The Icebreaker
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 22,278
- 65,817
Ungekua Me ningefikiri ni ule mwiko mwingine ambao nao husonga ugali pia.Desturi ya nyumbani kwetu ukisonga ugali ukimaliza mwiko lazima uuoshe. Marufuku kuacha mwiko mchafu. Hata sijui ina maana gani ila nimekua nayo mpaka leo nikimaliza kusonga ugali lazima nioshe mwiko kabla hata chakula hakijafika mezani.
Hapana Ila uzao wa Bibi mzaa baba Wana Mila hiyo na historian yao ni umasainiBila shaka wewe ni mmasai mkuu. Kuna ukoo mmoja wa kimasai (ukoo wa MOLLEL kama sikosei) hawaui nyoka, hata akiingia ndani ya nyumba.
Kabisa au sehemu hadhara'mgahawa au ymemaliza kula wengine bado wanaendelea ww unachojonoa meno ama unasukutua maji mdomoni..nakereka sana kuna wale hawakufunzwa kutafuna chakula wakiwa wamefumba mdomo unaweza dhani anafua kumbe anakula ni chwa chwa pwa chwa khaa- kujichokonowa pua mbele za watu. Ni tabia ambayo kwetu haijwahi kukubalika kuanzia kwa watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwetu Pwani.
Imefikia mpaka mimi siikubali kabisa na nashindwa kujizuwia mtu akijichokonowa mbele yangu, nampa wazi, nendachooni jichokonowe mpaka uchoke kisha nawa mikono yako kwa sabuni, usije kuwapa watu mkonoau kutushikia vitu na mauchafu yako.
Kinyaa.
Kuna wengi sana hawana mafundisho ya maadili kutokea utotoni, nashukuru sisi wa shule za zamani na madrasa tulifunzwa mambo mengi ya kutokukahirisha watu.Kabisa au sehemu hadhara'mgahawa au ymemaliza kula wengine bado wanaendelea ww unachojonoa meno ama unasukutua maji mdomoni..nakereka sana kuna wale hawakufunzwa kutafuna chakula wakiwa wamefumba mdomo unaweza dhani anafua kumbe anakula ni chwa chwa pwa chwa khaa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Sisi wapare haturuhusiwi kufanya mapenzi kabla ya ndoa
Wapi huko?Huko nilipotokea ni marufuku mwanamke aliyeolewa kulala na chupi isipokuwa tu kipindi akiwa mwezini
Nielekeze mimi bibiKuna wengi sana hawana mafundisho ya maadili kutokea utotoni, nashukuru sisi wa shule za zamanai na madrasa tulifunzwa mambo mengi ya kutokukahirisha watu.
Nakumbuka madrasa Usraadh wetu alikuwa na somo kabisa kila siku ya Jumatano mwenyewqe akiliita "Kir'h", kwa maana "karaha".
Mengi sana madogoi madogoi ya kila siku tulifyundishwa. Kwenye maadili ya kula tulifundishwa:
1) Tusinawe mikono kabla ya watu wazima.
2) Tusikae kula na watu wazima mpaka tukaribishwe.
3) tusijipitishe watu wanapokula.
4) tukinawa, tusikumute mikono mbele za watu, ikibidi kuikung'uta uebde pembeni kabisa.
5) hakuna kujamba kwa sauti au bila sauti wakati wa kula.
6) Namna ya kukohoa ukiwashwa koo wakati wa kula.
Dah mambo ni mengi sana tulifundishwa, yanayosaidia sana kuwa na tabia "natural" ambazo hazikirihishi wengine.
Sifahamu madrasa na shule za siku hizi kama wana wakati huo.
Shule tulikuwa na somo kabisa linaitwa "domestic science" moja ya mada zake ilikuwa ni "ethics". Hili kwa tuliosoma zamani, tulifundishwa na Mwalim Muhindi, simsahau anaitwa madam Jasmin, alikuwa kijana mtanashati enzi hizo. Alitunfundisha mema mengi sana tena sana.
