Tafafakari yangu na maoni yangu kwa Watumiaji wa huu mtandao

Majaliwa kassim majaliwa ndiyo aliyempa JAMBIA LA KUUA WATU Huyo mtu anayeitwa MAFWELE.
Leo nani hajui kwamba mafwele ndiyo anahusika na mauaji, utesaji na utekaji wa watu?
Nani alimuua mzee kibao kama siyo mafwele?
Huyo mafwele anaishi wapi mpaka yeye auwe watu alafu aendelee kuishi na kula pesa za watu anao wauwa?
 
Kwa mfano nikisema ccm ni wezi wa kura,

Hilo ni tusi au reality?
 
Wakuu!
Naona replies nyingi kwenye huu uzi zimeenda tofauti na Tafakari yangu kabisa. Lengo la kuanzisha huu uzi ilikuwa ni kuwakumbusha tu Members wenzangu matumizi ya uhuru wao wa kutoa maoni mtandaoni hata kama tunatumia fake id's.

Wiki iliyopita kuna Member aliandika maneno yasiyokuwa na staha hata kidogo. Kuwatuhumu Wabunge na Mawaziri wanawake wote wameshatembea na wanafanya maamuzi katika teuzi mbalimbali katika nafasi au vyeo serikalini.

Mpaka Mheshimiwa waziri Dkt. Gwajima D ile comment akaiona na akamjibu yule aliye comment naye akaishia kuomba msamaha tu.

Kabla ya kujibu chochote Soma na uelewe sio kukurupuka na kujibu kwa utashi wako.
 
Naomba unijubu,

Kusema ccm ni wezi na wanufaika wa vitendo vya vizi wa kura kwa kukataa Reforms kupata Tume huru ya uchaguzi,

Kuwaita wezi wa kura ni tusi au ni ukweli wenyewe?
 
Kwa heshima na taadhima, naomba kuchukua nafasi hii kuwashauri ndugu zangu watumiaji wenzangu wa mtandao huu mkubwa na huru wa JamiiForums. Tukiwa sehemu ya jukwaa hili lenye mchango mkubwa katika kukuza mijadala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na hata kidemokrasia, hatuna budi kuwa na nidhamu ya hoja, staha ya lugha, na kuheshimu misingi ya maadili ya mtandao huu pamoja na sheria za nchi yetu.

Kwa masikitiko makubwa, kumekuwepo na wimbi la baadhi ya wachangiaji kutumia lugha ya matusi, kejeli na dharau kubwa wanapolizungumzia Chama Cha Mapinduzi (CCM) – chama kinachoongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ingawa kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni, haki hiyo haipaswi kuvuka mipaka ya kistaarabu na kugeuka kuwa matusi au uchochezi.

Tafadhali tukumbuke yafuatayo:

1. CCM ni chama kinachoongoza serikali kwa ridhaa ya wananchi kupitia sanduku la kura. Kukitukana chama hiki si tu kutoheshimu uamuzi wa Watanzania wengi, bali ni kudhalilisha taasisi inayobeba uongozi wa nchi.

2. Kama una hoja dhidi ya uongozi wa mtu fulani au sera fulani, tumia lugha ya staha, hoja zenye msingi na uwasilishe kwa njia inayojenga. Kukosoa kwa heshima kuna nafasi kubwa ya kusikilizwa kuliko kutukana kwa jazba na kejeli.

3. Matumizi ya majina bandia (fake id's ) hayana maana iwapo yanatumika kupandikiza chuki, matusi na madhara ya kijamii au kisiasa. Uhuru wa mtandao si leseni ya matusi.

4. Tanzania ni yetu sote – itajengwa kwa hoja, mijadala yenye tija na heshima kwa tofauti zetu, si kwa matusi ya kisiasa yanayoashiria chuki au dhihaka.

Naomba niweke bayana: Kumkosoa kiongozi ni haki ya kidemokrasia, lakini kumtukana au kudhalilisha chama kizima kwa ujumla ni upungufu wa hekima na ni hatari kwa mshikamano wa kitaifa.

Tuendelee kujenga hoja, si kubomoa heshima ya taasisi. Tusikubali kuwa vyanzo vya sumu ya mgawanyiko wa taifa kupitia maneno yetu.

Tuijenge Tanzania yetu kwa heshima, busara na uzalendo.
Umerudisha fomu?
 
Leo nadhani umeshinda kwa lishangazi la ccm.

Taasisi au chama chochote na hata serikali yoyote ile inapokuwa haiwajari na kuwaua raia wake na hafatilii mbaya zaidi mkuu wa nchi anasema kifo ni kifo tu.Serikali ya namna hiyo inastahili kila aina ya lugha iwe nzuri au mbaya matusi au kuzomewa maana imekoswa uhalali wa kurinda wana nchi.

Watu wanaongea hayo yote maana wanauchungu sana nafisini mwao wana hasira kali mno.Imagine ndg wa mzee kibao unaweza kuwaambia kwa lugha gani wakakuelewa? kama hawatakukata panga basi una bahati.

Ebu vaa uhalisia wa familia ya mdude hao akisimama kwa uchungu akataukana serkali utasema hana adabu au serikali ndo haina adabu.
 
Kwa masikitiko makubwa, kumekuwepo na wimbi la baadhi ya wachangiaji kutumia lugha ya matusi, kejeli na dharau kubwa wanapolizungumzia Chama Cha Mapinduzi (CCM) – chama kinachoongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ingawa kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni, haki hiyo haipaswi kuvuka mipaka ya kistaarabu na kugeuka kuwa matusi au uchochezi.
Nilianza kukupuuza niliposoma haya hapo juu.

Nenda kawaambie wenzako wawe wa kwanza kuwa na sifa hizo unazotuletea na kutuhimiza hapa.

Unatumia lugha ile ile ya walaghai wenzio huko kwenye Genge na huyo Samia Suluhu Hassan mwenyewe! Hivi hamtambui kwamba matatizo haya mnayaanzisha wenyewe? Tendeni HAKI; kuweni wakweli kwa waTanzania, halafu uone kama kutakuwa na lazima yoyote ya kuleta uchafu wako humu JF.

Hopeless Kabisa.
 
Kukosoa kwa heshima kuna nafasi kubwa ya kusikilizwa kuliko kutukana kwa jazba na kejeli.
Tumekwisha vuka hatua hiyo ya kubembelezana, kwa sababu ya ukiziwi wenu.

Tueleze kwa nini hamtaki pawepo na marekebisho ya kanuni za uchaguzi, ili HAKI itendeke katika kuwaata viongozi. Kinacho wazuia kufanya hivyo ni kitu gani?

Eti "kukosoa kwa heshima"; heshima kwa watu wanaoteka na kuoteza waTanzania?
 
Tuendelee kujenga hoja, si kubomoa heshima ya taasisi. Tusikubali kuwa vyanzo vya sumu ya mgawanyiko wa taifa kupitia maneno yetu.

Tuijenge Tanzania yetu kwa heshima, busara na uzalendo.
Ungeeleka ushauri wako huu huko kunakoanzia matatizo ya mfarakanyo wa taifa, ungeonekana kuwa mtu wa maana sana.
Hapa unakuja kuwalaumu wahanga wa ubovu wa hao unaowakingia kifua; na wewe kujionyesha kuwa mmoja wao.
 
Waambie kwanza waache kutumia polisi kuua na kuteka watu ndio na sisi tutaongea nao kwa sitaha

Angalia waumini wa Gwajima wanavyoteswa na CCM

Halafu vaa viatu vyao Chawa wewe!!
central si unapajua nenda kawaambie
 
Back
Top Bottom