Taifa letu ni Salama na lenye utulivu kisiasa Kwa sababu ya hawa Majenerali Pichani. Wanasiasa na viongozi Mnajifunza Nini hapa?

Taifa letu ni Salama na lenye utulivu kisiasa Kwa sababu ya hawa Majenerali Pichani. Wanasiasa na viongozi Mnajifunza Nini hapa?

Kina uchungu wa kuteka na kuuawa kwa sababu wananchi haohao ndio wanaotekwa na kuuawa na kulazimishwa kuongozwa na viongozi ambao hawakuwachagua.
Kazi ya CCM ni kuwaletea maendeleo watanzania.kazi ambayo imefanyika kwa ufanisi mkubwa sana tangia kupatikana kwa uhuru wa Taifa letu.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ukiona vyaelea ujuwe vimeundwa.tupo hapa tulipo tukiwa na utulivu wa kisiasa kwa sababu kuna watu walijitoa kwa jasho na Damu kulilinda ,kulipigania na kulitetea Taifa letu.tupo hapa tulipo kwa sababu kuna watu walitimiza vyema sana wajibu wao na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa letu badala ya matamanio yao binafsi.

Tupo hapa tulipo kwa sababu kuna watu waliamua kuilinda,kuitetea,kuihifadhi na kuilinda katiba yetu ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania dhidi ya wenye uroho na uchu wa madaraka.tupo hapa tulipo kama Taifa kwa sababu ya wazalendo ambao waliamua kwa jasho na Damu kulibeba Taifa letu katika mioyo ,vifua na Mabega yao.

Tupo hapa tulipo kama Taifa kwa sababu kuna watu waliamua kusahau na kuwa mbali na familia zao kwa ajili ya kupigania na kulinda maslahi ya Taifa letu. Ni uchapakazi wao, kujitoa na kujitolea kwao,uadilifu wao, uzalendo wao,uaminifu wao na kulinda viapo vyao kwa Taifa letu ndio kumefanya Taifa letu kuendelea kuwa lenye Amani,utulivu na usalama wa kutosha.

Watanzania tutambue ya kuwa hawa wazee wetu wameumia sana ,kuteseka sana ,kunusurika kifo na kupoteza Maisha yao kwa sababu ya kulilinda Taifa letu. Wamevuja jasho na Damu kutetea na kuilinda mipaka yetu. miili yao ilijaa na kuvuja jasho kwa ajili yetu watanzania. Hivyo hatuna budi kuwaheshimu,kuwaombea na kutambua mchango wao na uzalendo wao uliotukuka kwa Taifa letu ambao hakuna pesa ya aina yoyote ile na ya kiwango chochote kile inaweza kulingana na kujitoa kwao walikofanya kujitoa Maisha yao kwa ajili yetu.

Mungu wa Mbinguni aendelee kuwajalia Maisha marefu hawa Majenerali wetu.aendelee kuwapatia afya njema na uhai, kwa sababu ni hazina kwa Taifa letu na mawazo yao bado yanahitajika sana kwa Taifa letu.
View attachment 3143045

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Huyu mkuu Mr Lucas,mbn kama kuna genes za uchawa,anatumwa nin??? Maana hii issue ya mi5 tena imekuwa desturi yako kutuandikia,nafikiri upelekwe mirembe wakachunguze mentality fitness yako,wana jamiiforums tutagharamikia matibabu
 
Bila shaka wewe ni mhamiaji haramu hapa Nchini.Maana kila mtanzania mwenye akili Timamu na anayejitambua anafahamu wazi kuwa Taifa letu litaendelea kuwa mikononi Mwa RAIS wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan hadi 2030.
 
Ni chawa tu kama wewe ndiyo wanataka huyo kizmkazi aendelee.
 
Ni chawa tu kama wewe ndiyo wanataka huyo kizmkazi aendelee.
Na ikibidi ikifika 2030 tutabadilisha katiba yetu ili aendelee kuongoza Taifa letu mpaka Mwisho .Na huna cha kutufanya wala kufanya tukitaka kuibadilisha Katiba yetu .utapiga makelele lakini tulichoamua kitakuwa ndio hicho hicho
 
Mbadilishe na nani wewe kidampa anakujua nani. Dhalim alijaribu huo upuuzi leo yuko wapi?
 
Mbadilishe na nani wewe kidampa anakujua nani. Dhalim alijaribu huo upuuzi leo yuko wapi?
Ndo nimeshakwambia hivyo kuwa tukitaka kubadilisha tutabadilisha tu na huna cha kufanya wala kuzuia chochote kile.utapiga kelele kama debe tupu na mwishowe utanyamaza tu.
 
Umwambie nani wewe kibuyu huna ujualo zaidi ya uchawa tu. Huyo hata hiyo 2025 hagombei, biashara yake imeisha.
Mama ni hadi 2030 tunaendelea kutamba naye na baada ya hapo tunaweza kubadilisha katiba ili aendelee kuongoza Nchi yetu.
 
Back
Top Bottom