TAFAKURI YA TAFAKARI YA BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA (TEC)
ILILOTOLEWA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 15 TAREHE 2025

Mwandishi,
H.M Mponda (Msema Kweli)
MA, Digital International Relations & Diplomacy
Mtanzania Mzalendo.
Utangulizi.
Ndugu Watanzania wenzangu, panapotokea jambo zito katika taifa ni busara watu kukaa na kutafakari wamefikaje katika jambo hilo kwa akili huru na uzalendo wa kweli pasina huba wala chuki. Nikiwa Mtanzania niishiye nje ya nchi, nimekuwa nikifuatilia yanayotokea nyumbani na kuona mwelekeo hasi ambao kama haukuwekewa breki, taifa letu linaweza kuendelea na maumivu ambayo tumeshayapata.
Kile kiitwacho “TAFAKARI YA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA (TEC) JUU YA YALIYOTOKEA SIKU NA BAADA YA UCHAGUZI -2025” kimetolewa baada ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kulihutubia bunge wakati akilizindua bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo ni kulihutubia taifa. Kwa hiyo mantiki inatujulisha wazi kuwa kiitwacho “Tafakari ya TEC” ni jibu kwa hotuba ya Mheshimiwa Rais tena jibu linalotoka kwa Wahashamu Maaskofu ambao husikika wakisema “Mamlaka Zote za Binadamu Zimetoka Kwa Mungu”. Kwa hivyo zinafaa kutiiwa.
Nitangulize kusema nawapongeza Baraza la Maaskofu kwa kutambua kuwa nchi yetu ina mamlaka na ndiyo maana wakaandika “Mamlaka Zinazohusika”. Lakini jambo unaloweza kuanza kuliona ni jinsi gani “Tafakari ya TEC” ilivyoepuka kuitaja hotuba ya Mheshimiwa Rais hata mara moja katika tafakuri yao. Katika elimu ya diplomasia hiki hujulikana na “silent protest” ambayo ni aina ya “ukosefu wa utii kwa mamlaka lakini pasina kutumia nguvu”. Mwelekeo huu wa ukosefu wa utii kwa mamlaka umekuwa unaonekana wazi kutoka kwa Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) na baadhi ya viongozi wengine wa dini ya Kikristo nchini akiwemo Mchungaji Josephat Gwajima, Askofu Bagonza na wengine hata kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Maaskofu wa TEC walifikia kutoa matamko ya Kifalsafa kuhamasisha wananchi wasishiriki uchaguzi kupitia Katibu Mkuu wa TEC Padri Dkt Kitima pale ambapo siku chache kabla ya Oktoba 29 alizungumza hadharani akisema “Maaskofu hawakwambii uende au usiende kupiga kura. Fuata dhamira yako inakwambia nini kama raia”. Katika mazngira ya uchaguzi wa mwaka huu yalivyokuwa, kauli hii ikitoka kwa Baraza la Maaskofu ni maelekezo ya wazi kwa waamini wao kwamba wasiende kupiga kura.
Mwenendo wa Maaskofu wa TEC wakati wa kuelekea uchaguzi na hata baada ya uchaguzi inaonesha wazi Maaskofu hao wamechukua nafasi ya kisiasa ya kuwa wa walalamikaji badala ya kutokuwa na upande ili wawe wapatanishi kwa sababu maandiko Biblia yao yanasema “Heri 2 Kwa msimamo ambao umeoneshwa na Maaskofu wa TEC dhidi ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tangu wakati wa kilichoitwa Sakata la DP World kuhusu Bandari ya Dar es Salaam, ni wazi hawafai kuwa wapatanishi walio huru kwa kuwa hata katika kadhia hii ya uchaguzi 2025 tayari wanao upande, ule wa vyama vya upinzani.
Yatokanayo na Tafakari ya TEC
Ukiupitia kwa makini waraka wa “Tafakuri ya TEC” utapata maswali mengi sana kuliko majibu kwa jinsi ambavyo waraka huo umeonesha wazi TEC imekusudia kuufanya utawala wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uwe mgumu kwa sababu ambazo tutazieleza baadae.
