DOKEZO TAHADHARI: Afisa TRA ahatarisha maisha ya wakazi Mbezi Juu Kwa Sanya kwa kujenga ghorofa 4 bila kibali, kwenye msingi dhaifu wa nyumba ya chini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
mmemkagua mkathibitisha hana vibali au ni roho mbaya tu?
 
benki zinatoa mikopo na huenda ofisi pia inatoa mikopo ina riba nafuu, sio kila kitu ni wizi
 
benki zinatoa mikopo na huenda ofisi pia inatoa mikopo ina riba nafuu, sio kila kitu ni wizi
TRA wanatoa mkopo kwa wafanyakazi? Kuanzia lini?

Pia mkopo wa bank wa kujenga jengo kama hilo kwa mshahara wao haiwezekani. Labda tusema ana biashara kubwa inayomuingizia faida
 
Alikuwepo ila mlipiga vita tumuombe Mungu waje wengine.
 
Analipwa mshahara wa shilingi ngapi huyu kwa mwezi mpaka awe na jeuri ya kujenga jengo la ghorofa 4, kama hayuko kwenye lile kundi la wapiga dili wanaoshirikiana na wafanyabiashara wakwepa kodi!
 
Wivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
Taratibu za ujenzi wa ghorofa ni tofauti na ujenzi wa nyumba za kawaida. Kiashiria kimojawapo cha mtu anaejenga ghorofa kihalali ni uwepo wa lile bango la project. Yale mabango sijui yanaitwaje, ila pale utakuta jina na mmiliki, archtect, consultant, engineer etc... na project nzima hadi inakamilika inakuwa chini ya usimamizi wa hao watu. Ikitokea limeanguka, wataulizwa wao sio mmiliki. huwezi kuamka tuu na fundi wako unaemwamini mkaanza kujenga ghorofa. Mpaka mleta maada analeta dokezo hili inamaana kuna mapungufu kayaona.

Kuhusu alama nyekundu labda wenye mamlaka hawajaliona ama wanapozwa na afisaa wa TRA. Kwani likija kuangua wao watakuwepo? Au watu wakifa wao wanawahusu nini? Hii nchi ni zaidi ya uijuavyo🙂
 
TRA wanatoa mkopo kwa wafanyakazi? Kuanzia lini?

Pia mkopo wa bank wa kujenga jengo kama hilo kwa mshahara wao haiwezekani. Labda tusema ana biashara kubwa inayomuingizia faida
hujui kusoma au? nimeandika "huenda"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…