Nikiwaelekeza vitu wajukuu zangu sasa hivi nilivyofundishwa "primary School" enzi hizo, wananiona mtu wa ajabu.
Masalee ni kitu gani mkuu? Hebu elezea.Ni Marufuku/mwiko kukata "Masalee"(Kwa Kiswahili sijui jina lake....
Mwiko kujiangalia kwenye kioo usiku...( Ila tunajiangalia tu)
yaah , somo linaitwa cultural anthropology.Nimeipenda sana mada yako na huu uzi tukiutumia vizuri una fada kubwa sana kijamii.
Hili ni somo ambalo watu wanachukuwa mpaka PhD lipo kwenye "anthropology".

Makabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Hapa Tanzania, kwa mfano, kuna mambo fulani ambayo ni mwiko kufanyika katika jamii na ikitokea mmoja wa wanajamii akaenda kinyume na mwiko huo anaweza kupata balaa au kuwasababishia wanajamii wengine balaa.
Baadhi ya mambo/matendo hayo ni kama ifuatavyo:
1. Jogoo akiwika usiku kabla ya mapambazuko huchukuliwa kuwa ni laana ama uchuro. Adhabu yake ni kuchinjwa na kufanywa kitoweo.
2. Bundi akilia usiku karibu na maskani ni balaa. Ili kuepukana na hiyo balaa, unatakiwa kuamka ukoke moto na kuchoma punje za mtama kwenye moto huo hadi punje hizo zilipuke.
3. Kwa kabila letu, hairuhusiwi mtu kutupa tula (Sodom apple) kumvuka msichana au mvulana ambaye bado yupo jandoni. Kufanya hivyo kunaweza kusababisha kifo au kuleta balaa kwa mhusika.
4. Ukiwa unapita porini na kukuta uyoga (edible mushroom) usiuache hapo ulipo. Hata kama huutaki au hujisikii kuula, ungo’e na kuuweka sehemu iliyoinuka ili mtu mwingine anayeuhitaji akipita auchukue akale. Kuuacha bila kuung’oa inaweza kukusababishia matatizo au mikosi.
5. Maisha ya kijijini ni ya kijamaa na watu huishi kwa kusaidiana. Kuna wakati unaweza kukosa unga ukaenda kuomba kwa jirani. Hata kama huyo jirani uliyemuendea naye hana unga wa kukugawiwa, chombo ulichoenda nacho hakirudi bure. Angalau akuwekee unga kisoda kimoja kwenye chombo hicho ili kisirudi tupu. Ni mwiko chombo hicho kurudi tupu.
6. Ukitembelewa na mgeni ambaye hajakutembelea baada ya muda mrefu hata kama huna chakula mmegee ukoko kutoka kwenye sufuria atafune au hata fundo la maji anywe. Ni mwiko mgeni huyo kuondoka kwako bila kula chochote.
Hii ni baadhi ya miiko ninayoweza kukumbuka kwa haraka haraka. Nitaongezea mingine wasaa mwingine. Je, wewe kwenye kabila lako au mahali ulipokulia, ni miiko gani umewahi kuishuhudia na mpaka inaheshimiwa? Tupia mmoja hapa tujifunze kitu.
Nawasilisha.
iyo ni tabia mbaya ila sio mwiko- kujichokonowa pua mbele za watu. Ni tabia ambayo kwetu haijwahi kukubalika kuanzia kwa watoto wadogo mpaka watu wazima. Kwetu Pwani.
Imefikia mpaka mimi siikubali kabisa na nashindwa kujizuwia mtu akijichokonowa mbele yangu, nampa wazi, nendachooni jichokonowe mpaka uchoke kisha nawa mikono yako kwa sabuni, usije kuwapa watu mkonoau kutushikia vitu na mauchafu yako.
Kinyaa.
Kwetu kumuua CHATU ni bora uue mifugo yote. NI mwiko hata kumuona amekufaMakabila yote hapa Afrika au nchi nyingine za Ulaya, Asia na Marekani, wanayo miiko, mila au desturi zilizozoeleka kiasi cha kurithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.