1. Hakuna Kauli ya Kuzungumzia Hotuba ya Mhe. Rais
Kila mwenye busara angetarajia kusoma angalau hata ibara moja ikizungumzia hotuba ya Rais aliyoitoa kwa taifa wakati akizindua bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Ijumaa Tarehe 14 Novemba 2025. Lakini cha ajabu hakuna hata sehemu moja katika “Tafakari ya TEC” iliyozungumzia hotuba hiyo muhimu kwa taifa ambayo iliweka wazi Serikali itafanya nini kuhusu mambo ambayo “Tafakari ya TEC” imeyangumzia kuanzia maridhiano, uchunguzi wa kilichotokea Tarehe 29 Oktoba, mabadiliko ya katiba na mengine mengi muhimu kwa taifa. Ni kama vile Maaskofu wa TEC wamesema kimya kimya “Tumekusikia lakini hatuvutiwi na lolote kutoka kwako” huku hotuba hiyo ya Mhe. Rais ikipongezwa kila Mtanzania Mzalendo, mwenye akili timamu na busara kuwa ni hatua ya kwenda kuliponya taifa.
2. Haki ya Wananchi Kuandamana
“Tafakari ya TEC” iliandika chini ya ibara “KILA MAANDAMANO SI UHALIFU kwamba “Kuandamana ni haki ya raia kama njia ya kufikisha ujumbe au malalamiko ikiwa njia ya mazungumzo imeshindikana. Cha msingi yawe maandamano ya amani. Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania inatambua haki ya kufanya maandamano ya amani. Rejea Ibara ya 20 (1). Kisha Tafakari ya TEC ikaendelea “inasikitishakuona kuwa waandamanaji waliojitokeza siku ya uchaguzi wote waliwekwa katika mwavuli wa uhalifu. Adhabu ya mwandamanaji siyo kuuawa”. Ni kweli kuwa (1) Kila maandamano si uhalifu (2) kuandamana ni haki ya raia kwa mujibu wa katiba ibara waliyoitaja (3) Maandamano yanapaswa kuwa ya amani. Jambo ambalo Maaskofu wa TEC wanapaswa kulizingatia ni kwamba “There is no right without obligation” – hakuna haki isiyo na wajibu. Kama waandamanaji wanayo haki ya kuandamana, na wao wanawajibu wa kutekeleza wakati wa maandamano yao kwa mujibu wa Mkataba wa KImataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa - “International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR)”-kulinda usalama wa taifa, utulivu wa jamii na kuzuia vurugu na chuki. Lakini tafakuri yetu inatuachia maswali ya kuwauliza Maskofu wa TEC.
Je, yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025 yalikuwa maandamano au vurugu na mapambano? Kama maana ya maandamano kwa Maskofu waliofanya sala na maombi kabla ya kuandika “Tafakuri ya TEC” ni yale mambo yaliyofanywa na wanaowaita “Waandamanaji” -kuchoma mali za watu binafsi na zile za umma, basi kuna shida kubwa kwa viongozi hawa wa dini au kuna chuki kubwa 3 iliyojificha dhidi ya serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa sababu najua kwa usomi wao wanayajua vizuri yote haya.
Ni kweli maandamano si tu haki ya raia kwa mujibu wa kikatiba ya nchi. Lakini pia tuwafahamishe Maaskofu kwamba kwa mujibu wa “International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR)”-kifungu cha 19, kinatoa haki ya uhuru wa maoni na kujieleza. Lakini pia kifungu hicho hicho kinawekea kikomo uhuru huo na kwamba “unaweza kuzuiliwa kwa sababu za: - Kulinda usalama wa taifa, Kulinda utulivu wa jamii na Kuzuia vurugu au chuki. Ni haki na wajibu wa mamlaka za nchi kuzuia hata maandamano kama yatakwenda kinyume na kifungu hiki cha ICCPR. Sasa tuwaambie Maaskofu wa TEC na wengine wanaowaunga mkono, hata kama Tarehe 29 Oktoba kungekuwa na maandamano halafu Serikali ikaona kuwa kuna tishio kwa usalama wa taifa au kuvuruga utulivu wa jamii, kuzua vurugu na kupandikiza chuki, basi Serikali ingepaswa kuyazuia maandamano hayo.
