Pre GE2025 Tamaa ya Tundu Antipas Lissu, Kuutaka uwenyekiti wa CHADEMA taifa ni utashi wake binafsi au shinikizo kutoka nje ya nchi kwa wanao mbackup!

Pre GE2025 Tamaa ya Tundu Antipas Lissu, Kuutaka uwenyekiti wa CHADEMA taifa ni utashi wake binafsi au shinikizo kutoka nje ya nchi kwa wanao mbackup!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama uliwahi kusikia kuna uwendawazimu, basi ni kama huu uliouandika.

Isije siku nyingine ukasema kuwa na Rais Samia anagombea Urais kutokana na shinikizo kutoka mataifa mbalimbali anayoyatembelea, chawa wake watakuteka na hatutakuona tena.

Hata kama una akili kidogo, jitahidi utumie vizuri akili ndogo uliyopewa kuliko kila wakati kuandika vitu vya kijinga kama unavyofanya.

Mwenzio Mwashambwa siku hizi kajirudi kidogo, haandiki upuuzi wa kufikia kiwango chako.
Tlaatlaah amekuwa mwendawazimu!
 
Kama uliwahi kusikia kuna uwendawazimu, basi ni kama huu uliouandika.

Isije siku nyingine ukasema kuwa na Rais Samia anagombea Urais kutokana na shinikizo kutoka mataifa mbalimbali anayoyatembelea, chawa wake watakuteka na hatutakuona tena.

Hata kama una akili kidogo, jitahidi utumie vizuri akili ndogo uliyopewa kuliko kila wakati kuandika vitu vya kijinga kama unavyofanya.

Mwenzio Mwashambwa siku hizi kajirudi kidogo, haandiki upuuzi wa kufikia kiwango chako.
Gentleman,
inashangaza sana kwakweli,
Asubuh mtu anatangaza nia ya kugombea umakamu mwenyekiti wa Chadema taifa, halafu ghafla tena jioni anatangaza kugombea uenyekiti kamili wa Chadema Taifa.

Hakuna shinikizo la kimataifa kutoka kwa mabwenyenye ya magharibi yanayombackup kweli?

au ni tamaa na uchu wa madaraka na vyeo?🐒
 
Mbowe awajibike tu.

Kama Mwenyekiti ameshindwa kukipeleka chama to the promised land(Magogoni)

Wameshindwa Uchaguzi huu mdogo uliopita.

...na mengine mengi tu.

Awajibike. Ajing'oe kwenye kinyang'anyiro cha Uenyekiti wa CHADEMA na abakie kuwa Mshauri/Caretaker tu

Hatahivyo,

Tundu Lissu nae awaachie wengine-Atakilipua chama.
Gentleman,
naona unang'ata na kupulizi kisayansi zaidi mambo haya.

uko fair kitaalamu sana aise
well done 💪👊
 
Mbowe hajali hayo mambo ya credibility, ingekuwa hivyo kina Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe, Dr Slaa, etc wote bado wangekuwa CHADEMA.

Kwa Mbowe CDM ni mfereji (sio mrija) wa kipato cha uhakika, kumbuka kuna kipindi wabunge wa CDM walikuwa wanachangia ela kila mwezi kwenye moshahara yao, ila mwisho wa siku ela zinarudi kwa Mbowe na team yake.

Wengi humo ndani washamchoka, angalia matendo ya John Mnyika, Godbless Lema, John Mrema, Mwita, etc wote ni kama wamejitenga na chama ila bado wapo chamami.

Zitto alijaribu fanya mabadiriko CHADEMA ila akaangukia pua, hawa wa sasa wakiangukia pua jua CHADEMA ipo vipande viwili.
Aise,
kumbe mambo ni mengi namna hiyo aise 🐒
 
uko ndani ya mada gentleman na umepiga utosini kabisa tena bila kuegemea upande wowote baina ya mafahali hawa wawili ndani ya chadema.

Ni muhimu ubabe wao ukaamuliwa kwenye sanduku la kura bila masharti yoyote 🐒
Inatakiwa watafsiri kwa vitendo maana ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
 
Lissu ni mtu wa vurugu tu, hana jipya, siasa za vurugu hazina nafasi Tanzania, Chiba anatafuta public sympathy.
 
Lissu ni mtu wa vurugu tu, hana jipya, siasa za vurugu hazina nafasi Tanzania, Chiba anatafuta public sympathy.
For sure na atawavuruga hadi wavurugike vizuri sana 🐒
 
sasa kama ni hivyo kulikua na haja gani kutangaza kutaka kugombea umakamu mwenyekiti, tena kwa mbwembwe na majigambo, huku akiapa kutopambana na Mbowe kwenye nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Chadema?

Nini kimebadilika ghafla,
tena kwa dhihaka na kejeli nyingi sana kutamani kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa?

ni uchu wa madaraka, tamaa ya vyeo au shinikizo za wanaomfadhili kutoka ng'ambo?

Kama unadai kapata shinikizo la wajumbe wa chama, ni wangapi hao wajumbe na shinikizo lilianza lini?🐒
Lissu na Mbowe ndiyo wenye majibu ya Uhakika Mkuu.. Mimi na wewe tunabuni tu na kuhisi huenda ni hivi, huenda ni vile..
 
Chairman wa sasa wa Chadema Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe, akizungumzia kusudio la Tundu Antipas Mughwai Lisu kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa, kwa namna yoyote ile atakua ameingia kwenye trap au mtego wa kisayansi alotegwa na kukoleza au kuzidisha joto, uhasama na vita ya madaraka ndani ya chadema hususani dhidi ya nafasi ya uenyekiti wa Chadema Taifa.

