roadmaster
JF-Expert Member
- Mar 21, 2023
- 1,609
- 2,751
Sio kosa lake ni sababu ya ujinga uliotukuka na lishe duniHuyo jamaa sijui anabwabwaja nini, udaktari haukimbiliwi hakuna kilaza anapeleka pua kule hata awe mtoto wa tajiri namna gani.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kosa lake ni sababu ya ujinga uliotukuka na lishe duniHuyo jamaa sijui anabwabwaja nini, udaktari haukimbiliwi hakuna kilaza anapeleka pua kule hata awe mtoto wa tajiri namna gani.
Maafisa wa tra wanalo [emoji1] maafisa wa tpa naona wao hawana shida
Hawa jamaa hawapigiwi kelele kabisaHalafu ndio wenye wana pesa kuliko hao TRA lakini wala jamii haiwahusudu wala nini.
Sijui ni kwa nini.
Malipo yote ya serikali ni kwa control numberHawa washenzi watumishi wa Tra ukiwakuta wanavojidai wana pesa,siku hizi hela wakichukua hawapeleki benki wanaweka nyumbani kwenye makabati ya nguo.
Hizo ni rushwa wanazochukua kwa wafanyabiashara kila siku
kwa hali hii watz lazima wakwepe kulipa kodi.
Kuna mmoja anadai huko nje hadi kilaza unapata udaktari, sijui ni vyuo gani huko nje vinatoa udaktari kwenye sahani.......labda vile vilivyomtunuku msukuma na babu tale PhD.Sio kosa lake ni sababu ya ujinga uliotukuka na lishe duni
Wewe ni mmojawapo upo TraMalipo yote ya serikali ni kwa control number
Uwe tajiri kwa njia za haki sio kwa janja janja.Nchi hii ni ya ajabu kweli ukiwa masikini ndio kuwa wewe ni mzalendo au ni ujinga tu! Wabongo tukiacha wivu wa maendeleo tutapiga hatua. Aliyewaloga kuwa matajiri wataishi kama mashetani ameshakufa.
Umejuaje kuwa huyo ni janja janja? Unapopata hela jaribu kula, kuweka akiba, kuwekeza kwenye biashara tofauti tofauti na kufanya maendeleo tuone kama hautoboi. Tatizo hela zenu badala ya kuziwekeza kwenye biashara tofautitofauti ili zizae zaidi nyie mnaanza na majumba makubwa mnayojenga kwa miaka 15 ambapo ungewekeza mishahara yenu hiyo kwenye biashara ungejenga jumba hilo kwa miaka 2🙉Uwe tajiri kwa njia za haki sio kwa janja janja.
Wengi tu wanaajiriwa. Ni jubudi zako tu. Kama ulijichanganya ukaajiriwa Kaliua DC shauri yako
Acha kushupaza fuvu hapa kujifanya muadilifu mno. Ukute mijitu design yako ikipata fursa mnatembea hata na sadaka za msikiti/kanisa.Kelele mnazopigaga kuhusu Ufisadi Huwa mnamaanisha nini ikiwa Mafisadi mnawaona ni wajanja na mashujaa?
Hujanijibu , kelele mnazopigaga kuhusu Ufisadi na in particular mkiwataja kina Mwigulu Huwa mnashupaza shigo Kwa Ajili ya nini? Unafiki au wivu wa kuzidiwa na wezi wenzenu?Acha kushupaza fuvu hapa kujifanya muadilifu mno. Ukute mijitu design yako ikipata fursa mnatembea hata na sadaka za msikiti/kanisa.
Ukweli usemwe tu, hapa wengi wanaojifanya kukandia ikiwemo wewe na muanzisha thread sio kwa sababu ya uzalendo bali ni sababu ya kuwa sio nyinyi mliepata nafasi ya kufanya alichofanya jamaa wa TRA.
Ingetokea nafasi zingebadilishwa na wewe ndio uwe jamaa wa TRA saa hizi ungekuwa umekaza misuli ya shingo hapa kusema unaonewa wivu.
Sema usemavyo lakini usijifanye mzalendo sana ikiwa wewe mwenyewe mganga njaa tu unaetumainia kutoka kwa fursa yeyote ile itakayojitokeza.
Ikifikia threshold litaanguka tu, sasa kama watu wanatoa tahadhari wasipuuzwe, maana ujenzi unaendeleaLabda kuhusu hizo pesa alizitolea wapi za kujengea ila sio kuhusu kibali mm nimejenga fensi sehemu yenye mchanga mwingi ikaja masika kuta limelala sijakaa vizuri likaanza kutoka ufa nikamalizia mwenyewe sembuse gorofa la floor nne lingekuwa lishashuka kitambo.
Kama ataibuka na kibali basi hakuna shida. Mimi nimeongelea endapo atakuwa amejenga jengo refu kama hilo bila kibali, huwa hakuna mazungumzo ya aina yeyote, maana wakati mnazungumza watu wanaweza kufa, kwahiyo linavunjwa lote kwanza, halafu ndio unaitwa kutoa maelezo juu ya michoro yako nk.kwa hiyo hujui kama kuna namna ya kukagua ametumia viwango gani vya ujenzi kulinganisha na michoro, iwapo ataibuka na michoro na vibali
kama hakuna jinsi ya kujua amejengaje basi majengo makubwa yanapaswa kukaguliwa hatua kwa hatua wakati wa ujenzi, mfano kukagua ususi wa vyuma kabla ya kumwaga zege
na pia bango liko wapi ? wahandisi wa manispaa nao wamezembea kutoliona jengo linajengwa mpaka ghorofa ya nne bila bango. Wajumbe na wenyeviti wa mitaa wana uwezo wa kushtukia na kuripoti Wasomali haramu kwenye maeneo yao within 3 days of arrival, lakini Mkurugenzi wa Halmashauri haoni jengo la floor nne lisilo na bango ! Vicarious negligence ya serikali inahusika.
Rushwa tuu mkuuHivi hawa jamaa wana pesa sana ee!!?
Umejuaje kuwa huyo ni janja janja? Unapopata hela jaribu kula, kuweka akiba, kuwekeza kwenye biashara tofauti tofauti na kufanya maendeleo tuone kama hautoboi. Tatizo hela zenu badala ya kuziwekeza kwenye biashara tofautitofauti ili zizae zaidi nyie mnaanza na majumba makubwa mnayojenga kwa miaka 15 ambapo ungewekeza mishahara yenu hiyo kwenye biashara ungejenga jumba hilo kwa miaka 2🙉
View attachment 2630959
Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.
Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.
Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.
Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.
Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.
Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.
Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.