Citizen_37
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 957
- 1,124
Walinywea kwa lipi jambo zito kuzidi la bandari?Kama TEC wana ubavu mbona kwa Magufuli walinywea.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walinywea kwa lipi jambo zito kuzidi la bandari?Kama TEC wana ubavu mbona kwa Magufuli walinywea.
Kitu kibaya ni kibaya tu. Hakuna cha kupambana na CHADEMA wala TEC...Kwa dhati kabisa ninawasihi wanaCCM tusije tukafanya kosa la kuwafananisha TEC na CHADEMA. Nimeona uzi wa ndugu Sir John Roberts akidai wanaCCM tuachiwe TEC kukabiliana nao. Naheshimu mawazo yake kama mwanaCCM mwenzangu ila siungi mkono hoja yake kwa 100%. Sir John labda haijui kiundani TEC akadhani nao pia watajibiwa kirahisi kama tunavyowajibu chama cha Mbowe.
Kanisa katoliki kama ilivyo CCM nalo limeenda hadi ngazi ya shina.. na linaongoza kwa kuwa na waumini wengi zaidi hapa nchini na duniani kwa ujumla. Wanaposema waraka wao utasomwa kwenye jumuiya ina maana hadi wananchi wa vijiji vya ndani huko Buhigwe au Kalambo wataamshwa usingizini. CHADEMA wao mambo yao huishia tu mijini na Twitter kwahiyo damage yao ni ndogo kulinganisha na hiki wanachofanya TEC.
Kingine kinachoogopesha ni hii tabia ya wakatoliki kuwa wakimya. Mapadre na maaskofu ni wasomi ambao tangu shuleni walikuwa ni vipanga yaani hawabahatishi. Wao wakishasema lao huwa hawahagaiki sana kubishana kitu kinachotia hasira mno. Ingekuwa CHADEMA hadi muda huu ungekuta Lema au Heche kashajitokeza na kuropoka pumba. Sasa hao TEC toka Padre Kitime aongee sijasikia kiongozi mwingine yeyote akiongea. Ni watu hatari. Hata tukisema CCM tuishambulie TEC kwa maneno bado itakua sawa na kujishambulia wenyewe kwasababu kuna wanaCCM wengi ambao ni wakatoliki. Kutakuwa na upinzani wa ndani.
Ikumbukwe pia hawa TEC hadi kutamka tayari wana mawasiliano na kiongozi wao mkubwa yaani Papa. Kwa msiojua nguvu ya papa mkasome kisa cha Papa Gregory VI na King Henry IV ndo mtaelewa vizuri. Mfalme alikalishwa kwenye baridi siku 3 akisubiri kuonana na papa amwombe msamaha. Haikuwa poa. Katoliki pia limekuwa likihusishwa na siasa za nchi nyingi duniani. Kwenye story ya vita ya Biafra huko Nigeria hili kanisa lilitajwa kufadhili waasi.
Wito wangu ni kuwasihi wasomi na wataalamu wa diplomasia & siasa ndani ya chama na serikali kukaa chini na TEC ili kumalizana nao. Kama kuna mbinu nyingine ambazo sio za kidiplomasia lakini zinaweza kutuliza hali ya hewa nazo pia zitumike.
Umeandika andika ila hapo mwishoni acha kunisingizia uongo kwamba "Heri wewe umeelewa na unajua kuwaheshimu watumishi wa Mungu - Maaskofu wetu.."... mimi naheshimu taifa la Tanzania na ninapenda liwe na amani. Ninawatambua hao mapadre na maaskofu ila wao wataheshimiwa na waumini wao kwamba ni watumishi wa Mungu ila sio mimi. Ukitaka kushinda vita usidharau uwezo wa adui yako. Mimi nilichokifanya nimekumbusha chama changu CCM kutodharau hawa TEC kwa sababu wanatajwa hadi kusaidia waasi kwenye Biafra civil war. Sehemu mbalimbali zenye machafuko hili dhehebu limekuwa likitajwa. Ukijumlisha na kashfa zao za ulawiti naona hakuna haja ya mtu mwenye akili timamu kuwaheshimu hao kuwa ni watumishi wa Mungu.Kitu kibaya ni kibaya tu. Hakuna cha kupambana na CHADEMA wala TEC...
Sasa wewe MamaSamia2025, kama Prof. Makame Mnyaa Mbarawa - Waziri wa Ujenzi & Usafirishaji (Mzanzibari) aliyetumwa na Rais Samia Suluhu Hassan (Mzanzibari) kutia saini mkataba huu wa kishenzi na kihuni aliwaita hawa maskofu na kujaribu kuwashawishi wakubaliane naye, ikashindikana kwa sababu hakueleweka, then hakuna cha kufanya. Hakueleweka kwa sababu mkataba wenyewe haushawishi mtu yeyote mwenye akili timamu na ufahamu kuuelewa ..
