Tafuta hela uheshimishe familia yako

Tafuta hela uheshimishe familia yako

Ukiwa na hela hata nguvu ya kuandika hasira zote hizo hutakua nazo. Cha msingi heshimisha familia yako kwa kuwa na mkwanja hayo mengine ni kelele tu zisizo na msingi.

Tajiri namba moja wa muda wote Suleiman alikuwa anaandika sasa wewe kapuku ambaye umebahatika Kupata hicho kimshahara ambacho hakifiki 1M na kinategemewa na ukoo mzima, alafu unasema ATI Watu wasiandike.

Unafikiri kila MTU ni mjinga asiyependa kuandika na kusoma kama wewe?
 
Screenshot_20230722-053856.png
 
Anaandika, Robert Heriel

Moja ya mambo yaliyonifanya nisome wakati ni mdogo, na sasa nahangaika kutafuta pesa ni suala la matukio ya misiba. Kwa kweli Taikon niliapa na katika hilo Mungu anajua, na atalisimamia yakuwa mke na watoto wangu kamwe hawataosheshwa masufuria na kutumwa tumwa bila adabu. Mke na watoto wangu lazima waheshimiwe, na hilo nitalifanya mimi mwenyewe ningali hai.

Kama ilivyo ngumu mimi kufanyiwa ujingaujinga ndivyo iwe hivyohivyo kwa mke na familia yangu. Unajiuliza leo nazungumzia nini?

Iko hivi; hakuna kitu kinauma kama mmeenda kwenye msiba halafu unaona mkeo au watoto wako wanatumwa tumwa na kufanyishwa makazi huku wake na watoto wa wenzako wakipiga tuu stori na kuagizwa kazi kwa adabu. Inauma! Inauma! Hasa sisi Watibeli jambo hilo tunajua linauma na ndio maana hatutaruhusu litokee kamwe.

Ni bora mtu asiende kwenye huo msiba. Hiyo kwetu ni bora, lakini kamwe hatutakubali mke na watoto wangu wahenyeshwe.

Sitaki mke wangu atumwe tumwe, sitaki watoto wangu watumwe tumwe bila adabu. Kama vile ambavyo hamuwezi kunituma tuma mimi na hamkuweza kunituma tuma mimi ndivyo hivyohivyo mtafanya kwa familia yangu. Dharau hazivumiliki.

Unakuta mama wa watu ameolewa labda mumewe kwenye hiyo familia ni maskini au tuseme anakipato duni, basi kwenye msiba atatumikishwa kama punda.

Kwenye kuchambua mchele yupo, hajamaliza utakuta anakuja mtu mwingine anamtuma akajaze maji kwenye pipa kwani tayari yamenunuliwa, anaacha kupembua mchele anaenda kuchota maji, akiwa huko amebeba ndoo saba anaambiwa na mwingine amalizie kwani wali unatakiwa kupikwa ajili ya wageni ambao wapo njiani, hajakaa vizuri anaambiwa masufuria yanatakiwa yasiribwe mchanga ili yasipate moshi.

Hajakaa vizuri, anatakiwa kusafisha vyombo vya mchana, halafu unakuta muda huohuo kuna wanawake kwa makumi wamekaa sebuleni au ukumbi wa msiba wanapiga stori. Ati wamependeza, ati wametoka Daslama, ati wametoka ng'ambo huko ughaibuni kwenye nchi za barafu. Kudadadadeki, mke wangu na binti zangu hujawatuma, labda kama sio familia yangu. Nasema hivi; labda sio familia yangu.

Mkewangu awe amesoma au hajasoma, hamuwezi kumfanyia hivyo. Awe mzuri au mbaya kulingana na macho yenu, hamuwezi mfanya mtumwa wenu. Awe na kazi au hana, haiwezekani kufanyiwa hayo. Kitendo cha kuwa mke wa Mtibeli hiyo ni hadhi ya juu kabisa ambayo anastahili kuheshimiwa.

Iwe Taikon nimechanga mchango mkubwa au mdogo, nimesoma au sijasoma, ninakazi au sina, kamwe haitowezekana mke na watoto wangu kuwa watumwa kwenye matukio ya misiba au ya sherehe.

