Uchaguzi 2020 Takwimu hazidanganyi: CCM wameshashinda Uchaguzi kwa Idadi ya Kura za Kanda ya Ziwa

Acheni fair play muone kama mtaambulia hata kura milioni 1
 
Kwani watoto wa shule za msingi nao wanapiga kura?
 
Siasa iko very dynamic na ukionacho kwa macho sio kinachotokea siku ya kupiga kura.kuna watu walishafanya maamuzi wanamchagua nani.na hawaji kwenye mikutano na hata umwambieje huwezi kumbadilisha mtazamo wake
Ni sawa na mimi kura yangu kwa Lissu, Jiwe akarudi chato
 
Mkuu na wewe unaonekana huifahamu vizuri Mara, ni mkoa wa kipinzani kwa miaka yote tangu chaguzi za vyama vingi zianze. Ebu niambie ni jimbo gani la mkoa wa Mara halijawahi kuwa chini ya upinzani.

Hesabu mnazopiga ndio zinakuwa ngumu kutokea kivitendo. Majimbo yote hayo JPM mwaka 2015 alikuwa anashinda kwa tofauti ndogo sana, sio kwamba majimbo wanayoshinda wabunge wa CCM basi wapiga kura wote ni CCM na yale ya CHADEMA si wapiga kura wote ni CHADEMA.

Nina uvivu wa kuandika lakini ningekupa historia ya mkoa huo tangu siasa za 1995 ambako baba wa taifa (RIP) mwenyewe alikuwa chini ya mbunge wa upinzani, huku Rorya ikienda kwa Mabere Nyaucho Marando, Mwibara ikienda kwa kijana wa upinzani na tangu hapo Musoma mjini imeshakuwa chini ya upinzani, Bunda ndio usiseme kabisa bila kusahau Serengeti na Tarime ambayo inatupa taabu sana na hata figisu za kuligawa jimbo hilo lilipelekea majimbo yote mawili kuwa upinzani. Kiufupi Mara na Kagera upinzani hupo na inabidi tuchange karata zetu vizuri sana na tuache blabla.
 
Utafiti wa hili poyoyo ni wa kijinga kabisa! Eti Lissu alipata mapokezi hafifu Mwanza hivi lilikuwa na macho hili? CCM walijaza watoto wa shule ndiyo mapokezi hayo?
 
Huoni hapo kuna takwimu za uchaguzi mkuu 2015 ambazo zlitolewa na NEC
 
Lissu ni kichaa, kila hotuba anabuni mbinu za kuuawa eti, leo kaja na habari ya sijui ndege itaanguka!! mara nini mara nchi itawaka moto, yaani analazimisha kuchaguliwa kwa kujaza hofu wananchi kwamba asipochaguliwa eti kitanuka!! Ovyo kabisa huyo Lissu, na hapati hata kura elfu hamsini walah!!
 
Kuanzia October 28, 2020 kutakua na vi🤣🤣🤣🤣 na vi😢😢😢😢😢 kwa wingi sana hapa jf
Mungu atujalie uzima tuu
 
Pamoja na hivyo pia, iukmbukwe kuwa wsehemu kubwa ya watu walioshinda katika ngazi za chinin level ya vjiji,kata,na majimbo ni wawakilishi wa CCM kitu kinachowaongezea credit katika ushawishi wa wananchi hasa katika kipindi cha kupiga kura

Kwa kuwa wao ni makada wa chama chao katika mahali walipo ni dhahiri kuwa bado wana nafasi kubwa ya kuwa na ushawishi mkubwa kwa watu wao wakati wa kura jmbo ambalo linamwongezea mgombea wa CCM nafasi ya kushinda kiti hicho cha uraisi kwa mwaka huu wa uchaguzi 2020 Oktoba
 
Magufuli wa CCM anakubalika sana kanda ya ziwa yote ndio maana hata mtoto mdogo ukimuuliza anajua John Pombe Magufuli ni nani
Hii inaonesha kabisa ni namna gani Mgombea huyu anakubalika Kwa jamii ya kanda ya ziwa
 
Kwa mwendu huu wa kufokea watu na kuwapiga mikwara pamoja na kupaniki? Labda abadilike.
 
Ila wanafunzi walipewa holiday wakaenda kuangalia fiesta, na wengi hawajafikia umri wa kupiga kura!
Demokrasia haimnyimi fursa mtu kuhudhuria na kumsikiliza mgombea lakini pia Magufuli mi kipenzi cha wananchi kujadili wahudhuriaje wawili katika moja ni hoja ya hovyo, uhalisia ni kwamba Rais anakubalika na anamvuto wakusikilizwa pindi anapoongea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…