Uchaguzi 2020 Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole

Uchaguzi 2020 Tamaa za Wateule wa Rais kutia nia Ubunge zitawaponza wengi. Ushahidi huu hapa wa Rais Magufuli na Humphrey Polepole

SN.BARRY

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2012
Posts
4,038
Reaction score
8,929
KUNA FUNZO LOLOTE KWA SASA?

Aprili 2019 Rais Magufuli ktk moja ya vikao vya ndani ya chama cha CCM, amemlaumu Naibu Waziri wa zamani wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na aliyewahi kuwa pia RC Tabora ndugu Ludovick Mwananzila kwa kumwita mwenye tamaa nyingi sana.

Mwananzila alishika nafasi ya unaibu waziri ktk awamu ya kwanza ya Kikwete na Mkuu wa Mkoa katika awamu ya pili baada ya kukosa ubunge mwaka 2010.

Rais Magufuli anamlaumu Mwananzila kwa kuwa baada ya kukosa ubunge 2010 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa lakini 2015 kwa tamaa zake alirudi tena jimboni kwake kuomba ubunge ilihali ana cheo kikubwa serikalini. Alifika mbali kwa kusema Mwananzila hafai hata kuwa Katibu Tarafa na ndiyo maana kampoteza kabisa.

Je, kuna funzo kwa wateule wa Rais Magufuli?


 
Kabisa ni amri kutoka mamlaka za juu.

Hapo siro atakua anapanga vikosi kwa ajili ya kesho, si ajabu hadi mazoezi wanafanya usiku huu kwa ajili ya membe kesho
 
Unapompa Mwanao Uji Anywe Halafu Anaringa Unamzaba Kibao Ili Abugie Uji Vizuri!!😀😁😂😅😏😏😐😃😃🤣


Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Ngojeni Kuzabwa Kibao!!!🤨😶😋😐
 
Back
Top Bottom