Si hivyo tu bali kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa( UN Resolution 1624) la mwaka 2005 linakataza uchochezi wa ugaidi na ghasia za kisiasa. Lakini pia Mkataba wa Roma “Rome Statute of the International Criminal Court (ICC) unasema wazi kwamba “Uchochezi wa ghasia, uharibifu mkubwa au uhalifu dhidi ya ubinadamu unaweza kuchukuliwa kama makosa ya jinai ya kimataifa iwapo athari zake ni kubwa”. Sasa tuwaulize Maaskofu wa TEC na wengine wanawaunga mkono, je tarehe 29 Oktoba kulikwa na maandamano au ghasia, vurugu, uharibifu mkubwa na uhalifu dhidi ya binadamu?
Maandamano yoyote yale kwa mujibu wa sheria za Tanzania, ni lazima yakidhi mashrti ya kisheria ikiwa ni Pamoja na kuandika barua kuwajulisha jeshi la polisi, kw anini wanaandamana, kupata kibali, kuelezea njia watakayopitia na wapi maandamano hayo yataishia. Kawaida maandamano huwa na Kauli Mbiu (Slogan) na mabango ya ujumbe huo. Je hayo yalikuweko Tarehe 29 Oktoba.
Hata viongozi wa Chadema walikana kuhusika kuandaa maandamano hayo. Je athari za kiitwacho ‘maandamano’ na Maaskofu wa TEC zilikuwa ndogo au kubwa? Kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifah apo juu ni nani anapaswa kutuhumiwa kwa makosa ya jinai kimataifa? Ni Serikali au waliopanga na kuchochea machafuko hayo ya Otoba 29? Jambo moja ambalo tunaweza kukubaliana na Maasofu wa TEC ni kwamba vyombo vyetu vya usalama navyo vilitumia nguvu kubwa (unproportional force) na hii ni kutokana na ukweli, kuwa na wao, kama ambavyo kila Mtanzania alivyopigwa na butwaa, maaskari wetu hawakuzoea vurugu kubwa kama hizi zilizoratibiwa na nguvu ilokuwa gizani zitokee kwa wakati mmoja nchi nzima. Ni wazi kuwa na wao wanapaswa kujifunza jinsi ya kukabiliana na machafuko kama haya kwa nguvu stahili.
3. Kulaani Mauaji ya Wavurugha Amani na Uslama wa Nchi
Ni ukweli usiopingika kwamba kupotea kwa uhai wa mwanadamu yeyote yule, hata awe mwandamanaji haramu, ni chukizo kubwa mbele za Mungu na wanadamu wote. Kama taifa tunaugulia kwa majonzi na ndiyo maana Mheshimiwa Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, akawataka wabunge na wote waliohudhuria ufunguzi wa bunge Tarehe 14 Novemba 2025 kusimama kwa dakika moja kuwakumbuka waliopoteza maisha yao katika vurugu hizo ambao ni raia na hata askari polisi na wengi wa waliouawa waliingizwa tu katika mkumbo.
Lajini swali la kujiuliza, kama Maaskofu wa TEC wanauchungu kiasi hichi kwa mauaji ya raia kwa ghasia za uchaguzi, walikuwa wapi mwaka 2001 pale Wazanzibari hasa Wapemba walipouawa, kujeruhiwa na wanawake kubakwa? Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu (International Human Right Watch) liliripoti watu 35 kuuawa huko Pemba mwaka 2001 huku Chama cha wananchi (CUF) kikitoa idadi ya watu 67 zaidi ya 1,000 kujeruhiwa. Ni tukio baya liliwafanya watanzania wenzetu kuwa wakimbizi nchini Kenya.
