Tafafakari yangu na maoni yangu kwa Watumiaji wa huu mtandao

Mkuu umeandika vizuri. Ila hao jamaa unaoshauri wanaamini wana akili kuliko mtu yeyote asiyefuata matakwa yao au mtizamo wao. Watatukana yeyote kwa tusi lolote.

Mimi kama Mwana CCM na mtiifu kwa Serikali, baada ya kushindwa kuwavumilia nimeamua siku nyingi tu, kujenga hoja inapobidi, kuwarudishia matusi wanapotukana na kumtukana yeyote anatakayenitukana au kumtukana Kiongozi yeyote wa CCM au Serikali na kuwatisha vilevile wanpoleta vitisho. Sera yangu mimi kwao ni "An eye for an eye"!

Naamini kwa kufanya hivyo, tutaenda sambamba!
Hiyo inaweza kuwa ya wasiohulikana
 
No Reform No Election.
Hakika! Kusema ukweli kabisa CCM hawastahili heshima hata kidogo. Haiwezekani watu zaidi ya 100 kutekwa, kuteswa au kuuawa kabisa halafu hakuna kiongizi yeyote kuanzia RAIS, Makamu wa RAIS na waziri Mkuu aliye kemea jambo hili ovu! Halafu anakuja mjinga mmoja anataka tuwape HESHIMA....!
 
Malalamiko ya raia ilibidi yawe Moral codes zao.
Kwa ujinga walionao vichwani wanajiona wao ndio kila kitu.
ISHI au Ishia.
unyenyekevu na uadilifu viifaa vya Utumwa.
 
Huu uzi ufutwe,ikiwezekana mamod muifute na ccm yenyewe...
 
Hakika! Kusema ukweli kabisa CCM hawastahili heshima hata kidogo. Haiwezekani watu zaidi ya 100 kutekwa, kuteswa au kuuawa kabisa halafu hakuna kiongizi yeyote kuanzia RAIS, Makamu wa RAIS na waziri Mkuu aliye kemea jambo hili ovu! Halafu anakuja mjinga mmoja anataka tuwape HESHIMA....!
Maajabu ya 10 ya dunia yatakuwa
 
Kwa heshima na taadhima, naomba kuchukua nafasi hii kuwashauri ndugu zangu watumiaji wenzangu wa mtandao huu mkubwa na huru wa JamiiForums. Tukiwa sehemu ya jukwaa hili lenye mchango mkubwa katika kukuza mijadala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na hata kidemokrasia, hatuna budi kuwa na nidhamu ya hoja, staha ya lugha, na kuheshimu misingi ya maadili ya mtandao huu pamoja na sheria za nchi yetu.

Kwa masikitiko makubwa, kumekuwepo na wimbi la baadhi ya wachangiaji kutumia lugha ya matusi, kejeli na dharau kubwa wanapolizungumzia Chama Cha Mapinduzi (CCM) – chama kinachoongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ingawa kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni, haki hiyo haipaswi kuvuka mipaka ya kistaarabu na kugeuka kuwa matusi au uchochezi.

Tafadhali tukumbuke yafuatayo:

1. CCM ni chama kinachoongoza serikali kwa ridhaa ya wananchi kupitia sanduku la kura. Kukitukana chama hiki si tu kutoheshimu uamuzi wa Watanzania wengi, bali ni kudhalilisha taasisi inayobeba uongozi wa nchi.

2. Kama una hoja dhidi ya uongozi wa mtu fulani au sera fulani, tumia lugha ya staha, hoja zenye msingi na uwasilishe kwa njia inayojenga. Kukosoa kwa heshima kuna nafasi kubwa ya kusikilizwa kuliko kutukana kwa jazba na kejeli.

3. Matumizi ya majina bandia (fake id's ) hayana maana iwapo yanatumika kupandikiza chuki, matusi na madhara ya kijamii au kisiasa. Uhuru wa mtandao si leseni ya matusi.

