DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wizi wizi wizi
Ndio maana kila mtu anataka kazi Tra sasa

Sasa kila mtanzania atataka akafanye kazi Tra,wanaweka pesa mpk kwenye makabati ya nguo nyumbani

Wengi wao watumishi wa Tra wanachezea sana pesa na wanawake
Tenaa mnooo yaaan
 
Dear kuna biashara nilifungua, jamani mchaka mchaka wa leseni, mapato, kodi, kitambulisho cha mfanya biashara.

Sasa biashara ilikua chini ya 1.6mil mbna hadi ilikufa, kwa week mara 2 mtu wao anapita kunikabaa.

Sasa aoneshee vyanzo vyake vya mapato ili watu wa tathimini hakuna tatizo. Aaah wee hawa wamezidi bhana, uliona wale wa kariakoo walivyo kuwa wanalia wanafata watu hadi nyumbani. Khaaaaah
 
Pia aeleze anafanya biashara gani ukizingatia ni mtumishi wa umma, tuna haki ya kujua
 
Labda kakopa, mfano Kama salary slip yake inasoma 3, milioni tsh,ana uwezo wa kuchukua 180 NBC au crdb akajenga kwa hatua
 
umejuaje hana kibali?
 
Too much f**k with people,kuwa TRA hapa ndio tatizo na wengi wakimwona mtu Yuko TRA na anafanya maendeleo basi Hela kazitoa humo Tena kwa wizi,Kuna watu wamefanya kazi makampuni binafsi huko anagali mayanki kabisa wakajipanga wakawekeza haafu sasa mwishowe wakaamua kutafuta heshima ya kufanya kazi sehemu nzuri au shirika la kiserikali lenye JINA.

Kuna watu wa sampuli hii.sio kila anayepiga hatua akiwa TRA basi Hela kazipatia humo.

But Kwa upande mwingine huko hakuna mishahara mikubwa.ipo chini sana,issue ni vitengo ,Kwa maana ya Fringe benefits,sio wizi.kuna watu huko wana TGS ambayo haifiki 1M ila mtu huyo unakuta Halali nyumbani mara Tano Kwa mwezi ni safari tu,hizo perdiem unafikiri atakua mwenzako?

Rizika na unachokipata ,haimanishi pia ukipata utaweza Fanya kama yeye.suala la maendeleo sio ukubwa wa kipato.Anza na ulicho nacho na Fanya busara kwenye uwekezaji na kuwa na nidhamu ya matumizi.Sio kila aliefanikiwa ni mwizi au mpigaji.
 
Sawa, ila usijitoe akili, kule wanabambikia watu kodi ili mkae pembeni mfanye mazungumzo, wanaumiza sana watu. wamchunguze tu, kwani kuna ubaya gani?
 
Sijawahi kuona TRA officer asiye na sura ya 'toa chochote Kitu' tangu nizaliwe na mikoa yote niliyoishi na hawa ndio wanatuweka kwenye list ya nchi zenye wapenda rushwa.
 
Sijawahi kuona TRA officer asiye na sura ya 'toa chochote Kitu' tangu nizaliwe na mikoa yote niliyoishi na hawa ndio wanatuweka kwenye list ya nchi zenye wapenda rushwa.
Kataa hiyo mentality ndugu yangu,Kuna watu waadilifu sana,na Wana mfanikio makubwa tu.

Ukiwa nje ni rahisi kuona hivyo,ukiwa ndani ni rahisi kuusoma mchezo.

Ntakupa mfano.Kwenye mabank Kuna mishahara midogo sana,lakini je mbona vijana wanapiga hatua?je wanaiba?na wanaibaje?
 
Sawa, ila usijitoe akili, kule wanabambikia watu kodi ili mkae pembeni mfanye mazungumzo, wanaumiza sana watu. wamchunguze tu, kwani kuna ubaya gani?
Ukibambikiwa Kodi nenda kashtaki,ukikubali kubambikiwa basi ni unyonge.kuna watu wanashindwa kufanya biashara Kwa sababu ya makadirio ya Kodi.Tatizo jingine watanzania hatupendi uwazi,unapewa grace period ,halafu ikifika muda wa kuonesha return ya biashara unambwela mbwela.Tatizo kubwa Lina anzia hapo.Ni ngumu kubambikiziwa Kodi,ukilipa kama inavyotakiwa huwezi kuja kutwa na deni la mamilioni,ukikwepa wakikufuma ndio lawama za kubambikiziwa

Labda niseme Kwa biashara zetu Kodi ni nyingi na zinaumiza,Kuna muda uaweza kuona kabisa Hela nyingi ni Kodi na faida ni kidogo Sana,unaacha kulipa Kodi,mwishowe unalimbikiza ukija kupewa invoice unashangaa,na huu ndio uhalisia Kwa wengi.

Ukiwa mzito wa kulipa Kodi,jaribu kuangalia biashara zisizo na utitiri wa Kodi na hutokumbana na kadhia ya Kodi za kubambikiziwa.


La mwisho,sio kila mtumishi wa TRA anahusika na Kodi.Ni mamlaka ya mapato,Ina vitengo vingi sana.Sio kila mtumishi w TRA anayefanikiwa mtaani basi yupo kwenye kitengo cha Kodi.Tuachane na hizi habari za kuwa brainwashed.
 
Jaribu wewe uone, yule aliyebambikiwa bilioni 30 kodi uliona kilichomtokea? Angekubali kuwapa rushwa wangemyondolea hiyo kodi, ila kwakuwa kajifanya kichwa ngumu, wakamfungulia na kesi ya uhujumu uchumi. Acha kabisa, keshaenda kote hadi kwa waziri mkuu, lakini wapi. Hawa watu hawana utu
 
Kun kitu inaitwa big fish,big fish wakizinguana dagaa unatakiwa kukaa pembeni,ukiona wenye ukwasi wanakwaruana ujue Kuna michongo wameshazulimiana.Ndio mana wengi wanaishia kukimbilia kwenye siasa.masuala ya madai ya Kodi hasa za kufikishana mahakamani Kwa kesi za uhujumu yako deeply rooted.Sio maswala ya kawaida,ufahamu kabisa hata kauli mbiu ya TRA ni "Voluntary tax compliance" ukiona issue imefikia forceful compliance ujue Kuna shida.

wanaenda na sera ya voluntary ili kuvutia wawekezaji na kutengengeneza mazingira rafiki ya biashara Kwa sababu mtu asipotaka lipa Kodi anaua biashara anaangalia mishe isio na Kodi umiza kichwa ni hasara Kwa serikali.

Haya mambo ya kufikishana mahakamani ni michongo tu iliobuma watu waaamua kukomoana au kufilisiana.
 
Kodi Bilioni 30 kwa kontena 10 za vitenge ni kubambikiana kodi. Na ukikataa kukaa na pembeni kujadiliana nao iki uwape rushwa utajuta, muulize mama Bonge akwambie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…