Kwa nini hatukuona Tafakari ya TEC kulaani mauaji hayo kama hii ya sasa? Au waliouawa wakati ule hawakuwa binadamu Watanznaia kama hawa waliouawa safari hii? Je ni kwa sababu waliouawa ni Wapemba na Waislamu au pengine kwa kuwa Rais wa wakati huo alikuwa muamini wao (Benjamin William Mkapa) na Rais huyu wa sasa si muamini wao? Mauaji ya Pemba 2001 yalimfanya hata Rais Mwendazake Benjamin William Mkapa, kujutia kama alivyoeleza mwenyewe katika kitabu chake “Maisha Yangu, Dhamira yangu”. Mababa aaaskofu wa TEC kulikoni undumilakuwili huu? Je hiyo ndiyo haki mnayoihubiri?
4. Kutoa Maagizo kwa Serikali
Tafakari ya Maaskofu wa TEC chini ya ibara “Nini Kifanyike” inaandika “Taifa letu limeumizwa na ni hatari linaweza kugawanyika zaidi. Sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania tunashauri wale wenye dhamana ya kutuongoza wazingatie mambo yafuatayo ili kuepusha vurugu na mauaji yasitokee tena:
Katika waliyoyashauri, mambo mawili yanajipamabanua ambayo ni jambo la (2) lililokuwa KUWAJIBIKA. Hapo Maaskofu wakataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wote waliohusika na mauaji WAWAJIBIKE au KUWAJIBISHWA na mamlaka zao za uteuzi na jambo la (3) UCHUNGUZI ambapo “Tafakari ya TEC” ilishauri ufanyike uchunguzi utakaowashirikisha wadau wa NDANI na NJE na watoke kwenye tume huru isiyofungamana na upande wowote kama jumuiya na taasisi za Kimataifa, Taasisi za dini, Asasi za Kiraia na Wataalamu wa haki na mambo ya Kidemokrasia.
Ni ushauri murua lakini unaacha maswali yafuatayo – kwa nini Maaskofu wametaka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wote waliohusika na mauaji katika Serikali ndiyo pekee wawajibishwe au wawajibike? Je kabla ya uchunguzi utajuaje mkosaji ni nani? Je wale waliokuwa wakichochea maasi, vurugu na uvunjifu wa usalama na amani kwa miezi kadhaa kabla ya uchaguzi hadi kufikia kusema hadharani Oktoba 29 “TUTAKINUKISHA TENA TUTAKINUKISHA KWELI KWELI, maaskofu wa TEC wanasema wachukuliwe hatua gani?”. Maaskofu wa TEC hawakuona kuwa na hawa ni wauaji wa vijana wetu kwa mujibu wa sheria za kimataifa tulizozieleza awali? Kwa nini undumilakuwili huu kwa Maaskofu ambao wanajitapa kuhimiza watu watende haki?
KWA NINI MAASKOFU TEC WANAFANYA HIVI?
Kanisa Kupoteza Udhibiti wa Bandari ya Dar es Salaam.
Awali tulisema tutaeleza tunachokifikiri kuwa sababu za Maaskofu wa TEC kuonesha chuki ya wazi kwa utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Kwa tafakuri yetu, awali Maaskofu hawa walionesha kuufurahia ujio wa Rais Dkt Samia Namara moja wakaomb akukutana nae. Lakini Serikali yake ilipokuja na maamuzi ya kukabidhi uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa 5 kampuni ya DP World kutoka Dubai, hapo Maaskofu wa TEC wakatokwa na nyongo wazi wazi. Sote ni mashahidi jinsi Maskofu hawa walivyotumia madhabahu zao kupinga ujio wa DP World.