4. Tanzania ni yetu sote – itajengwa kwa hoja, mijadala yenye tija na heshima kwa tofauti zetu, si kwa matusi ya kisiasa yanayoashiria chuki au dhihaka.

Naomba niweke bayana: Kumkosoa kiongozi ni haki ya kidemokrasia, lakini kumtukana au kudhalilisha chama kizima kwa ujumla ni upungufu wa hekima na ni hatari kwa mshikamano wa kitaifa.

Tuendelee kujenga hoja, si kubomoa heshima ya taasisi. Tusikubali kuwa vyanzo vya sumu ya mgawanyiko wa taifa kupitia maneno yetu.

Tuijenge Tanzania yetu kwa heshima, busara na uzalendo.
Kuna jamaa wa mbogamboga huwa anatukana watu sijui wamempiga ban jina linaanza na S nimemsahau jina kamili kila post yeye ni kutukana tu
 
Hakika! Kusema ukweli kabisa CCM hawastahili heshima hata kidogo. Haiwezekani watu zaidi ya 100 kutekwa, kuteswa au kuuawa kabisa halafu hakuna kiongizi yeyote kuanzia RAIS, Makamu wa RAIS na waziri Mkuu aliye kemea jambo hili ovu! Halafu anakuja mjinga mmoja anataka tuwape HESHIMA....!
Wanauudhi sana
 
Kwa heshima na taadhima, naomba kuchukua nafasi hii kuwashauri ndugu zangu watumiaji wenzangu wa mtandao huu mkubwa na huru wa JamiiForums. Tukiwa sehemu ya jukwaa hili lenye mchango mkubwa katika kukuza mijadala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na hata kidemokrasia, hatuna budi kuwa na nidhamu ya hoja, staha ya lugha, na kuheshimu misingi ya maadili ya mtandao huu pamoja na sheria za nchi yetu.

Kwa masikitiko makubwa, kumekuwepo na wimbi la baadhi ya wachangiaji kutumia lugha ya matusi, kejeli na dharau kubwa wanapolizungumzia Chama Cha Mapinduzi (CCM) – chama kinachoongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ingawa kila Mtanzania ana haki ya kutoa maoni, haki hiyo haipaswi kuvuka mipaka ya kistaarabu na kugeuka kuwa matusi au uchochezi.

Tafadhali tukumbuke yafuatayo:

1. CCM ni chama kinachoongoza serikali kwa ridhaa ya wananchi kupitia sanduku la kura. Kukitukana chama hiki si tu kutoheshimu uamuzi wa Watanzania wengi, bali ni kudhalilisha taasisi inayobeba uongozi wa nchi.

2. Kama una hoja dhidi ya uongozi wa mtu fulani au sera fulani, tumia lugha ya staha, hoja zenye msingi na uwasilishe kwa njia inayojenga. Kukosoa kwa heshima kuna nafasi kubwa ya kusikilizwa kuliko kutukana kwa jazba na kejeli.

3. Matumizi ya majina bandia (fake id's ) hayana maana iwapo yanatumika kupandikiza chuki, matusi na madhara ya kijamii au kisiasa. Uhuru wa mtandao si leseni ya matusi.

4. Tanzania ni yetu sote – itajengwa kwa hoja, mijadala yenye tija na heshima kwa tofauti zetu, si kwa matusi ya kisiasa yanayoashiria chuki au dhihaka.

Naomba niweke bayana: Kumkosoa kiongozi ni haki ya kidemokrasia, lakini kumtukana au kudhalilisha chama kizima kwa ujumla ni upungufu wa hekima na ni hatari kwa mshikamano wa kitaifa.

Tuendelee kujenga hoja, si kubomoa heshima ya taasisi. Tusikubali kuwa vyanzo vya sumu ya mgawanyiko wa taifa kupitia maneno yetu.

Tuijenge Tanzania yetu kwa heshima, busara na uzalendo.
Ujue ushindi wao wa magumashi. Mtu aliyeshinda uchaguzi kihalali hawezi kuteka kuuwa wala kupoteza wananchi wake wanaokosoa.
 
Back
Top Bottom