DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wengi tu wanaajiriwa. Ni jubudi zako tu. Kama ulijichanganya ukaajiriwa Kaliua DC shauri yako
IMG_20230523_092920.jpg

Kila Mtanzania atataka akafanye kazi Tra, serikali zibeni mianya ya rushwa ya hawa watumishi.deni linajifutaje?makadirio makubwa ya kodi

Pale kariakoo wafanyabiashara waliwaambia kila kitu
 
...Hela zinamuwasha ! Ziko nyingi Mpaka anaamua Kujenga Ovyo ovyo TU ili Zimuondoke ! ...
 
Kilaza utakatiza wapi kwenye medicine, labda hivyo vyuo mlivyoanzisha huko vichochoroni
Hebu tutajie hivyo Vyuo vya uchochoroni tuvijue,
Soma Medicine ukaajiriwe halmashauri ulipwe 1.5m, Wakati wenzio wanasoma B.Com+CPA unawakuta Tra wanakula 3.5m
 
Hebu tutajie hivyo Vyuo vya uchochoroni tuvijue,
Soma Medicine ukaajiriwe halmashauri ulipwe 1.5m, Wakati wenzio wanasoma B.Com+CPA unawakuta Tra wanakula 3.5m
Swala siyo kulipwa swala una akili ya kusoma medicine?kuna madaktari kibao hawategemei hata mshahara na hiyo 3.5m ni takataka kwao.
 
View attachment 2630959

UPDATE: Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule ametembelea Mtaa wa Nia Njema Mei 23, 2023, baada ya kusoma post hii ya JF

DC aliambatana na Mhandisi wa Wilaya na maafisa wengine. Baada ya kukagua ujenzi wa gorofa hilo, wamebaini kuwa linajengwa bila kibali cha manispaa na chini ya kiwango, hivyo kuhatarisha maisha ya wananchi

DC ameagiza kiongozi wa serikali ya mtaa awekwe ndani kwa kushindwa kuchukua hatua

Pia DC amempa siku 1 afisa wa TRA anayemiliki jengo hilo aripoti ofisi yake

Wakazi wa Mtaa wa Nia Njema, Mbezi Juu, wanaishukuru JF kwa kusaidia malalamiko yao yamfikie DC na hatua kuchukuliwa kusitisha ujenzi wa gorofa hilo hatarishi


Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.

Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.

Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.

Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.

Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.

Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Ndio nyumba zetu hizi Dar
 
Swala siyo kulipwa swala una akili ya kusoma medicine?kuna madaktari kibao hawategemei hata mshahara na hiyo 3.5m ni takataka kwao.
  • hao Madaktari ambao hawategemei salary ni wa kuhesabu hapa Tanzania
  • akili hizo zako za kusoma Medicine bila kuwa na hela ni upuuzi.
  • kwani mkuu kupata hiyo CPA ni kitu rahisi?
 
Umeelewa kilicholalamikiwa?
Ghorofa nne ilipaswa kuwe na bango nje la kuonyesha details za jengo. Wao wanaohoji usalama wao wapo sahihi, goba mwaka Jana limewahi kuporomoka na majirani wakafa

Nimeelewa ndiyo maana nikachangia, hiyo habari kaleta kiumbea na kiroho mbaya!
 
Dear hapanaaa, hapa nakupingaaa watu wailoko huko kwa system wanatunyonya sisi wa chinii.

Mwanzoni nilikua nna mtazamo km wako. Ila lilipokuja kunikutaaa, nilibadili akiliii.

Wanyonge tunanyonywa had jasho, afu wao wana neemeka khaaah.

Dear nipinge ni haki yako!

Wewe kakunyonya nini? naamini hata wewe ukija kukaa
sehemu yenye upenyo wa kupiga hela utapiga!!!

Wabongo wengi tuna mind set ya kuchukia / kutowapenda watu walionacho au waliopo sehemu flan!

Hujui kipato cha mtu, hujui anatafuta hela kivipi why uone unanyonywa jamani watu hawategemei mishahara tu!!
 
Punguzeni roho mbaya. Vijana wanalima majaruba ya mipunga kwao usukumani. Bado mangombe kanunua kawekeza. Ameamua ajenge pagala mnamuwaza. Watanzania wanawivu sana.
Ndo kichakaa cha kujifichia, kilimo na ufugaji, aoneshee hiyo miradi yake ya kuingiza hicho kipatooo.
 
Back
Top Bottom