DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hawa washenzi watumishi wa Tra ukiwakuta wanavojidai wana pesa,siku hizi hela wakichukua hawapeleki benki wanaweka nyumbani kwenye makabati ya nguo.

Hizo ni rushwa wanazochukua kwa wafanyabiashara kila siku

kwa hali hii watz lazima wakwepe kulipa kodi.
Malipo yote ya serikali ni kwa control number
 
Aisee huyu fala awe wa mfano hawezi kuwa mwizi kiasi hiki huyu aende jela kwanza anajenga magorofa kwa pesq gani, tuwafunue wote hao watumishi wa TRA hii jeuri ndiomana wanatufanyia ujambazi kwenye biashara zetu
 
Sio kosa lake ni sababu ya ujinga uliotukuka na lishe duni
Kuna mmoja anadai huko nje hadi kilaza unapata udaktari, sijui ni vyuo gani huko nje vinatoa udaktari kwenye sahani.......labda vile vilivyomtunuku msukuma na babu tale PhD.
 
Nchi hii ni ya ajabu kweli ukiwa masikini ndio kuwa wewe ni mzalendo au ni ujinga tu! Wabongo tukiacha wivu wa maendeleo tutapiga hatua. Aliyewaloga kuwa matajiri wataishi kama mashetani ameshakufa.
 
Nchi hii ni ya ajabu kweli ukiwa masikini ndio kuwa wewe ni mzalendo au ni ujinga tu! Wabongo tukiacha wivu wa maendeleo tutapiga hatua. Aliyewaloga kuwa matajiri wataishi kama mashetani ameshakufa.
Uwe tajiri kwa njia za haki sio kwa janja janja.
 
Uwe tajiri kwa njia za haki sio kwa janja janja.
Umejuaje kuwa huyo ni janja janja? Unapopata hela jaribu kula, kuweka akiba, kuwekeza kwenye biashara tofauti tofauti na kufanya maendeleo tuone kama hautoboi. Tatizo hela zenu badala ya kuziwekeza kwenye biashara tofautitofauti ili zizae zaidi nyie mnaanza na majumba makubwa mnayojenga kwa miaka 15 ambapo ungewekeza mishahara yenu hiyo kwenye biashara ungejenga jumba hilo kwa miaka 2🙉
 
Kelele mnazopigaga kuhusu Ufisadi Huwa mnamaanisha nini ikiwa Mafisadi mnawaona ni wajanja na mashujaa?
Acha kushupaza fuvu hapa kujifanya muadilifu mno. Ukute mijitu design yako ikipata fursa mnatembea hata na sadaka za msikiti/kanisa.

Ukweli usemwe tu, hapa wengi wanaojifanya kukandia ikiwemo wewe na muanzisha thread sio kwa sababu ya uzalendo bali ni sababu ya kuwa sio nyinyi mliepata nafasi ya kufanya alichofanya jamaa wa TRA.

Ingetokea nafasi zingebadilishwa na wewe ndio uwe jamaa wa TRA saa hizi ungekuwa umekaza misuli ya shingo hapa kusema unaonewa wivu.

Sema usemavyo lakini usijifanye mzalendo sana ikiwa wewe mwenyewe mganga njaa tu unaetumainia kutoka kwa fursa yeyote ile itakayojitokeza.
 
Hujanijibu , kelele mnazopigaga kuhusu Ufisadi na in particular mkiwataja kina Mwigulu Huwa mnashupaza shigo Kwa Ajili ya nini? Unafiki au wivu wa kuzidiwa na wezi wenzenu?

Haya ni aina ya maoni ya Watazn wengi kwamba kumbe Ufisadi ni ujanja na ushujaa si ajabu Nyerere anaonekana ni WA kudharauliwa Kwa sababu hakuamua kujimilikisha mali za Nchi.
 
Labda kuhusu hizo pesa alizitolea wapi za kujengea ila sio kuhusu kibali mm nimejenga fensi sehemu yenye mchanga mwingi ikaja masika kuta limelala sijakaa vizuri likaanza kutoka ufa nikamalizia mwenyewe sembuse gorofa la floor nne lingekuwa lishashuka kitambo.
Ikifikia threshold litaanguka tu, sasa kama watu wanatoa tahadhari wasipuuzwe, maana ujenzi unaendelea
 
kwa hiyo hujui kama kuna namna ya kukagua ametumia viwango gani vya ujenzi kulinganisha na michoro, iwapo ataibuka na michoro na vibali

kama hakuna jinsi ya kujua amejengaje basi majengo makubwa yanapaswa kukaguliwa hatua kwa hatua wakati wa ujenzi, mfano kukagua ususi wa vyuma kabla ya kumwaga zege

na pia bango liko wapi ? wahandisi wa manispaa nao wamezembea kutoliona jengo linajengwa mpaka ghorofa ya nne bila bango. Wajumbe na wenyeviti wa mitaa wana uwezo wa kushtukia na kuripoti Wasomali haramu kwenye maeneo yao within 3 days of arrival, lakini Mkurugenzi wa Halmashauri haoni jengo la floor nne lisilo na bango ! Vicarious negligence ya serikali inahusika.
Kama ataibuka na kibali basi hakuna shida. Mimi nimeongelea endapo atakuwa amejenga jengo refu kama hilo bila kibali, huwa hakuna mazungumzo ya aina yeyote, maana wakati mnazungumza watu wanaweza kufa, kwahiyo linavunjwa lote kwanza, halafu ndio unaitwa kutoa maelezo juu ya michoro yako nk.

Tambua, majengo marefu yenye vibali huwa yanakaguliwa hatua kwa hatua wakati wa ujenzi na watu toka CRB na kupewa go ahead kila baada ya hatua flani ya ujenzi, na ikigundulika kasoro unavunja kioande hicho chenye kasoro unakirudia, ndio unaendelea.
 
Umejuaje kuwa huyo ni janja janja? Unapopata hela jaribu kula, kuweka akiba, kuwekeza kwenye biashara tofauti tofauti na kufanya maendeleo tuone kama hautoboi. Tatizo hela zenu badala ya kuziwekeza kwenye biashara tofautitofauti ili zizae zaidi nyie mnaanza na majumba makubwa mnayojenga kwa miaka 15 ambapo ungewekeza mishahara yenu hiyo kwenye biashara ungejenga jumba hilo kwa miaka 2🙉
IMG_20230523_092920.jpg

Watumishi wa Tra wakiwa wanawekeza kwenye biashara 🤔
 
View attachment 2630959

Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.

Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.

Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.

Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.

Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.

Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
IMG_20230523_092920.jpg

Wanakuambia wanawekeza biashara hawa
 
Back
Top Bottom