Tafakuri: Kuna nini nyuma ya mashambulizi haya kwa Makamba?

Tafakuri: Kuna nini nyuma ya mashambulizi haya kwa Makamba?

Wizara hiyo ina changamoto nyingi sana. Mtu pekee aliyekuwa na uelekeo wa kuimudu ni Prof. Muhongo. Bahati mbsya awamu ya 5 ilikuwa haiwataki watu wenye independent brain.
Safi, we umeongea kama mtu mwenye akili huru.
 
Mtatumia kila njia kumsafisha
ila ubovu wa makamba hasa suala la kukatika katika ovyo na mgao wa umeme hauhitaji elimu ya chuo kikuu kugundua kua jamaa Ni mbabaishaji au anatuhujumu kwa maksudi kabisa.
Huyu jamaa lawama zote nilikuwa siamini ila juzi alichokiongea Mwanza na wafanyakazi wa TANESCO ndio niliamini hakuna kitu pale
 
Anyways ngoja nikuache, maana badala ya kutumia akili unaanza kutumia hisia.
Shida yangu mimi, kama ungeamua kunielewa, ni kuelezwa, kwa usahihi na ushahidi, huo wizi na ubaya wake mwingine ili tuzungumze lugha moja nanyi mnamshambulia. Kusema tu mwizi, amefeli f4 n.k bila kutushahidisha inafanya wengine tushangae imekuaje kwani?!!!
 
Mimi sijamtaja kwamba ni mwizi, maana hapo nitakuwa natumia hisia. Lkn uongo wake kuhusu mradi wa JNHEP mimi sitamsamehe kamwe. Hawezi kuhujumu legacy ya taifa akaangaliwa tu.
 
Katika viongozi makini na wawajibikaji na Makamba huwa unamhesabu.

Huyu angepewa wizara ya michezo basi ila wizara ya Nishati chenga tupu.

Kwanza hakuna wizara ambayo makamba amewahi kupewa nikaona utendaji kazi,ubunifu kama Tunavyoona akina LUKUVI alipoingia katika wizara ya Makazi.

Kwa kuwa wote tunatafuta mkono uingie kinywani aendelee tu hakuna namna.
 
Huyu jamaa lawama zote nilikuwa siamini ila juzi alichokiongea Mwanza na wafanyakazi wa TANESCO ndio niliamini hakuna kitu pale
Aliongeaje kiongozi? Hiyo ya kutaja neno 'upuuzi' au?
 
Katika viongozi makini na wawajibikaji na Makamba huwa unamhesabu.

Huyu angepewa wizara ya michezo basi ila wizara ya Nishati chenga tupu.

Kwanza hakuna wizara ambayo makamba amewahi kupewa nikaona utendaji kazi,ubunifu kama Tunavyoona akina LUKUVI alipoingia katika wizara ya Makazi.

Kwa kuwa wote tunatafuta mkono uingie kinywani aendelee tu hakuna namna.
Ni kwa vile ni vigumu kumridhisha kila mtu, kuna wenzako humu wamesifia sana utendaji wake alipokuwa wizara ya mazingira na muungano!
 
Hivi ukariri huu mnaoufanya wa kuhujumiwa JNNP mkaririshaji wenu nani?!!!!! Maana naona hamna hoja sasa isipokutema huo ushuzi. Walinda legacy mmekaririshana huo upuuzi na bila aibu mnautema popote pale hadi watoto wadogo wanakushangaeni wakati mwingine.
Nina uhakika hujui chochote kinachoendelea huko zaidi ya kukaririshwa tu......
Post clips za Nini kinaendelea HUKO!!

Mara ya Mwisho clip ilionyesha Jk na Mwinyi wameenda ki ziara kule!!!

Nakukumbusha kuwa mradi ule ulipaswa kukamilishwa mwaka huu na kazi ianze!!Mbona KIMYA!!?

Mara kumebomoka!!mara crane!!maneno ni Mengi Sana!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA!!!
 
Mimi sijamtaja kwamba ni mwizi, maana hapo nitakuwa natumia hisia. Lkn uongo wake kuhusu mradi wa JNHEP mimi sitamsamehe kamwe. Hawezi kuhujunu legacy ya taifa akaangaliwa tu.
Kama ni hivyo, basi sasa ngoja tushauri awe anakwenda na makamera na makelele meeengi pale mradini kila siku ili ajiondokee na shutuma hizi!
 
Mwambie Makamba, hiyo kazi ya Sales and Marketing manager ya Taifa gas anayoifanya atumie fedha za kampun iliyomuajiri, aache kutumia fedha zetu, kodi zetu zina matumiz muhimu na zinapatikana kwa shida sana, aache mara moja
 
Ogopa sana nchi kutumika kwa maslahii ya mtu binafsi hata kama ni mfanyabiashara mkubwa kiasi gani huwaga inakua na mwisho mbaya sana... ROSTAM kasaini mkataba wa gas mbele ya Mama sijui kama nchi inafaidika vipi ila naona imekaa vibayaa.. leo hii waziri anaanza kugawa mitungi ya taifa gas sasa je ni mradi wa nani??? serikali ina percent ngapi?? isijekuwa ya kigwangala kutumika QNET watu wakapigwaa... unamgawia mtungi mtu hiyo taifa gas ikiisha naenda kujaza wapi??? na ana hela ya kujaza?? gas sio 1000 hapo ndo utaona suala la matumizi ya mkaa yatarudi palepale na motive ya hii program imekaa kimaslahi zaidi ya kanjibai
 
Post clips za Nini kinaendelea HUKO!!

Mara ya Mwisho clip ilionyesha Jk na Mwinyi wameenda ki ziara kule!!!

Nakukumbusha kuwa mradi ule ulipaswa kukamilishwa mwaka huu na kazi ianze!!Mbona KIMYA!!?

Mara kumebomoka!!mara crane!!maneno ni Mengi Sana!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA!!!
Mradi mkubwa kama ule ndg makadirio ya kukamilika kwake huwa kunaendana na 'if all factors will remain constant'. Sasa tuulizane kiongozi; je, tangu ilipotoka ahadi hiyo, kila jambo lipo vile vile?!!!

Ushahidi wa hili upo pia ktk kuchelewa kwa mabarabara, madaraja n.k na imekuwa hivyo, kwa kumbukumbu zangu katika vipindi vyote va uraisi. Daraja la mto wami limechelewa, sgr imechelewa, vivuko vilichelewa n.k mbona sisikii au sikusikia matusi mengi kwa mawaziri wa huko?!!!!
 
Back
Top Bottom