Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Ujenzi wa mabwawa kwa miaka ile ulikuwa rahisi ila baada ya tekinolojia mpya kuja umekuwa ni aghali na unatumia muda mrefu kuanza matumizi kuliko jotoardhi, upepo, sola na mawimbi ya bahari ambavyo gharama zake ni ndogo na hutumia muda mfupi kukamilika.Mbona umeme wa maji ni mpango wa muda mrefu na cheap kabisa. Ndiyo maana unaona China kila siku anaijenga.
Ulaya ndiko walikoanza kutumia vyanzo nilivyovitaja, hebu fikiria nchi hizo zilivyo ndogo kisha wamege kilomita elfu kujenga bwawa wakati wanaweza kutumia viwanja vitatu vya mpira na wakapata kiwango cha umeme sawa na wa bwawa! Tena kwa muda mfupi na bila kuhofia upungufu wa maji. Kenya ni moja ya mifano tu zipo nchi nyingine kadhaa za Afrika na ulaya.Kwahiyo unataka kusema Kenya inazidi china na nchi za ulaya au?
Ukiwa unaendelea kustaajabu nikuulize: Je, Mabwawa madogo yaliyopo ufanisi wake ukoje?Nafikiri toka uhuru hatujawahi kufanya mradi mkubwa namna hii. Kukamilika kwake kutatujengea roho ya uthubutu kwenye miradi mikubwa.
Eneo la ziwa litakuwa na ukubwa wa karibu km za eneo 1,350. Hii ni kama mara mbili ya ukubwa wa Mtera. Na kwa eneo litakuwa la tano nyuma ya ziwa Rukwa.
Japo ziwa Rukwa ni kubwa kwa eneo, likiwa na km za mraba 5700+. Ziwa la Nyerere litakuwa na maji mengi zaidi. Km za ujazo bilioni 33 dhidi ya 20 za ziwa Rukwa.
Litakuwa ni moja ya maziwa makubwa ya kutengenezwa na binadamu kwa ujazo. Ziwa kubwa kuliko yote la kutengenezwa duniani ni ziwa Kariba, likiwa na ujazo wa km za ujazo 180.
Umeme MW 2100 utatufaa sana. Hope tutaanza kupikia na umeme. Aliyethubutu kuanza mradi huu aliona mbali sana.
Mkianza kupikia Umeme mniite MBWA, Niko paleeee nimekaaUmeme MW 2100 utatufaa sana. Hope tutaanza kupikia na umeme
Lakini hao hao China hawategemei umeme wa maji peke yake.Mbona umeme wa maji ni mpango wa muda mrefu na cheap kabisa. Ndiyo maana unaona China kila siku anaijenga.
Una kadi ya CCM?Tutaruhusiwa kwenda kuogelea hapo ziwani?
Eneo la Selous ni km za mraba 45,000. Eneo lililofunikwa na maji ni 1,350. Kama asilimia 3 hivi. Kwa uwiano, kama miti milioni tatu iliyokatwa ndiyo asilimia 3, basi kuna miti karibu milioni mia moja bado ipo.
BTW, 25 percent ya Tz ni hifadhi. Ni nchi chache duniani zimefika hapo, hata hao viherehere wa kujidai kutufundisha mazingira na uhifadhi. Ni mpumbavu tu ndiye atatunyoshea kidole kuwa hatujali mazingira na uhifadhi.
Yaani zamani ilikuwa rahisi kujenga mabwawa kuliko siku hizi? Sema labda siku hizi yanayojengwa ni makubwa sana ndiyo maana yanachukua muda mrefu na ghali. Umeme wa maji bado ni relevant sana. Bado haujapatikana umeme cheap kama wa maji. Kwa nchi zenye potential ya umeme wa maji ni ujinga kukimbilia options za gharama. Hivyo vyanzo unavyotaja, ukitaka vizalishe kiasi kama umeme wa maji gharama yake ni kubwa mno, tafuta gharama zake kwa MW.Ujenzi wa mabwawa kwa miaka ile ulikuwa rahisi ila baada ya tekinolojia mpya kuja umekuwa ni aghali na unatumia muda mrefu kuanza matumizi kuliko jotoardhi, upepo, sola na mawimbi ya bahari ambavyo gharama zake ni ndogo na hutumia muda mfupi kukamilika.
Ulaya sehemu kubwa ni tambarare ndiyo maana haifai kwa Hydropower. Lakini nchi zenye maporomoko kama Norway, Iceland na Russia wanatumia sana umeme wa maji. Lazima uangalie jambo litakalo faa mazingira yako.Ulaya ndiko walikoanza kutumia vyanzo nilivyovitaja, hebu fikiria nchi hizo zilivyo ndogo kisha wamege kilomita elfu kujenga bwawa wakati wanaweza kutumia viwanja vitatu vya mpira na wakapata kiwango cha umeme sawa na wa bwawa! Tena kwa muda mfupi na bila kuhofia upungufu wa maji. Kenya ni moja ya mifano tu zipo nchi nyingine kadhaa za Afrika na ulaya.
Hayo mabwawa ndiyo yanatupa umeme. Bila hayo, huu mgao wa juzi ungekuwa mwaka mzima. Na ni kwaida kwa mabwawa ya umeme, linaweza kuwa na uwezo wa MW2115, lakini wakainstall turbines za 1500MW tu.Ukiwa unaendelea kustaajabu nikuulize: Je, Mabwawa madogo yaliyopo ufanisi wake ukoje?
Je, ni mradi upi mkubwa ulishasimamiwa kikamilifu na hawa watu na ukawa na tija?
Je, tusubirie hadi lini kabla ya kuja kutangaziwa kuwa upo chini ya kiwango? Au uzalishaji umedorora au Kuna ufisadi mkubwa sana umebainika??
