Mgagaa na Upwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 13,481
- 28,116
Ghorofa la pesa za wizi hizo,kimuonekano jamaa hana hata miaka 5 kazini pesa ya nyumba kama hiyo kaitoa wapi pumbavu,jamaa kaleta uzi ili tujiongeze tuWivu tu unakusumbua.
Ukiona ghorofa imesimama hadi hapo jua ana kibali tayari vinginevyo ungeshakuta Alama nyekundu.
Sasa mnadhani ndo litakuwa lenu?Ghorofa la pesa za wizi hizo,kimuonekano jamaa hana hata miaka 5 kazini pesa ya nyumba kama hiyo kaitoa wapi pumbavu,jamaa kaleta uzi ili tujiongeze tu
Kikubwa sio letu kikubwa mamlaka zianze kudili nae,hujui tu hao jamaa wa tra,latra na wale jiji wanaosimamia parking wanavyotia watu umaskini halafu ni majank tu ila si waeledi kwenye kazi zaoSasa mnadhani ndo litakuwa lenu?
Ache wakwibe tu kama wana kwibaHata huyo mama ake atafuatiliwa, unadhani hii case inahusu Gold digger?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Boni analo hili.
Huyu katoa wapi hizi pesa za kujengea gorofa? Ashughulikiwe haraka sanaView attachment 2630959View attachment 2630960
Afisa wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), Boniventure Pascal Madia (pichani), maarufu kama Boni amezua taharuki kubwa kwa wakazi wa Mbezi Juu kwa kujenga jengo la ghorofa 4 bila kibali cha Manispaa na bila kufuata viwango vya kitaalamu vya ujenzi na kutishia maisha ya wakazi hao kwa hofu ya jengo hilo kuanguka siku zijazo.
Wakazi wa Mbezi Juu/Goba bado wana kumbukumbu ya kuanguka kwa gorofa eneo la Goba kwa Awadhi mwaka 2021 na kuuwa watu wanne na sasa wanahofia maafa mengine kwenye Mtaa wa Nia Njema eneo la Mbezi Juu kwa Sanya.
Hofu ya wakazi wa eneo hilo ni kuwa afisa huyo wa TRA anajenga magorofa hayo chini ya viwango kwa kutumia nondo zenye milimita ndogo na mafundi wa mtaani bila kibali cha ujenzi cha manispaa.
Wakazi wa Mbezi Juu wanasema Boni alinunua nyumba ya chini iliyojengwa kwa msingi hafifu halafu akaigeuza kuwa jengo la gorofa 4 kwa kupandisha gorofa juu, huku akitumia mafundi wa mtaani, bila kibali cha ujenzi na bila kujenga msingi madhubuti unaoweza kujenga jengo la gorofa 4.
Hofu kubwa ya wakazi hao ni kuwa jengo hilo la gorofa linaloendelea kujengwa chini ya viwango huenda litadondoka siku zijazo na kuuwa watu kwenye eneo hilo.
Kila siku, wakazi hao wanapigwa na butwaa kuona afisa huyo wa TRA akiongeza gorofa kupanda juu kwenye jengo hilo, huku wakijua kuwa limejengwa kwenye msingi hafifu wa nyumba ya chini.
Viongozi wa serikali ya mtaa wa Mbezi Juu Kwa Sanya na Mtaa wa Nia Njema wameshindwa kuchukua hatua yoyote kuepusha maafa hayo na wanaachia gorofa hilo liendelee kujengwa bila kibali na chini ya viwango na kuhatarisha maisha ya wananchi.
Huyu ni mwizi na Hawa ndio wanawashmbua wafanyabiashara harafu nao wanalalamika badala ya kuwaeipotiAfisa wa TRA ana mshahara shingapi?
Hamna kitu ni Ufisadi na asivyo na akili anajenga hapo hapo kazini kwakeHivi hawa jamaa wana pesa sana ee!!?
Hakuna Cha unafiki,mbona mnalalamikia Ufisadi then fisadi unamtetea tena ,Huwa mnalalamikia nini Sasa?Halafu ukute jamaa alienzisha huu uzi anakunywa na mshkaji kila weekend, akiwa na shida anaenda kwa jamaa kuomba msaada na kumsifia kila kukicha wakiwa wote. Na hata wakienda site anampamba kuwa kajenga mziga wa mjengo mtaani watamkoma. Kumbe moyoni anaungua.
Binadamu ni wanafiki sana.
Kamdamganye mkeoPunguzeni roho mbaya. Vijana wanalima majaruba ya mipunga kwao usukumani. Bado mangombe kanunua kawekeza. Ameamua ajenge pagala mnamuwaza. Watanzania wanawivu sana.
Vimishahara vya mil.2 hata mil.50 hupati ndio uje kujenga gorofa?Wapo wafanyakazi wengi tu wa kukopeshwa milioni 100. Ila ni wale wenye mishahara mikubwa.
Sizani kama Afisa wa TRA ana mashahara wa kumfanya akopesheke milioni 100.
Sizani kama mshahara wa afisa wa tra unazidi milioni 3.
Labda kuhusu hizo pesa alizitolea wapi za kujengea ila sio kuhusu kibali mm nimejenga fensi sehemu yenye mchanga mwingi ikaja masika kuta limelala sijakaa vizuri likaanza kutoka ufa nikamalizia mwenyewe sembuse gorofa la floor nne lingekuwa lishashuka kitambo.Kama lina kibali, shida ipo wapi? Si itajulikana tu? Kikubwa hapo aeleze alipotoa hizo pesa, kama ni mshahara itafahamika, tunechoka kubambikiwa kidi za bikioni 30 ili tukae meza ya mazungumzo
TRA = MizaniHivi hawa jamaa wana pesa sana ee!!?
NI WIVU TU hapo ukiangalia hata lawama zilivyokaa hamna kitu ya namna hiyoSijui case ya huyu ila kuna mikopo ya ujenzi bank kutokana na mshahara wako.....unalipa taratibu up to 15 years....
Hiii inaitwa Tit for Tat [emoji23][emoji3] kaumizwa nayy kaja kuumumizia humu nashangaa huu uzi uko hai mpaka mda huu.Mtoa mada kinachokusumbua ni wivu, umaskini na njaa, hata kama umepishana kauli na mtu aina haja ya kuanika taarifa zake binafsi mitandaoni, na inaonekana you know him very well yaani ulichokifanya hapa ni whistleblowing. investigation itaanza kufanyik as soon as TAKUKURU wakipata hii taarifa
Lesson taken: Don't trust anyone
Na we ukipata upenyo pigaaaaa kwibaaaaVimishahara vya mil.2 hata mil.50 hupati ndio uje kujenga gorofa?