Upinzani wa kweli aliousema Mwalimu kuwa ungetoka ndani ya CCM, ndiyo ule wa akina Dr. Slaa, akina Mbowe, akina Lowasa, akina Sumaye na akina Ngombare Mwiru. Lakini kwa bahati mbaya walipoenda kwa watu, jamii iliyojaa unafiki, woga na undumilakuwili, wengine walikata tamaa na kuamua kurejea CCM ili angalao wamalizie maisha yao kwa amani.
Kuwatetea Watanzania wajinga, wanafiki, waoga, ndumilakuwili wa nna kama ya huyu mleta mada, hawa ambao leo watashangilia udikteta, keshokutwa wanalaani udikteta, ni kazi ngumu sana.
Wale ambao wameendelea kuwa wap8nzani mpaka leo, kwa mazingira ya Tanzania, tena katikati ya jamii ya Watanzania, wanahitaji medali za dhahabu. Hakuna kazi ngumu kumtetea mtu mjinga na mnafiki.
Hivi unadhani kule Kenya, Raila angeitisha maandamano, halafu watu wasitokee, na kuwe na watu wanafiki wengi wa aina ya huyu mleta mada, unadhani Serikali ingeshusha bei za vyakula? Sana sana, Raila angekamatwa na kuwekwa ndani kama alivyofanywa Mbowe na kutengenezewa kesi ya ugaidi au uhaini. Halafu watu wajinga wa aina ya Idugunde kila siku wangekuwa mitandaoni wakisema Raila Gaidi.