myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 166,767
- 705,461
Ipo, ila nyumba ya kawaida kwa mfanyakazi..Sijui case ya huyu ila kuna mikopo ya ujenzi bank kutokana na mshahara wako.....unalipa taratibu up to 15 years....
Hapo kachomwa..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ipo, ila nyumba ya kawaida kwa mfanyakazi..Sijui case ya huyu ila kuna mikopo ya ujenzi bank kutokana na mshahara wako.....unalipa taratibu up to 15 years....
👹👹👹kwa mshahara gani wa tra hupewe hela ya kujenga ghorafa 4..Sijui case ya huyu ila kuna mikopo ya ujenzi bank kutokana na mshahara wako.....unalipa taratibu up to 15 years....
Sasa huyu ndio aje kuchukua kodi utajua hujui na anaujenzi huo..View attachment 2630959View attachment 2630960
Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia (pichani), maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.
Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.
Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.
Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.
Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.
Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.
Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Lakini kula kwa urefu wa kamba kumeruhusiwa mzee, huenda kijana kapata kamba yake mapema huwezi jua.kijana wa miaka 33 hivi anamiliki mjengo wa ghorofa 4
noma sana aisee
Na kweli ila huenda jina la kiwanja na mjengo kafanya kama Hakimi.Kaká Boni kazi anayo, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
angekuwa na utajiri wa aina hiyo ya mjengo ungekuta hakuajiriwa bali amejiajiriKwamba yeye kwao ni masikini?
Kuna watu wameajiriwa ila wana utitiri wa urithi mkubwa tuSijui case ya huyu ila kuna mikopo ya ujenzi bank kutokana na mshahara wako.....unalipa taratibu up to 15 years....
Kuna afisa mmoja wa TRA alikuwa anatudai kodi miaka kadhaa iliyopita. Baada ya majadiliano ya muda mrefu, wakaja na options zao kama kawaida. Hii ya Kaizari na hii ya kwetu. Tukalipa ya Kaizeri. Pressure ikawa juu lazima wao walipwe Chao.Wivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
huyu dogo km ni kweli ni naona hana akili. vilevile nchi hii isipotungwa sheria km za China kuwa huyu ikithibitika ni kweli adhabu yake ni kunyongwa na mali inataifishwa hakuna adhabu inayoweza kuwafaa zaidi ya hiyo. Sasa km hili dogo tu linajenga ghorofa, wakubwa zake je, na wako wangapi. Sasa mchwa km hawa watatosheka kwa uchumi upi. Na huyu mpaka kustaafu kwake atakuwa amejenga maghorofa mangapi.Wivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
kama ripoti ya CAG ilianikwa uwanjani kweupe, na wezi wakajulikana maramojaIkishindikana sheri za kunyongwa basi afilisiwe mali zake zote na afukuzwe kazi mara moja aende kutumikia kifungo cha maisha jela km tuko serious kweli. Kuwafilisi na kuwapeleka jela maisha kutawakatisha tamaa kujikusanyia mali nyingi za uwizi. Shida nani atamfunga majaji wenyewe wanakula rushwa balaa.
Uko sawa.Nchi hii Ukiwa Mtumishi wa Umma usipoiba unazomewa ukiiba unapongezwa kwasababu ni ngumu Sana kuendesha kesi dhidi ya MAFISADI na wabadhilifu wanatumia technicalities za kisheria kulinda uovu wao na kuwaambukiza WATOA MAAMUZI utajiri na kuwatoa kwenye mstari.
Ni vigumu pia katika mazingira ya Haki za Binadamu na Demokrasia kupambana na Aina ya MAFISADI WALIOPO Afrika.
Hoja ya mwandishi ni udhaifu wa kazi hajagusia kipato cha Boni ila mijadala imehama. Nafikiri hoja zake zinalenga kuepusha vifo ambavyo vinaweza kuathiri sisi wana jf au ndugu na marafiki. Kikubwa serikali ifuatilie.Issue hapa sio gorofa kujengwa mtaani ila aliyejenga ni afisa tra alafu, ni hivi tu watu wanalalamika kuhusu rushwa iliyo kithiri kutoka kwa baadhi ya maofisa Wa tra wakitumia mwanya Wa sheria mbaya za kodi kujinemeesha Wao binafsi na kuharibu mitaji na future za watu.