KERO Tafadhali Serikali fungieni mchezo wa AVIATOR, Mchezo sio fair na unaua ndoto za Vijana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ushatoa maumivu yako sasa nenda kachukue jembe kalime, uje utoe ushuhuda hapa ulivyofanikiwa ili vijana waachane na hiyo aviator uliyotaja.
Sawa buda, kesho naingia shambani.
 
Ndoto zako zilikua kuwa tajiri kwa usiku mmoja mwekezaji kameza ndoto zako

Badili attitude wachana na kamari kijana hakuna mafanikio huko

Mafanikio (ikiwemo utajiri ni mchakato ) mrefu sana kubali steps wachana na overnight changes
Sawa Mkuu, nimepokea ushauri huu.

Ila Aviator *****.
 
Reactions: a45
Mchezo wa kamali ni sitarehe kama ilivyo pombe

Shida ni kwamba vijana wanaifanya kamali kuwa ajira badala ya sitarehe
Yani uliwe hela useme ni starehe? Wake up buda.
 
Kwa miaka ya hivi karibuni vijana wengi na baadhi ya watu wazima wamejiingiza kwenye kamari kama sehemu ya kutafuta kipato. Kwa bahati mbaya imekuwa maumivu na stress mara dufu
Acha Mkuu, vijana tunapata pressure kwenye umri mdogo.
 
Upumbavu wa hali ya juu.
Na hili nalo unataka usaidiwe?
Tunapoelekea siku tako likikuwasha utaenda kuomba serikali ikusaidie.
Kwani siyo kazi ya serikali? Dunia kote kudhibiti madhara ya kamari au madawa ya kulevya ni serikali inakuwa kiongozi. Kwa zama hizi za electronics, kudhibiti madhara ya kamari ni rahisi japo huwezi kuondoa kabisa. Wanatakiwa waweke sheria kuwa kila mtoa huduma ahakikishe wanaocheza wana account zilizofunguliwa kwa kutumia utambulisho maalum eg vitambulisho vya NIDA, na waweke limits za mcheza kamari kwa wiki au mwezi.
 
Qur'an
5:90
{ یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوۤا۟ إِنَّمَا ٱلۡخَمۡرُ وَٱلۡمَیۡسِرُ وَٱلۡأَنصَابُ وَٱلۡأَزۡلَـٰمُ رِجۡسࣱ مِّنۡ عَمَلِ ٱلشَّیۡطَـٰنِ فَٱجۡتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ }
[Surah Al-Māʾidah: 90]

Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
 
Wewe ndio ujiepushe na kamari. Hakuna aliyewahi kufanikiwa kwa kucheza kamari.
 
hii kali hii!
»kila mbongo anataka kuwa RUBANI bila kupitia mafunzo ya chuo. hongereni mapailoti wa kwenye tarakilishi.
 
Aviator imeondoka na ada yangu, upande wa vifaa. Alaaniwe aliyeanzisha mchezo huu.
 
Nimekua mraibu wa kamari kwenye mchezo wa Aviator, nimepoteza zaidi ya milioni 14 hela ya biashara Sasa hivi Sina kazi
 
Hapo wa kufungiwa ni hao vijana.wazalishe mazao wakiwa chini ya uangalizi. Program za BBT zimekimbiwa na vijana wapenda kitonga kama hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…