Hakuna yeyote chini ya hii Dunia ambaye kwenye matukio ya namna hiyo ambaye anatakiwa kumgeuza mkeo na watoto wako kuwa watumwa. Hakuna. Na kamwe sitakubali na haitotokea mke wangu na watoto wangu wakageuza watu wengine kuwa watumwa na kuwadharau katika matukio ya misiba na sherehe kwa sababu sisi Watibeli hatupo hivyo. Sisi ni watu wa Upendo, Haki, ukweli na Akili.

Mkifika kwenye msiba wekeni taratibu, kila mtu atoe na kujitoa kadiri ya alivyowiwa. Msitake kufosi mambo makubwa ili yawe mizigo kwa watu wengine.

Mwenye milioni kumi akatoa milioni moja na mwenye laki moja akatoa elfu kumi wote wametoa sawa. Yupo atakayetoa kwa kuwiwa na mapenzi na yupo atakayetoa kwa sifa na kwa vile anavyo.

Mke afanye kazi vile moyo wake unavyotaka. Sio ajilazimishe au alazimishwe, hiyo sio Haki. Huo ni unafiki ambao sisi Watibeli ni jambo baya na linalofanywa na watu wa hovyo.

Kama mke na watoto kwa hiyari yao watataka kusafisha masufuria na kuwa wapishi bila kuangalia wengine wakiwategea au kuona ndio kazi inayowahusu (labda kwa vile wametoa mchango mdogo) basi hilo sio kosa kwa sababu ni hiyari ya mke na watoto wangu.

Kutoka kwako Dar au Ulaya na kuchanga pesa nyingi hakukufanyi uwanyanyase na kuwatesa wake na waume wa ndugu zako. Ni bora usitoe tuu hakuna kitakachopungua. Ni bora nisitoe mchango mkubwa ikiwa nitautumia mchango huo kuwanyanyasa wengine.

Nazungumzia unyenyekevu ambao ni sehemu ya Upendo. Kutojiona bora kuliko wengine.

Kama mimi na familia yangu sijioni bora kuliko wengine basi vivyohivyo siwezi ruhusu mtu ajione bora kuliko mke na familia yangu.

Vijana, na wote msomao ujumbe huu, kamwe usiruhusu yeyote akudharau. Kumbuka dharau ipo kwenye uovu. Yaani kama utafanya uovu na maasi au uhalifu basi utadharauliwa lakini hakuna dharau kwenye kuwa na kipato kikubwa au kidogo, hayo ni majaliwa.

Kuwa mtupi au mrefu, kuwa mweupe au mweusi, kuwa mzuri au usiye na sura ya kuvutia, yote ni majaliwa. Mtu asikudharau wala kuidharau familia yako Kwa mambo hayo. Hivyo ndivyo kuishi kwa kuheshimiana na kupendana.

Wewe ukiwa na pesa ni wewe na familia yako huko. Ukija nyumbani kwenye msiba pesa zako hazina maana yoyote isipokuwa moyo wako. Kama utataka unyenyekewe ili utoe hizo pesa hilo futa akilini mwako.

Tutafanya msiba wa gharama inayoendana na mioyo ya watu. Hatutahitaji sifa zisizo na maana yoyote. Lengo ni mpendwa wetu apumzike kwa amani na sio kumnyenyekea yeyote.

Halikadhalika na kwenye harusi na mambo mengine.

Hivyo ndivyo Taikon Master ninavyomaliza ujumbe huu ukiwa na usia kwa wana na binti za Tibeli.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Utafutaji wa pesa uko overated ndo maana siku hizi binadamu tunakufa mapema.
 
Mods ingefaa mrejeshe kishwa cha uzi kama kilivyokuwa.
Niliyeandika ninajua nilitaka wasomaji wapate ujumbe upi.

Hicho kichwa kimepotosha maana nzimavya nilichoandika
 
Tajiri namba moja wa muda wote Suleiman alikuwa anaandika sasa wewe kapuku ambaye umebahatika Kupata hicho kimshahara ambacho hakifiki 1M na kinategemewa na ukoo mzima, alafu unasema ATI Watu wasiandike.

