Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Kwa heshima na taadhima, naomba kuchukua nafasi hii kuwashauri ndugu zangu watumiaji wenzangu wa mtandao huu mkubwa na huru wa JamiiForums. Tukiwa sehemu ya jukwaa hili lenye mchango mkubwa katika kukuza mijadala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na hata kidemokrasia, hatuna budi kuwa na nidhamu ya hoja, staha ya lugha, na kuheshimu misingi ya maadili ya mtandao huu pamoja na sheria za nchi yetu.
Kwa masikitiko makubwa, kumekuwepo na wimbi la baadhi ya wachangiaji kutumia lugha ya matusi, kejeli na dharau kubwa wanapolizungumzia Chama Cha Mapinduzi (CCM) – chama kinachoongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ingawa kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni, haki hiyo haipaswi kuvuka mipaka ya kistaarabu na kugeuka kuwa matusi au uchochezi.
Tafadhali tukumbuke yafuatayo:
1. CCM ni chama kinachoongoza serikali kwa ridhaa ya wananchi kupitia sanduku la kura. Kukitukana chama hiki si tu kutoheshimu uamuzi wa Watanzania wengi, bali ni kudhalilisha taasisi inayobeba uongozi wa nchi.
2. Kama una hoja dhidi ya uongozi wa mtu fulani au sera fulani, tumia lugha ya staha, hoja zenye msingi na uwasilishe kwa njia inayojenga. Kukosoa kwa heshima kuna nafasi kubwa ya kusikilizwa kuliko kutukana kwa jazba na kejeli.
3. Matumizi ya majina bandia (fake id's ) hayana maana iwapo yanatumika kupandikiza chuki, matusi na madhara ya kijamii au kisiasa. Uhuru wa mtandao si leseni ya matusi.
4. Tanzania ni yetu sote – itajengwa kwa hoja, mijadala yenye tija na heshima kwa tofauti zetu, si kwa matusi ya kisiasa yanayoashiria chuki au dhihaka.
Naomba niweke bayana: Kumkosoa kiongozi ni haki ya kidemokrasia, lakini kumtukana au kudhalilisha chama kizima kwa ujumla ni upungufu wa hekima na ni hatari kwa mshikamano wa kitaifa.
Tuendelee kujenga hoja, si kubomoa heshima ya taasisi. Tusikubali kuwa vyanzo vya sumu ya mgawanyiko wa taifa kupitia maneno yetu.
Tuijenge Tanzania yetu kwa heshima, busara na uzalendo.