say it again - At this era, ni aibu kutembeza bakuli ili mpate pesa za ARVs
 
tutakunywa kroloquine kama hawaleti ARV sisi ni nchi tajiri
Kama mdudu wa corona tulimtokomeza kwa maombi tu, sembuse huu Ukimwi? Kila mkoa tutaweka askofu wa hadhi ya gwajiboy maombi yakufa mtu yatapigwa mpaka huo Ukimwi ujute kuzaliwa.
 
Sisi ni matajiri hakuna shida, tunajenga SGR, Bwawa kubwa la kufua umeme wa megawati 2000+, tumenunua ndege 11, mbali na ujenzi wa vituo vya afya, nk hivi vyote ni fedha za ndani nini dawa za magonjwa nyemelezi!!

Maboko awe makini kusema ni miaka miwili tu
Ni kweli, kama tunanunua madawa yenye gharama kubwa ya kansa, haya hayatatushinda. Halafu unajua dawa zenyewe ni zipi? Just Co- trimoxazole
 
Nasema hivi: hamuwezi kuwa mnagongana peku daily harafu mnasubiri beberu aje kuwapa condoms na ARVs bure. Kama mnaweza kununua ndege kwa cash money, mnaweza kulipia condoms ninyi[emoji846]
Hakuna muda wa kupoteza na hakuna pesa ya kupoteza. Ifike pahala tukubali kufa ili vizazi vipya viishi kwa amani na kufaudu uchumi unaojengwa sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Moshi. Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (Tacaids) imesema wafadhili wa dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi ya Ukimwi wamejitoa.

Taarifa hiyo imetolewa jana na mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Leonard Maboko kwenye ufunguzi wa wiki ya Ukimwi duniani uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mandela vilivyopo Kata ya Pasua, Moshi mjini.

Hata hivyo, alisema mfuko ulioanzishwa na tume hiyo (AIDS Trust Fund) ulioanzishwa mwaka 2015 utasaidia kuziba pengo litakalokuwepo kwa miaka miwili.

“Wafadhili wameendelea kupungua nchini lakini huu mfuko wa ndani utasaidia kupunguza haya mapengo,” alisema Maboko.

Sasa hivi, alisema wafadhili wanatoa dawa za ARV lakini dawa za kupambana na kuzuia magonjwa nyemelezi wamejitoa.

Alisema mfuko huo utawasaidia Watanzania wanaohitaji dawa zilizokuwa zinatolewa na wafadhili waliojitoa.

Kwa upande wake, mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema takwimu zinaonyesha maambukizo ya Ukimwi yamepungua mkoani humo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2004 mpaka asilimia 2.6 mwaka 2018.

Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kupima afya zao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kujua hali za afya zao na kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.

Kilele cha siku ya Ukimwi duniani ni Desemba mosi.

Chanzo: Mwananchi
Nilisha andika before hata kuwepo hii habari
 
Utasikia "kwani mlipokuwa mnanichagua niliahidi kuleta ukimwi?"
67890.jpg
 
Hali ni njema ila sehemu kubwa ya Dawa hizi hupatikani kupitia mifuko ya wahisani kama hao USAIDS na UK AIDS na mashirika mengine. Sasa kama wahisani wanajitoa unadhani itakuwaje juu ya upatikanaji wa dawa Mkuu. Na kuna kipindi baadhi ya wagonjwa walikuwa wanakosa hizi za dawa za magonjwa nyemelezi na baadhi uwezo wao kifedha haukua mzuri kitu kilichopelekea baadhi ya wagonjwa kutoonekana tena kwenye vituo kuja kuchukua dawa ambayo inaacha maswali labda huyu mtu alivuta au alihama kituo.
Lakini hoja yangu hasa ni kwamba, wahisani hawa tunaowaita mabeberu wamekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii yetu hasa watu wanao ishi na VVU. Sasa hizo dawa zikianza kukosekana kwa msaada maana yake anapaswa ajinunulie mwenyewe. Ni changamoto kubwa sana na ukizingatia watu hawa baadhi yao Afya zao zinakuwa zimedhoofika hata kazi za kujiingizia mia mbili mia tatu wengine wanakuwa hawawezi . Mungu aibariki Tanzania na viongozi wake.
Jibu ni moja tu hizi dawa hazitibu ukimwi. Zinarefusha maisha. Kama zinarefusha maisha, tujiulize sisi waathirika hatuna nyege?. Kama tunanyege tunazimaliza vipi?, Je kwa kupiga nyeto au kwa kushiriki tendo?.

Tuache ujinga, narudia tena tuache ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom