Saido alistahili kwanza kafunga magoli kwenye Club mbili tofauti.
Hiyo inaonesha uwezo binafsi aa mchezaji katika kufunga bila kutegemea Quality ya wachezaji wengine ambao watamsaidia kufanikisha lengo.
Mayele angecheza kwenye Club kama Geita asingeweza kutoka na magoli yale ambayo Saido alifunga.
Pili, Saido ni Attacking Midfielder. Hakai eneo la mwisho, huyu role yake ya kwanza ni ku supply mipira kwa Strikers hivyo kuona anakupa double profit hicho sio kitu kidogo.
Tatu ameonesha ni mchezaji ambaye anaweza kufunga katika mazingira yeyote, Mayele sijui kama alishawahi kupiga freekick.
Mayele penati tu ilimshinda.
Lakini Saido kaonesha makali kwenye kila department na tena kaimaliza eneo lake kaanza kutifua na kwenye maeneo ya Strikers ambapo huko sio kwake.