Taja tabia yako/mazoea yako fulani hivi ambayo huyapendi na unasumbuka kuiacha/kuyaacha please don't be shy someone might give you a solution here

Taja tabia yako/mazoea yako fulani hivi ambayo huyapendi na unasumbuka kuiacha/kuyaacha please don't be shy someone might give you a solution here

Kama bandiko linavyojieleza sisi km binadamu tunatabia binafsi au mazoea fulani ambayo sisi wenyewe hatupendezewi nayo sasa huu uzi ni wa kila mtu kutaja tabia au mazoea yk ambayo unatamani uachane nayo ila imekuwa ngumu sana.

Tafadhali kuwa muwazi huwezi jua ukasaidiwa kupitia hapahapa jamii forum

Nianze na mm mimi, 'ninatabia fulani ya kukaa upweke yaani muda mwingi natamani kuwa peke yangu peke yangu mahusiano yangu mengi yanafeli sababu ya hii tabia yangu sijui itaachana nayo vipi'...?
FB_IMG_1696237722078.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumpigia Mzee simu yakumjulia hali.ashazoea akiona wikimoja sijatimba nyumbani kwake kumuona anapiga simu mwenyewe.siwezi kumpigia kama Sina inshu yamaana kwake ninacho jitahidi nikwenda kumuona tuu angalau lisaa limoja nasepa..

ananilaumu kwanini wikinzima sipigi simu namwambia kazi Mzee😅😅
 
Sipendi hii tabia ya huku duniani kuwa charming…muda mwingi nakuwa happier.. ikitokea siku nakuwa busy + kimya na mambo yangu wanaonizunguka wanaanza kuuliza ninawaza nn? Nani kanikwaza… wanajua napenda Fanta 🤣 basi wanaanza kusema waninunulie fanta.
ndo vizuri huwezi kosa mchumba
 
Utani na masihara, mtu anaweza kunitongoza asijue km nimemkubali au nimemkataa. Nishatukanwa na men wengi baada ya kugundua simaanishi kile nilichowakubalia 🤣🤣🤣🤣
Niko hivo sipendi kununa, unaweza kukasirika me nikawa nacheka SITUNZI HASIRA
ndo vizuri inakua rahisi kuzoeana na watu
 
Kama bandiko linavyojieleza sisi km binadamu tunatabia binafsi au mazoea fulani ambayo sisi wenyewe hatupendezewi nayo sasa huu uzi ni wa kila mtu kutaja tabia au mazoea yk ambayo unatamani uachane nayo ila imekuwa ngumu sana.

Tafadhali kuwa muwazi huwezi jua ukasaidiwa kupitia hapahapa jamii forum

Nianze na mm mimi, 'ninatabia fulani ya kukaa upweke yaani muda mwingi natamani kuwa peke yangu peke yangu mahusiano yangu mengi yanafeli sababu ya hii tabia yangu sijui itaachana nayo vipi'...?
Madada wa kazi aisee. Sijui ntaachaje hili suala 😂
 
Tabia yangu kujitenga na ndugu zangu, wajomba mama wadogo na binamu na wengine,

Napenda niwe peke yangu anytime katika mambo yangu ata kama nikipata shida huwa namaliza mwenyewe bila ya kiwashilikisha.

Maana kipindi nipo mdogo niliishi nao sana na walininyanyasa sana. Mpaka nmekuwa mkubwa sipendi ndugu wala kuwa na mawasiliano nao.

Na wakinitafuta wao mara nyingi huwa sina story nyingi na wakikata simu himeisha iyo.

Hapo shida nn nini bosi hapo nafanyaje ili nikae sawa
 
Ukali uliopitiliza.
To be honest mimi ni MKALI hadi najiogopa.

Ninapokasirika hakuna mtu huwa na nguvu mbele yangu.

Ni vigumu sana kunikasirisha au kuniona nimekasirika katika maisha halisi.

Lakini nikikasirika huwa hapatoshi.

Hasira zimenitia hasara kadhaa but nashindwa kuziacha.

Eee Mungu nisaidie mimi
Punguza kisusio na nyama mkuu🤣
 
Tabia yangu nikumuahidi mtu jambo nisiloweza kulitimiza,tena naweza kumuahidi kwakusisitizi hii tabia imekuwa sugu mno saana kwangu

Huwa najipanga kuiacha lakini najipata nashindwa kabisa
kitu ambacho najuwa kabisa siwezi ila naweza nikakuahidi
watu wangu wa karibu wananilakamikia saana kuhusu hii tabia ila kwangu imekuwa ngumu kuiepuka
Huyu ni mimi haswa
 
Punguza kisusio na nyama mkuu🤣
Kisusio?
Sijawahi kuonja.

Nyama nakula kuliko.

Bro, ukali ni asili ya jamii yangu.
Ni watu wapole mnoo, muonekano wa kitumishi/pastor...material🤣🤣🤣🤣

Lakini ukifanikiwa kumchokoza akachokozeka.....wewe kimbia tu
 
...kucheka cheka muda wote nikiwa naongea na mtu yeyote... Hii tabia siipendi lakini nashindwa kuiacha, msaada please... Yaan hadi hapa nilipo naandika hii komenti nacheka cheka tu na kutabasamu...
 
Back
Top Bottom