Waraka wa Baraza la Maaskofu katoliki ulitolewa Agosti 18,2023, kupinga mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai na ukasomwa katika makanisa ya Katoliki nchini kote Jumapili ya Tarehe 20 Agosti 2023. Lakini ni kwa nini Kanisa Katoliki lilishupaa kupinga DP World isipewe mkataba wa kuendesha bandari ya Dar es Salaam Pamoja na faida za kiuchumi za mkataba huo kama ilivyodhihirika kwa faida kubwa inayopatikana hivi sasa? Moja ya sababu ni Kanisa kuhisi chini ya uangalizi wa DP World, halitoweza tena kuitumia bandari ya Dar es Salaam kwa maslahi yake kama awali kwani Kanisa hilo limekuwa likiitumia bandari ya Dar es Salaam kwa kuingiza mali za Kanisa n ahata Maaskofu binafsi kwa kushirikiana na wafanyabiashawa wao.
Julai 20 mwaka 2023 Dkt. Wilbroad Slaa, ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) alipata kusema hadharani kwamba “Silaha zilikuwa zinaingizwa nchini kwa jina la Kanisa”. Kama hali ndiyo ilikuwa hivi, unadhani watafurahia bandari hiyo kuwa chini ya wasimamizi kama DP World ambao Kanisa halina ushawishi au udhibiti nao? Kupoteza udhibiti wa Bandari ya Dar es Salaam ni moja ya sababu kubwa za chuki ya Baraza la Maaskofu Katoliki kwa utawala wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Hawa wana maumivu katika kubinafsishwa Bandari ya Dar es Salaam na hawajasahau kwa sababu kufanya hivyo kumewakosesha misamaha ya kodi na kuingiza bidhaa kwa maslahi ya Maaskofu
Serikali Kuboresha Huduma za Jamii
Tangu ukoloni, Kanisa Katoliki limekuwa mtoaji mkubwa wa huduma za kijamii kama vile elimu ya shule, elimu ya vyuo vikuu na vyuo vya kazi, shule za ufundi na huduma za afya hata kuliko serikali. Mwaka 1992, Makanisa ya Kikristo nchini kupitia Kamisheni ya Kikristo ya Huduma za Jamii yaani Christian Socvial Services Commission (CSSC) yaliingia Mkataba wa Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) na Serikali ya Tanzania.
Katika Mkataba huo uliotiwa saini wakati Mwendazake Edward Lowassa alipokuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu wa Tanzania, Serikali ilitakiwa kutoa fedha, wahadhiri, wataalamu na kila aina ya misaada kwa vyuo vikuu na hospitali za Makanisa. Wakati huo Makanisa yalikuwa yakitoa zaidi ya asilimia 40 ya Elimu ya Vyuo Vikuu na Hospitali zikiwemo Hospitali za Rufaa nchini.
Sasa hali imebadilika.
Tangu utawala wa Rais Mtaafu Kikwete, Mwendazake John Magufuli na sasa Dkt Samia Suluhu Hassan, Kanisa linahisi kubanwa mbavu katika huduma za Jamii za elimu ya chini, elimu ya kati, vyuo vikuu na huduma za afya. Ujenzi wa Shule za Sayansi kila Mkoa pamoja na Uboreshaji wa Shule Kongwe na Bora za Serikali zimepelekea kupungua Kwa Ushawishi wa Wazazi kupeleka Wanafunzi kwenye Shule zao
Kwa Sababu huduma bora zimeanza kuapatika katika shule za Serikali pamoja na Ufaulu mkubwa unaoongezeka mwaka hadi mwaka. Shule za Seminari zilizokuwa zikitamba sasa zinakabana koo na zile za Serikali katika shule kumi bora. Katika huduma za afya, ujenzi wa vituo vya zahanati kila kijiji na vituo afya kila Kata kwa kipindi cha Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo amejenga Vituo vya Afya visivyopua 2500, Ujenzi wa Hospital za Wilaya takribani 187, Huduma za Madaktari Bingwa Kwa hospitali zote za Rufaa za Serikali, Ununuzi wa Vifaa vya MRA kutoka hospitali mbili 2 tu Bugando na Muhimbili mpaka sasa Mikoa 26, Huduma za CT Scan kutoka Hospital mbili mpaka -Bugando na Muhimbili, hadi sasa Mikoa 26.
