DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Issue hapa sio gorofa kujengwa mtaani ila aliyejenga ni afisa tra alafu, ni hivi tu watu wanalalamika kuhusu rushwa iliyo kithiri kutoka kwa baadhi ya maofisa Wa tra wakitumia mwanya Wa sheria mbaya za kodi kujinemeesha Wao binafsi na kuharibu mitaji na future za watu.
 
Halafu ukute jamaa alienzisha huu uzi anakunywa na mshkaji kila weekend, akiwa na shida anaenda kwa jamaa kuomba msaada na kumsifia kila kukicha wakiwa wote. Na hata wakienda site anampamba kuwa kajenga mziga wa mjengo mtaani watamkoma. Kumbe moyoni anaungua.

Binadamu ni wanafiki sana.
 
Akija na michoro mizuri ya msingi kuna namna ya ku prove kilichomo chini ya ardhi na kilijengwa vipi ? Size ya nondo na ratio ya zege la mikanda miwili ya chini unawezaje kuithibitisha kama hukuwepo siku wanamwaga zege ? Au jiwe la jamvi, unajuaje ametandika ubuyu au jiwe kichwa wakati yote yashafukiwa chini ya jamvi?
 
View attachment 2630959View attachment 2630960


Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia (pichani), maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.

Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.

Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.

Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.

Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.

Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.

Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Huyo bwanamdogo mshahara wake ni kiasi gani, tanzie hapo.
 
Halafu ukute jamaa alienzisha huu uzi anakunywa na mshkaji kila weekend, akiwa na shida anaenda kwa jamaa kuomba msaada na kumsifia kila kukicha wakiwa wote. Na hata wakienda site anampamba kuwa kajenga mziga wa mjengo mtaani watamkoma. Kumbe moyoni anaungua.

Binadamu ni wanafiki sana.
Inawezekana pia..
 
Back
Top Bottom