Frank Hood
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 597
- 1,374
kingine cha kuongezea,ss hv ukiacha uwezo binafs timu inacheza kitimu zaidi na sio kutegemea uwezo binafs wa mchezaji zaid.Ndio maana zinapigwa pasi milio 10,809,023/-. Sio km msimu uliopita unakuta bila mbio za kisinda timu inafel au km Mukoko au Fei toto akikosekana mnaumiza kichwa.Tofauti ipo kubwa sana, msimu uliopita. tukianza na wachezaji ni kwamba kulikuwa na wachezaji walio na kiwango bora lakini pia kulikuwa na rundo la wachezaji wasiokuwa na ubora.
Kaseke
Adeyuni
Mukoko
Nchimbi
Farid musa
Mauya
Hawa ndio walikuwa miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa kwenye kikosi cha Yanga kupata matokeo au kubadilisha mchezo, lakini hao wote wamekuwa wasuguaji wa benchi kwa sasa hadi Mukoko ambaye aliimbwa sana msimu uliopita hivyo unaona ni quality ya wachezaji waliosajiliwa na Yanga.
La pili ni performance ya timu. Kwa misimu kadhaa iliyopita performance inaoneshwa na Yanga kwenye mchezo wa wiki ya wananchi haitotokea tena kuonekana kiwango kama kile katika mechi yoyote ile ya Yanga lakini saivi unaona utofauti. Yanga wanaonesha kuimarika mechi hadi mechi hivyo kadri siku inavyoenda timu inakuwa imara angalia aina ya mpira unaochezwa na Yanga siku hadi siku wanazidi kubadilika, anzia kwa soka waliochezewa Simba mpaka kufikia jana kwa Azam.
Tatu ni kwamba Yanga walikuwa wanafeli kwa kutokuwa na wachezaji mbada (ufinyu wa wachezaji) na ndio maana Yanga walikata moto kwenye mzunguko wa pili kwavile wachezaji walitumia nguvu nyingi sana mzunguko wa kwanza hivyo wakachoka. Ila kikosi kingekuwa kipana wangefanya rotation ya wachezaji. Saivi unaona ni tofauti Bangala kiungo anacheza beki anacheza. Mukoko hana nafasi kikosi cha kwanza lakini atatumika kwenye rotation ya timu kama ilivyo kwa wachezaji wengineo