Takwimu za bwawa la Nyerere zinastaajabisha sana

Hakika hii ni project kubwa kuwahi kutokea toka uhuru.

Atakaepinga aseme project kubwa anayoijua
JNHPP was wastage of money. Hilo dude litabakia white elephant. Litajengwa ila halitakuja kuzalisha hizo megawati 2,100 za umeme.

Kwa maamuzi ya Dikteta mmoja mkemia asiyeamini sayansi, tumeharibu baioanuai ya selous na kukata miti yenye saizi ya ukubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam. Hili litatugharimu milele.

Kwa sasa Kinyerezi 1 & 2 zinachangia 60% ya umeme tunaotumia Tanzania.

Miradi yote ya maji yaani Kidatu, Mtera, Kihansi, Nyumba ya Mungu, Hale, Pangani nk inachangia 40%. Numbers don't lie. Kilichofanya miradi hiyo ikwame ndiyo kitakachokwamisha na na JNHPP
 
Eneo la Selous ni km za mraba 45,000. Eneo lililofunikwa na maji ni 1,350. Kama asilimia 3 hivi. Kwa uwiano, kama miti milioni tatu iliyokatwa ndiyo asilimia 3, basi kuna miti karibu milioni mia moja bado ipo.

BTW, 25 percent ya Tz ni hifadhi. Ni nchi chache duniani zimefika hapo, hata hao viherehere wa kujidai kutufundisha mazingira na uhifadhi. Ni mpumbavu tu ndiye atatunyoshea kidole kuwa hatujali mazingira na uhifadhi.
 
Bwawa la Kariba limekata pumzi, kuna mgao wa umeme na hili liwe fundisho kwetu.
Hayo hutokea. Mwaka huu kulikuwa na ukame mkubwa dunia nzima. China walikuwa na mgao, maziwa ya kuzalisha umeme yalikauka. Ulaya ukame wa hatari ulitokea.
 
Hayo hutokea. Mwaka huu kulikuwa na ukame mkubwa dunia nzima. China walikuwa na mgao, maziwa ya kuzalisha umeme yalikauka. Ulaya ukame wa hatari ulitokea.
Ndiyo sababu Kenya wameamua kuzalisha kutokana na jotoardhi, upepo na sola, sijui kama hivi navyo vitakauka na baadhi ya nchi wameingia kwenye mawimbi ya bahari.
 
Mimi ngoja nisubiri tu umeme uwake, maana hata mkwere wakati wa gesi alisema mengi sana
 
Ndiyo sababu Kenya wameamua kuzalisha kutokana na jotoardhi, upepo na sola, sijui kama hivi navyo vitakauka na baadhi ya nchi wameingia kwenye mawimbi ya bahari.
Kenya hawana mito ya kutosha. Nusu ya nchi yao ni jangwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…