Hapa hakuna cha Sir John Roberts wala wewe MamaSamia2025 unasema nini kwenye hili jambo lenu kukubalika...
Hili jambo liko kwenye point of no return kwa sababu mkataba huu ni kinyesi ambacho kimeshaingia funza na kinatoa harufu Kali ya uvundo. Haiwezekani kukipaka rangi yoyote ili kionekane kizuri..!!
Kama ni lazima sana bandari zetu za Tanganyika zipate mwekezaji sasa toka nje ya sisi wenyewe, then the best decision ni kurudi kwenye drawing board na kutangaza tender upya, kwa uwazi na kila kampuni ambayo itakuwa interested, iombe na atakayeshinda tender hiyo Kwa mujibu wa vigezo vyetu, basi anapewa kazi hiyo...
Kuna ugumu gani kufanya hivi? Je, serikali itajiona sio serikali tena iwapo italiacha hili jambo? Kwanini tumatafuta shida na matatizo pasipo sababu za msingi za kufanya hivyo?
Ni ujinga sana kwa serikali kuanza kupambana na wananchi ambao serikali imewekwa hapo na wao kwa sababu ya jambo hili..
Heri wewe umeelewa na unajua kuwaheshimu watumishi wa Mungu - Maaskofu wetu..
Innalilah!?TEC watumie busara zaidi maana hiki chama chakavu hakikawii kuwaita BAKWATA ili mgogoro wa kuligawa Taifa uanze.
Kuna kundi la UVCCM linawakusanya Mashehe huku TMK ni kusambaza sumu za Udini
Umoja wetu wa Kitaifa ni TUNU ya kujivunia.
huyu jamaa amejitAhidi kwelikweli kuyaweka sawa mwenye sikio na asikieWito wangu ni kuwasihi wasomi na wataalamu wa diplomasia & siasa ndani ya chama na serikali kukaa chini na TEC ili kumalizana nao. Kama kuna mbinu nyingine ambazo sio za kidiplomasia lakini zinaweza kutuliza hali ya hewa nazo pia zitumike.!
Hili bungo litemeni yataisha
Afadhali mmeanza kupata tuakili.Kwa dhati kabisa ninawasihi wanaCCM tusije tukafanya kosa la kuwafananisha TEC na CHADEMA. Nimeona uzi wa ndugu Sir John Roberts akidai wanaCCM tuachiwe TEC kukabiliana nao. Naheshimu mawazo yake kama mwanaCCM mwenzangu ila siungi mkono hoja yake kwa 100%. Sir John labda haijui kiundani TEC akadhani nao pia mbazo sio za kidiplomasia lakini zinaweza kutuliza hali ya hewa nazo pia zitumike.
Pole sana kwa kukusingizia..!Umeandika ila hapo mwishoni acha kunisingizia uongo kwamba "Heri wewe umeelewa na unajua kuwaheshimu watumishi wa Mungu - Maaskofu wetu.."
Kipi kinapaswa kuwa cha kwanza kupewa heshima; Mungu aliyeiumba Tanzania na kukufanya wewe uishi ndani yake au Tanzania iliyoumbwa na Mungu?.mimi naheshimu taifa la Tanzania na ninapenda liwe na amani.
I now understand you..Ninawatambua hao mapadre na maaskofu ila wao wataheshimiwa na waumini wao kwamba ni watumishi wa Mungu ila sio mimi.
Saa mbovu km vile inataka kusema ukweli.Ni ujinga uliotukuka kulinganisha Chama cha Siasa na Kanisa Moja Takatifu La Mitume [emoji1][emoji1]
Wanaccm Wote leo wamehudhuria Kanisani utadhani kulikuwa na Posho kama kwenye vikao Vya Uchawa na tulikuwa Wapole haswa bora utengwe na Chama Lakini siyo Dhehebu lako [emoji23][emoji91]
Mimi ni mtu mwenye akili nyingi sana na ninapenda Tanzania iendelee kuwa na amani. Wanachofanya TEC ni kuchonganisha wananchi na serikali na mbinu wanayotumia sio ya kuichukulia poa. Ni mbinu hatariAfadhali mmeanza kupata tuakili.
