Uchaguzi 2020 Takwimu hazidanganyi: CCM wameshashinda Uchaguzi kwa Idadi ya Kura za Kanda ya Ziwa

Uchaguzi 2020 Takwimu hazidanganyi: CCM wameshashinda Uchaguzi kwa Idadi ya Kura za Kanda ya Ziwa

Acheni fair play muone kama mtaambulia hata kura milioni 1
 
Kwani watoto wa shule za msingi nao wanapiga kura?
Screenshot_20200907-220443_Parallel Space.jpg
 
Siasa iko very dynamic na ukionacho kwa macho sio kinachotokea siku ya kupiga kura.kuna watu walishafanya maamuzi wanamchagua nani.na hawaji kwenye mikutano na hata umwambieje huwezi kumbadilisha mtazamo wake
Ni sawa na mimi kura yangu kwa Lissu, Jiwe akarudi chato
 
Pole sana Magufuri siyo msubi. Hilo eneo la chato robo tatu ya wakaazi ni wasukuma ambao walihamia miaka ya katikati ya hamsini kwa ajili ya kilimo cha pamba. Si hapo tu chato wasukuma wapo shimwanyi, kyamuyolwa ambayo yako wilaya ya Muleba eneo lote la kusini ya mji wa Biharamulo hadi Kakonko mkoani Kigoma wasukuma wamejaa na sasa wameshaingia wilaya ya karagwe na wanalima mpunga na kufuga kwa kwenda mbele. Halafu eti unasema Geita Magufuri hapendwi Geita, nani anakudanganya, mkoa wa Geita una majimbo ya Uchaguzi saba na yote CCM ilishinda mwaka 2015. Aidha, kusema eti Mara ni nusu kwa nusu ni uongo, mkoani wa Mara kwenye upinzani wa kweli ni Majimbo mawili tu ya Tarime, wakati Rorya, Musoma mjini na vijijini, Bunda vijijini Mwibara pamoja na Butiama na robo tatu ya Serengeti ni CCM tu kwa kwenda mbele, sasa hiyo nusu kwa nusu unaipata wapi ? Huko Kagera upinzani ni robo tu kote CCM tu. Wadanganye wasioifahamu kanda ya Ziwa.
Mkuu na wewe unaonekana huifahamu vizuri Mara, ni mkoa wa kipinzani kwa miaka yote tangu chaguzi za vyama vingi zianze. Ebu niambie ni jimbo gani la mkoa wa Mara halijawahi kuwa chini ya upinzani.

Hesabu mnazopiga ndio zinakuwa ngumu kutokea kivitendo. Majimbo yote hayo JPM mwaka 2015 alikuwa anashinda kwa tofauti ndogo sana, sio kwamba majimbo wanayoshinda wabunge wa CCM basi wapiga kura wote ni CCM na yale ya CHADEMA si wapiga kura wote ni CHADEMA.

Nina uvivu wa kuandika lakini ningekupa historia ya mkoa huo tangu siasa za 1995 ambako baba wa taifa (RIP) mwenyewe alikuwa chini ya mbunge wa upinzani, huku Rorya ikienda kwa Mabere Nyaucho Marando, Mwibara ikienda kwa kijana wa upinzani na tangu hapo Musoma mjini imeshakuwa chini ya upinzani, Bunda ndio usiseme kabisa bila kusahau Serengeti na Tarime ambayo inatupa taabu sana na hata figisu za kuligawa jimbo hilo lilipelekea majimbo yote mawili kuwa upinzani. Kiufupi Mara na Kagera upinzani hupo na inabidi tuchange karata zetu vizuri sana na tuache blabla.
 
Usijidanganye kuwa Magufuli anakubalika kanda ya ziwa kwa lile tamasha. Mkoa wa mara ni nusu kwa nusu, Mkoa wa Kagera hawataki kumsikia kwa matusi yake wakati wa tetemeko.

