Taja tabia yako/mazoea yako fulani hivi ambayo huyapendi na unasumbuka kuiacha/kuyaacha please don't be shy someone might give you a solution here



Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumpigia Mzee simu yakumjulia hali.ashazoea akiona wikimoja sijatimba nyumbani kwake kumuona anapiga simu mwenyewe.siwezi kumpigia kama Sina inshu yamaana kwake ninacho jitahidi nikwenda kumuona tuu angalau lisaa limoja nasepa..

ananilaumu kwanini wikinzima sipigi simu namwambia kazi MzeeπŸ˜…πŸ˜…
 
ndo vizuri huwezi kosa mchumba
 
ndo vizuri inakua rahisi kuzoeana na watu
 
Madada wa kazi aisee. Sijui ntaachaje hili suala πŸ˜‚
 
Tabia yangu kujitenga na ndugu zangu, wajomba mama wadogo na binamu na wengine,

Napenda niwe peke yangu anytime katika mambo yangu ata kama nikipata shida huwa namaliza mwenyewe bila ya kiwashilikisha.

Maana kipindi nipo mdogo niliishi nao sana na walininyanyasa sana. Mpaka nmekuwa mkubwa sipendi ndugu wala kuwa na mawasiliano nao.

Na wakinitafuta wao mara nyingi huwa sina story nyingi na wakikata simu himeisha iyo.


Hapo shida nn nini bosi hapo nafanyaje ili nikae sawa
 
Punguza kisusio na nyama mkuu🀣
 
Huyu ni mimi haswa
 
Punguza kisusio na nyama mkuu🀣
Kisusio?
Sijawahi kuonja.

Nyama nakula kuliko.

Bro, ukali ni asili ya jamii yangu.
Ni watu wapole mnoo, muonekano wa kitumishi/pastor...material🀣🀣🀣🀣

Lakini ukifanikiwa kumchokoza akachokozeka.....wewe kimbia tu
 
...kucheka cheka muda wote nikiwa naongea na mtu yeyote... Hii tabia siipendi lakini nashindwa kuiacha, msaada please... Yaan hadi hapa nilipo naandika hii komenti nacheka cheka tu na kutabasamu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…