Unafikiri kila MTU ni mjinga asiyependa kuandika na kusoma kama wewe?
Sijakataza ww kuandika ila nimekwambia ukiwa na hela utapunguza hayo makasiriko ulioandika. Nakuona mfalme njozi ushaota nimeajiriwa 😂😂😂😂 dogo simtumikii mtu yoyote hapa duniani kiufupi sina boss na hakuna wa kunilipa 😂😂😂
 
Hizo kazi nafikiri watu hawafanyi kama hawana masilahi nazo,maana matukio kama misiba yanawapata watu wote,Sasa wewe ukiwa unachanga Hela TU halafu kwenye nguvu kazi hutaki kuwajibika,likitokea kwako watu watakuchangia Hela na nguvu kazi hawatahusika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo ndio ukae kama sanamu,msiba ni kusaidia shughuli.
Hata ukiwa na hela usipo ungana na wenzio katika kusaidia kazi hakuna umaana wa kwenda kwenye huo msiba

Huwezi elewa nazungumzia nini.
Ukisoma soma Kwa ufahamu na sio Kutumia Viungo visivyo Sahihi.
 
Sio kweli, pesa au utajiri sio sababu ni Heshima na uoga wa KINAFIKI TU.

Kuna mzee mmoja hana pesa hakuwahi kuwa na pesa za maana lakini aina ya maisha anayoishi, ilikuwa ni ngumu sana kumuendesha kumdharau wala familia yake na watoto wake. Ni mtu wa haki haki na mwenye misimamo kweli kweli bila kujali mahali alipo, cheo wala sura ya mtu, hana uwoga wowote wala uonevu wowote ule ni haki haki mpaka leo mtaani masikini kwa matajiri wanamuogopa na kumuheshimu sana na familia yake.

Nakubaliana na mtoa mada pesa sio sababu kabisa ni heshima na Uoga wa kinafiki tuu.
Sikupingi ila ukiwa na misimamo bila kipato unaonekana zezeta.
 
Hizo kazi nafikiri watu hawafanyi kama hawana masilahi nazo,maana matukio kama misiba yanawapata watu wote,Sasa wewe ukiwa unachanga Hela TU halafu kwenye nguvu kazi hutaki kuwajibika,likitokea kwako watu watakuchangia Hela na nguvu kazi hawatahusika.

Sent using Jamii Forums mobile app

Na wengi inawatokea hivyo. Wanawapa shida Watoto au Ndugu ambao wanaishia kuomba Msamaha
 
Ungekuwa na hela usingepata muda wa kuandika maupumbavu marefu namna hii. Hamna mwenye hela wa namna hii. Tafuta hela uache pumba na kelele
 
Kiufupi kama huna mkwanja familia yako itadharaulika hatakama unamisimamo. Vitoto vyako vitaonekana vichafu vichafu lazima vitatumwa mkeo kaja kavaa masampula lazima akachoteshwe maji na ikiwezekana atachimbishwa hadi kaburi. Mleta mada maeneo kama msibani ukishaona watu fulani wanajitenga ondoka hapo kajitafutie chimbo ujifiche ww na vitoto vyako usivyotaka vitumwe. Mwenye hela akiona wife wake anatumwa sana utaskia hebu chukua funguo nenda na watoto njini kawatafutie masweta ya kuvaa akiondoka unamtext hebu kale alafu watembeze watoto kazi zikiisha ntakustua. Inarahisisha mtu kutochoka na kulimbikiziwa makazi kibao. Ila fanya hivyo ukiwa na mkwanja kama ww ni hohe hahe toa mchango wa nguvu zako na utoe kweli
 
Epuka kipato kidogo mkuu yaani ukishazidiwa mkwanja kwenye familia lazima utatumwa tu hata wanao wataonekana vinyamkera fulani

Pesa ni matokeo Mkuu.
Unaweza fanya kazi na ukawa na kipato kidogo au cha Kati.
Epuka kufanya kazi ikiwa lengo ni Kupata mapesa mengi. Pesa haijai.

Watoto wanaoonekana vinyamkera ni as wale wazazi ombaomba, wanaojipendekeza Kwa Ndugu wenye Pesa.

Ukishakuwa ombaomba na MTU wa kujipendekeza lazima uwe kinyamkera
 
Ungekuwa na hela usingepata muda wa kuandika maupumbavu marefu namna hii. Hamna mwenye hela wa namna hii. Tafuta hela uache pumba na kelele

Wewe sio kama NI fukara tuu Bali hata Akili hauna.
Ninaweza kukutajia mabilionea ambao wameandika vitu vingi na bado wanapesa.
Alafu kuna ninyi makapuku mnaojifanya mko busy alafu Maisha yenu ya taabu
 
Back
Top Bottom