Hata kwao geita hakubaliki kivile, turufu yake iko Mwanza na anatumia mbinu ya kuongea kisukuma mikutanoni wakati ye kazaliwa Chato, wilaya Biharamulo, mkoa wa Kagera, kabila msubi. Aliileta Chato geita kimkakati baada ya kuwa apendwi kule Biharamulo
Utafiti wa hili poyoyo ni wa kijinga kabisa! Eti Lissu alipata mapokezi hafifu Mwanza hivi lilikuwa na macho hili? CCM walijaza watoto wa shule ndiyo mapokezi hayo?
 
Tanzania tuna historia gani ya takwimu hadi useme ulichoandika ni takwimu.Hii nchi bado haina watu wengi hivyo wenye misimamo thabiti itakayokufanya uje na historia ata angalau ya mwaka mmoja achilia mitano.Kuna watu hawakumbuki na wala hawajishughulishi kukumbuka 2015 wagombea waliongea kitu gani.Wengi wanaangalia ya leo na ikifika siku ya kura itategemea kaamkaje siku hiyo.Kwahiyo ulichokiandika hakina tofauti na mtu aliyebeti kamari ya mpira kwa timu fulani kwakuangalia kiwango cha mechi zake za nyuma bila kujua lolote linaweza kutokea uwanjani.
Huoni hapo kuna takwimu za uchaguzi mkuu 2015 ambazo zlitolewa na NEC
 
Lissu ni kichaa, kila hotuba anabuni mbinu za kuuawa eti, leo kaja na habari ya sijui ndege itaanguka!! mara nini mara nchi itawaka moto, yaani analazimisha kuchaguliwa kwa kujaza hofu wananchi kwamba asipochaguliwa eti kitanuka!! Ovyo kabisa huyo Lissu, na hapati hata kura elfu hamsini walah!!
 
Kuanzia October 28, 2020 kutakua na vi🤣🤣🤣🤣 na vi😢😢😢😢😢 kwa wingi sana hapa jf
Mungu atujalie uzima tuu
 
Pamoja na hivyo pia, iukmbukwe kuwa wsehemu kubwa ya watu walioshinda katika ngazi za chinin level ya vjiji,kata,na majimbo ni wawakilishi wa CCM kitu kinachowaongezea credit katika ushawishi wa wananchi hasa katika kipindi cha kupiga kura

Kwa kuwa wao ni makada wa chama chao katika mahali walipo ni dhahiri kuwa bado wana nafasi kubwa ya kuwa na ushawishi mkubwa kwa watu wao wakati wa kura jmbo ambalo linamwongezea mgombea wa CCM nafasi ya kushinda kiti hicho cha uraisi kwa mwaka huu wa uchaguzi 2020 Oktoba
 
Usijidanganye kuwa Magufuli anakubalika kanda ya ziwa kwa lile tamasha. Mkoa wa mara ni nusu kwa nusu, Mkoa wa Kagera hawataki kumsikia kwa matusi yake wakati wa tetemeko.

Hata kwao geita hakubaliki kivile, turufu yake iko Mwanza na anatumia mbinu ya kuongea kisukuma mikutanoni wakati ye kazaliwa Chato, wilaya Biharamulo, mkoa wa Kagera, kabila msubi. Aliileta Chato geita kimkakati baada ya kuwa apendwi kule Biharamulo
Magufuli wa CCM anakubalika sana kanda ya ziwa yote ndio maana hata mtoto mdogo ukimuuliza anajua John Pombe Magufuli ni nani
Hii inaonesha kabisa ni namna gani Mgombea huyu anakubalika Kwa jamii ya kanda ya ziwa
 
Kwa mwendu huu wa kufokea watu na kuwapiga mikwara pamoja na kupaniki? Labda abadilike.
 
Ila wanafunzi walipewa holiday wakaenda kuangalia fiesta, na wengi hawajafikia umri wa kupiga kura!
Demokrasia haimnyimi fursa mtu kuhudhuria na kumsikiliza mgombea lakini pia Magufuli mi kipenzi cha wananchi kujadili wahudhuriaje wawili katika moja ni hoja ya hovyo, uhalisia ni kwamba Rais anakubalika na anamvuto wakusikilizwa pindi anapoongea
 
Back
Top Bottom