Sehemu kubwa ni makaa ya mawe na maji. China wanazalisha MW zaidi ya milioni 2. Tunatakiwa kutumia vyanzo vyote tulivyo navyo, maana kazi ya kuzalisha umeme bado ni safari ndefu kwetu.Lakini hao hao China hawategemei umeme wa maji peke yake.
Hiyo ni hoja ya msingi, labda kama huitaki. Kuchukuliwa kwa 3% ya eneo la Selous si kitu ukilinganisha na faida ya mradi. Wangekuwa wanazamisha mbuga nzima wengi tungepinga...hoja yako ni sawa na kusema moyo hauna faida kwa binadamu kwasababu ni 0.6% ya mwili mzima.
..Nashauri tutumie hoja sahihi kutetea mradi wa umeme wa Stieglers.
Huu mradi ulikuwepo toka kitambo, Awamu ya Kwanza, ulikosa tu utekelezaji kutokana na mambo mengi muhimu na yenye kipaumbele zaidi, kama elimu, afya,. n.k.Nafikiri toka uhuru hatujawahi kufanya mradi mkubwa namna hii. Kukamilika kwake kutatujengea roho ya uthubutu kwenye miradi mikubwa.
Eneo la ziwa litakuwa na ukubwa wa karibu km za eneo 1,350. Hii ni kama mara mbili ya ukubwa wa Mtera. Na kwa eneo litakuwa la tano nyuma ya ziwa Rukwa.
Japo ziwa Rukwa ni kubwa kwa eneo, likiwa na km za mraba 5700+. Ziwa la Nyerere litakuwa na maji mengi zaidi. Km za ujazo bilioni 33 dhidi ya 20 za ziwa Rukwa.
Litakuwa ni moja ya maziwa makubwa ya kutengenezwa na binadamu kwa ujazo. Ziwa kubwa kuliko yote la kutengenezwa duniani ni ziwa Kariba, likiwa na ujazo wa km za ujazo 180.
Umeme MW 2100 utatufaa sana. Hope tutaanza kupikia na umeme. Aliyethubutu kuanza mradi huu aliona mbali sana.
Napinga.Hakika hii ni project kubwa kuwahi kutokea toka uhuru.
Atakaepinga aseme project kubwa anayoijua
Kweli, JPM pamoja na makandokando yake anatakiwa kuheshimika kwa uthubutu wake. heshima kubwa sana. Hakuwa kiongozi wa kuongoza tu ilimradi kukuche, akisubiri muda wake uishe kama hawa wengine. Hapo nimezungumzia kilomita za ujazo, ndiyo kilometers cubic kwa kiswahili.Huu mradi ulikuwepo toka kitambo, Awamu ya Kwanza, ulikosa tu utekelezaji kutokana na mambo mengi muhimu na yenye kipaumbele zaidi, kama elimu, afya,. n.k.
Hata hivyo, haiwezekani kutotambua uthubutu wa huyo aliyeufufua tena na kuuweka mbele zaidi, kama alivyofanya na Makao Makuu ya nchi. Huo ni uongozi wa uthubutu unaostahili heshima (ukiondoa mauchafu mengine).
Katika uwasilishaji wako umetumia "kipimo cha ujazo kuwa Km"? Bila shaka ukiwa na maana ya kilomita za mraba?
Kipimo sahihi kitakuwa "Cubic Meters" au hata "Cubic Kilometers"
Wanasema ndiyo uhamishaji mkubwa kabisa wa watu kuwahi kutokea Africa!!Napinga.
Projekti kubwa zaidi kuliko zote iliyowahi kufanyika Tanzania ni kujenga vijiji vya ujamaa. Hadi leo hii vipo, hata kama havijulikani kwa jina hilo.
Hata ujenzi wa viwanda vingi Tanzania ambavyo vyote vilitelekezwa, ni mpango mkubwa zaidi kuliko huu mradi mmoja.
Na hata sijui kama kuna nchi Afrika iliwahi kujenga viwanda vingi kiasi kile kwa wakati ule.Wanasema ndiyo uhamishaji mkubwa kabisa wa watu kuwahi kutokea Africa!!
Hiyo ni hoja ya msingi, labda kama huitaki. Kuchukuliwa kwa 3% ya eneo la Selous si kitu ukilinganisha na faida ya mradi. Wangekuwa wanazamisha mbuga nzima wengi tungepinga
Kufananisha viungo vya mwili vyenye kazi tofauti tofauti na mbuga ambayo ipo sawa karibu yote ni utoto. Kusema nimekariri sehemu nao ni utoto pia. Tujitahidi kujenga hoja kama watu wazima...hiyo hoja umeikariri toka kwa mtu fulani.
..swali langu ni dogo sana na liko hivi.
..moyo ni 0.6% ya mwili wa binadamu.
..mguu ni 17% ya mwili wa binadamu.
..ukiambiwa uchomolewe moyo au mguu utachagua kipi?
..kinachotakiwa kuangalia sio ukubwa wa eneo, bali umuhimu wa eneo husika kwa ekolojia nzima na mazingira ya mbuga ya Selous, bonde la mto Rufiji, na delta ya mto Rufiji.
..mjadala kuhusu mradi wa Selous uliburuzwa buruzwa tu. Hatukufanya majadiliano ya uwazi na ukweli. Tulitumbukiza propaganda na mihemuko.
Kufananisha viungo vya mwili vyenye kazi tofauti tofauti na mbuga ambayo ipo sawa karibu yote ni utoto. Kusema nimekariri sehemu nao ni utoto pia. Tujitahidi kujenga hoja kama watu wazima.