Taharuki: Mtanzania diaspora atekwa nyara Kilimanjaro

Kibaraka Wakili wa Polepole hajatoa taarifa kwa mamlaka husika?
Familia ya Polepole pia haijatoa taarifa?
Acha mizaha.
 
Jeshi la Polisi Tanzania limethibitisha kumkamata na kumshikilia Thadey Sabinus Kweka kwa tuhuma za makosa ya jinai ikiwemo uchochezi, likieleza kuwa hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi iliyotolewa siku ya Jumatatu Desemba 29, 2025 na Msemaji wa Jeshi hilo, Makao Makuu ya Polisi Dodoma, DCP David Misime, mtuhumiwa huyo alikamatwa usiku wa Desemba 28, 2025, mkoani Kilimanjaro, na kwa sasa anashikiliwa kwa ajili ya kuendelea na taratibu za kisheria.

Pia Soma: Taharuki: Mtanzania diaspora atekwa nyara Kilimanjaro

​

“Taratibu za kukamilisha ushahidi ikiwa ni pamoja na kupata maelezo yake juu ya tuhuma hizo unaendelea ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata”, imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa ya Polisi imekuja saa chache baada ya kusambaa kwa madai katika mitandao ya kijamii yakidai kuwa Thadey Kweka, Mtanzania anayeishi nchini Marekani na akitajwa kama mwanaharakati wa demokrasia na haki za binadamu, alikuwa ametekwa nyumbani kwake Moshi na watu waliodaiwa kuwa na silaha.

Imeelezwa kuwa Thadey Kweka aliwasili nchini Tanzania wiki iliyopita kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka, pamoja na kuhudhuria harusi ya ndugu yake mkoani Kilimanjaro.

Jeshi la Polisi halijatoa maelezo ya kina juu ya mazingira ya kukamatwa kwake zaidi ya kueleza kuwa alikamatwa kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huku likisisitiza kuwa uchunguzi unaendelea ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria.
​
 
Mpaka watu wapige kelele
 
Taarifa ya Jeshi la polisi nchini ambayo imetolewa hivi punde, imesema kuwa Thadey Sabinus Kweka amekamatwa na anashikiliwa na jeshi hilo kutokana na tuhuma za Jinai zinazomkabili mojawapo ikiwepo uchochezi.

Katika taarifa hiyo imesema kuwa mtuhumiwa huyo mwenye hati ya kusafiria namba C23858350 alikamatwa usiku wa Disemba 28, 2025 huko mkoani Kilimanjaro. .

"Taratibu za kukamilisha ushahidi ikiwa ni pamoja na kupata maelezo yake juu ya tuhuma hizo unaendelea ili hatua nyingine za kisheria ziweze kufuata" Taarifa hiyo imemalizika kwa kuandikwa kauli hiyo.
 
Hizi ndio sababu za kuingia Barabarani! ilitakiwa leoleo huko moshi watu wajaze mji kuandamana serikali kandamizi!

Bado narudia kusema SIMBACHAWENE NI KAMA KENGE TU ambalo halisikii!
unasema Rais kakutuma kuwaambia polisi wasikamate watu wanaochamba mtandaoni, ila wanakupotezea kwa kuwa ndio posho zao hizo
 
Msemaji wa jeshi la polisi anatoa taarifa ya kukamatwa kwa mtu mmoja? Kisa uchochezi
 
Mpaka watu wapige kelele

Polisi hawawezi kutoa matangaza ya kila mtu anayekanatwa. Huyu ilibidi watoe tangazo kwa sababu kuna watu wenye nia ovu walikuwa wanasambaza taarifa za kichochezi kuwa ametekwa.
 
Polisi hawawezi kutoa matangaza ya kila mtu anayekanatwa. Huyu ilibidi watoe tangazo kwa sababu kuna watu wenye nia ovu walikuwa wanasambaza taarifa za kichochezi kuwa ametekwa.
Ipo siku kibaka atakwapua simu..Police makao makuu watatoa taarifa kwa jamii.
 
Mimi nataka wamteke mpaka balozi wa Marekani nchini Tanganyika ili wakipate kile wanachokitafuta.

Sikio la kufa, hawajifunzi, mpaka jambo litokee.

Mshari na mgonvi asiye na nguvu humchokoza kila mtu. Ila akizabwa Kofi tu wa kwanza kupiga kelele.

Ngoja Kofi la Marekani lije, utaona makelele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…