Basi mfiche masaburi yenu yaliyopauka kama mmekalia majivu.Mimi ni mtu mwenye akili nyingi sana na ninapenda Tanzania iendelee kuwa na amani. Wanachofanya TEC ni kuchonganisha wananchi na serikali na mbinu wanayotumia sio ya kuichukulia poa. Ni mbinu hatari
Mbona alishasema, WaTanzania ni watu wa kuropoka alafu baadae wanakaa kimya!! Which is true.Samia amekosa kabisa mbinu za kuliongoza taifa, practically kwa sasa ameamua kukaa kimya, kila mwenye la kusema amsaidie kusema ili kumpunguzia mzigo wa tatizo alilotengeneza kwa ukaidi wake.
Bahati mbaya hawa anaowaacha waseme ilimradi kumtetea, sasa ndio wanazidi kulifanya tatizo liwe kubwa, kwasababu wanaropoka kwa namna ya hovyo isiyo na staha kwa wale wanaowasema, matokeo yake hali ya Samia ndio inazidi kuwa mbaya.
mbona hawahusiki kwa lolote hapo[emoji51][emoji51]chadema ni wapumbavu sana
waraka wa TEC utoshe kuwakilisha hao ndugu wengine akina CCT, CPTC na wengine wanaofanana nao. TEC wamemaliza kila kituTunapongeza TEC kwa kujitambua na kutetea watanganyika bila woga. Mmetimiza jukumu lenu kama viongozi wa kidini kuhakikisha ustawi wa waumini wenu unalindwa kwa njia yoyote ile.
Kuna watu wanasema siasa inachanganywa na dini. Mmejenga hospitali, hiyo ni dini? Mmejenga mashule , hiyo ni dini? Mmefungua vituo vya kulea watoto na mambo mengi sana. Tupuuze hawa wanasiasa uchwara wanaotaka ku propel mambo ya udini. Tunasubiri CCT.
ASANTE
nyie hamjui hao wajinga lazima wanahusikambona hawahusiki kwa lolote hapo[emoji51][emoji51]
Kwa dhati kabisa ninawasihi wanaCCM tusije tukafanya kosa la kuwafananisha TEC na CHADEMA. Nimeona uzi wa ndugu Sir John Roberts akidai wanaCCM tuachiwe TEC kukabiliana nao. Naheshimu mawazo yake kama mwanaCCM mwenzangu ila siungi mkono hoja yake kwa 100%. Sir John labda haijui kiundani TEC akadhani nao pia watajibiwa kirahisi kama tunavyowajibu chama cha Mbowe.
Kanisa katoliki kama ilivyo CCM nalo limeenda hadi ngazi ya shina.. na linaongoza kwa kuwa na waumini wengi zaidi hapa nchini na duniani kwa ujumla. Wanaposema waraka wao utasomwa kwenye jumuiya ina maana hadi wananchi wa vijiji vya ndani huko Buhigwe au Kalambo wataamshwa usingizini. CHADEMA wao mambo yao huishia tu mijini na Twitter kwahiyo damage yao ni ndogo kulinganisha na hiki wanachofanya TEC.
Kingine kinachoogopesha ni hii tabia ya wakatoliki kuwa wakimya. Mapadre na maaskofu ni wasomi ambao tangu shuleni walikuwa ni vipanga yaani hawabahatishi. Wao wakishasema lao huwa hawahagaiki sana kubishana kitu kinachotia hasira mno. Ingekuwa CHADEMA hadi muda huu ungekuta Lema au Heche kashajitokeza na kuropoka pumba. Sasa hao TEC toka Padre Kitime aongee sijasikia kiongozi mwingine yeyote akiongea. Ni watu hatari. Hata tukisema CCM tuishambulie TEC kwa maneno bado itakua sawa na kujishambulia wenyewe kwasababu kuna wanaCCM wengi ambao ni wakatoliki. Kutakuwa na upinzani wa ndani.
Ikumbukwe pia hawa TEC hadi kutamka tayari wana mawasiliano na kiongozi wao mkubwa yaani Papa. Kwa msiojua nguvu ya papa mkasome kisa cha Papa Gregory VI na King Henry IV ndo mtaelewa vizuri. Mfalme alikalishwa kwenye baridi siku 3 akisubiri kuonana na papa amwombe msamaha. Haikuwa poa. Katoliki pia limekuwa likihusishwa na siasa za nchi nyingi duniani. Kwenye story ya vita ya Biafra huko Nigeria hili kanisa lilitajwa kufadhili waasi.
Wito wangu ni kuwasihi wasomi na wataalamu wa diplomasia & siasa ndani ya chama na serikali kukaa chini na TEC ili kumalizana nao. Kama kuna mbinu nyingine ambazo sio za kidiplomasia lakini zinaweza kutuliza hali ya hewa nazo pia zitumike. Kinachofanywa na TEC ni kuchonganisha serikali na wananchi huku wakitumia mbinu hatari ambayo sio ya kubeza.