Tundu Lisu akijibiwa azma yake hiyo na chairman Freeman Mbowe, atakua amefanikiwa kumuingiza mbowe mtegoni, na ndipo sasa mambo na madudu mengine mazito zaidi na muhimu sana dhidi ya chairman Mbowe yataibuliwa na kuwekwa hadharini.

Na hilo ndilo lengo hasa la Tundu Lisu. Na huo ndio utakua mwanzo wa safari ya kujiengua chadema na kuelekea kwingineko kula maisha au kupata nafasi na fursa ya kugombea urasi uchaguzi mkuu ujao Oct 2025, endapo hoja na tuhuma zake dhidi ya chairman Mbowe zitapanguliwa kwa ufasaha.

Nadhani Tundu Lisu ana mambo mengi mno moyoni dhidi ya uongozi wa chadema Taifa, hata hivyo, mpaka kufikia uamuzi wa kutaka awe mwenyekiti wa Chadema Taifa. Tundu Antipas Mughwai Lisu, anahitaji mambo mawili tu kwenye vita hii. Ni awe mwenyekiti wa Chadema Taifa, au kujiengua chadema na kutafuta fursa za kisiasa kwenye vyama vingine vya siasa nchini.

Na hili linaweza kua ni shinikizo kutoka nje ya nchi, hasa kutoka kwa wale wanao wanaombackup yeye na familia yake huko ughaibuni. Ni dhahiri awali alionekana hayupo serious.

Kukaa kimya kwa Freeman Aikaeli Mbowe, kutampasua kichwa na kutamdhoofisha sana Tundu Lisu anaetamani majibizano, na hapo mbowe atakua ameupiga mwingi zaidi, akiendelea na harakati zake za kutetea kiti chake cha uenyekiti wa Chadema Taifa, kadiri ya mipango mikakati yake na ratiba zake, bila kumzungumzia Lisu hata kidogo.

Kwa kufanya hivi, Freeman Mbowe atakua amemkwaza Lisu, na kumlazimisha amchokonoe zaidi zaidi au kujaribu kupaint uongozi wa Mbowe kama kitu ambacho kiliidumaza chadema na kwamba uongozi wake uligubikwa na sintofahamu nyingi sana.

Na Mbowe akiendelea kukaa kimya zaidi bila kujibu chochote, atakua amemchanganya zaidi Lisu na kumjaza hofu ambayo itamfanya atathmini upya mpango na mtego wake huu wa kumchefua chairman Mbowe ili eti yeye aonekane bora zaidi.

Kiufupi,
katika mpambano na mgawanyiko huu ndani ya chadema, kama wadau wa bobevu, tunajifunza na tutabaini wazi nani miongoni mwa mafahali hawa wawili ndani ya chadema, anatumia sayansi ya siasa kufanya siasa na nani anatumia mihemko, chuki na kukurupuka katika kutafuta uongozi wa kisiasa ndani ya chadema.

Unadhani ni nani aliemshinikiza Lisu kuachana na kugombea umakamu mwenyekiti wa Chadema Taifa, na kuamua kumendea uenyekiti wa Chadema Taifa?

Je, ni shinikizo kutoka ndani ya nchi au nje ya nchi?🐒

Mungu Ibariki Tanzania.
Kwa wenye Akili zinazofanana na watu waliosomea Cuba jibu kwa swali lako ni kwamba hakuna shinikizo kutoka popote pale bali hii ni michezo ya kisiasa tu !

Gentlemen msianze kuwa na wasiwasi 😀 !
Japo Waswahili husemaga wasiwasi ndio Akili 😳🙏!
 
Gentleman,
Yapo mambo muhimu sana kujifunza

kwanza,
ni muhimu kujifunza kwenye hili, Je, ni tamaa au shinikizo la nje, Lisu kuacha kugombea umakamu mwenyekiti na kuutaka uenyekiti Taifa?

Jambo la pili,
Ni muhimu sana kujifunza, kati ya mafahali hawa wawili nani anatumia sayansi ya siasa na nani mkurupukaji katika kufikia azma zao za kisiasa?

Jambo la meisho,
makasiriko si muhimu sana kwenye hoja hii ya maana mno asubuhi hii, kua muungwana 🐒
Kila mtu Ana haki ya kugombea nafas yoyote ile, kwa muktadha wa demokrasia mbowe anatakiwa kuachia kiti kwa namna atakayoiona ni bora na isiyo na wasiwasi. Lakin ukisema mtu fulani anakurupuka utakuwa mshadadiaji wa vitu badala ya uhalisia
 
Kila mtu Ana haki ya kugombea nafas yoyote ile, kwa muktadha wa demokrasia mbowe anatakiwa kuachia kiti kwa namna atakayoiona ni bora na isiyo na wasiwasi. Lakin ukisema mtu fulani anakurupuka utakuwa mshadadiaji wa vitu badala ya uhalisia
kila mtu anahaki ya kugombea, halafu mbowe anatakiwa kuachia kiti, right? :pedroP:
haki ni ya nani sasa hapo?

siasa ni sayansi, siasa ni mahesabu.


unadhani nani kati ya mafahali hawa wawili anakurupuka na makelele mengi na mdomo, na nani anatumia mahesabu na sayansi kufikia azma yake ya kupata nafasi ya uongozi chadema?:BASED:
 
Hao matapeli wote wanatengenez tukio wapige ruzuku wagawane wajaze matumbo yao.
Hakuna, nasema hakuna upinzani hapo ni wasanii tu wote.
 
Back
Top Bottom