DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sasa huyu ndio aje kuchukua kodi utajua hujui na anaujenzi huo..
Anakufilisi kabisa huyu.
 
Nchi hii Ukiwa Mtumishi wa Umma usipoiba unazomewa ukiiba unapongezwa kwasababu ni ngumu Sana kuendesha kesi dhidi ya MAFISADI na wabadhilifu wanatumia technicalities za kisheria kulinda uovu wao na kuwaambukiza WATOA MAAMUZI utajiri na kuwatoa kwenye mstari.
Ni vigumu pia katika mazingira ya Haki za Binadamu na Demokrasia kupambana na Aina ya MAFISADI WALIOPO Afrika.
 
Wivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
Kuna afisa mmoja wa TRA alikuwa anatudai kodi miaka kadhaa iliyopita. Baada ya majadiliano ya muda mrefu, wakaja na options zao kama kawaida. Hii ya Kaizari na hii ya kwetu. Tukalipa ya Kaizeri. Pressure ikawa juu lazima wao walipwe Chao.
Bila kujua, kuna group lingine wadau wanalima pamoja. Ikaja issue ya kulipia ardhi. Jamaa anatoa ahadi zake ila bado kuna mdeni wake hajalipa.
Ni hivi sio wivu kama kila kitu ni halali. Mtu anafunga biashara ya mtu mwingine kwa dhuluma ili atusue kimaisha.
Ndio haya mambo ya kujenga vitu visivyoeleweka uchochoroni, wakidhani wamejificha
 
Wivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
huyu dogo km ni kweli ni naona hana akili. vilevile nchi hii isipotungwa sheria km za China kuwa huyu ikithibitika ni kweli adhabu yake ni kunyongwa na mali inataifishwa hakuna adhabu inayoweza kuwafaa zaidi ya hiyo. Sasa km hili dogo tu linajenga ghorofa, wakubwa zake je, na wako wangapi. Sasa mchwa km hawa watatosheka kwa uchumi upi. Na huyu mpaka kustaafu kwake atakuwa amejenga maghorofa mangapi.

Ikishindikana sheri za kunyongwa basi afilisiwe mali zake zote na afukuzwe kazi mara moja aende kutumikia kifungo cha maisha jela km tuko serious kweli. Kuwafilisi na kuwapeleka jela maisha kutawakatisha tamaa kujikusanyia mali nyingi za uwizi. Shida nani atamfunga majaji wenyewe wanakula rushwa balaa.
 
kama ripoti ya CAG ilianikwa uwanjani kweupe, na wezi wakajulikana maramoja
lakini C-in-C kahitimisha kwa kusema "hizo pesa mlizochukua hamtazikwa nazo"
wewe unategemea nini hapo ?
 
Uko sawa.
Kupambana na mafisadi wa Afrika ni ngumu..
 
Hoja ya mwandishi ni udhaifu wa kazi hajagusia kipato cha Boni ila mijadala imehama. Nafikiri hoja zake zinalenga kuepusha vifo ambavyo vinaweza kuathiri sisi wana jf au ndugu na marafiki. Kikubwa serikali ifuatilie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…