Huduma hizi zote zimeua soko la Zahanati na Vituo vya Afya vya Kanisa. Kanisa lililalamika Sana utaratibu wa Serikali kujenga Hospital au Kituo cha Afya wakati wao wameshajenga katika eneo hilo hilo kwamba inavunja Mkataba wa Maridhiano (MoU) wa mwaka 1992. Malalamiko haya walikwisha mwambia aliyekuwa Waziri wa Afya Mstaafu Dr. Seif Rashid aliyekuwa Mbunge wa Rufiji katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Madaktari wa Kanisa katoliki uliofanyika Msimbazi Centre-Dar es Salaam, pia Mkutano na Viongozi wa Madaktari katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Jimbo Kuu la Tabora pia waliendelea kulalamikia jambo hilo sambamba na kuulizia ile ruzuku ya asilimia 20 kutokana na MoU ya 1992 haipelekwi wenye Hospitali zao Teule.
Waliomba pia kuongezwa ruzuku hiyo ya Serikali kwa Hospitali za Makanisa kutoka asilimia 20 hadi asilimia 40. Maombi hayo waliyafikisha kwa aliyekuwa Waziri wa Tamisemi kipindi hicho Mhe. Innocent Bashungwa naye akayakubali na kumkabidhi aliyekuwa Naibu Katibu Tamisemi kipindi hicho kwa utekelezaji lakini inaelekea Serikali haiyatekelezi. Kudhibitiwa kwa matumizi sahihi ya malipo ya fedha ya watumishi wa Serikali waliopo katika Haspitali Teule za Kanisa kulikopelekea kuzuia fedha zilizokuwa zinatumika vibaya kulipia mishahara wachungaji mpaka hata Maaskofu. Kuna lile Jambo la Mhasibu mmoja kujirusha kutoka ghorofa ya nne na kufariki kutoka katika Hospital moja Rufaa Teule ya Kanisa iliyopo kanda ya ziwa kulitokana na “Payroll” aliyokuwa anaziandaa za ulipaji wa mishahara hewa ya madaktari bingwa takribaini 40 waliokuwa wanapelekea kutumia Shilingi Milioni 400 hewa kwa Mwezi!
Kwa hatua hizi za Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni wazi haiwezi kupendwa na Maaskofu hawa kiasi kwamba fursa yoyote ya kumkwaza wataitumia. Tunapata shida bure. Maaskofu walianza hoja ya uchaguzi hauna uhalali tangu wakati wa funga yao ya Novena Ushauri wa Bure kwa Maaskofu TEC Tuwashauri bure Maaskofu wa TEC na wengine kama wao waache kuihujumu Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sababu hata wasio waislamu wanakiri maisha yamekuwa na ahueni kubwa kwa maisha yao. Tunawashauri wawe “Wapatanishi” badala ya kuwa “Wachochezi” wa wanaoipinga Serikali.
Kwa kutokulaani kwao machafuko na vurugu kunawapa ujasiri wale wapingao Serikali na haya tunayashuhudia kwa “Likes” zilizoko katika mitandao ya kijamii kwa wanaosoma matamko ya Maaskofu. Ni bora Maaskofu na viongozi wengine wa dini wajifunze “Kuwa sehemu ya Ufumbuzi wa Matatizo ya Taifa letu na siyo kuwa sehemu ya matatizo hayo”. Kama taifa tunao uwezo wa kuzungumza na kutatu amatatizo yetu kwa njia za mani na siyo kuchochea vurugu chini ya mwavuli wa KUTETEA HAKI NA DEMOKRASIA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA - AMEEN
Soma: PostGE2025 - Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC): Mauaji ya Oktoba 29 yachunguzwe na Taasisi huru zisizoegemea upande wowote, ikiwemo za Kimataifa