Hizi hazimo kwenye Biblia.
1: Sikukuu za Krismass na Easter.
2: Kunena kwa Lugha ambazo mnenaji na wasikilizaji wote hawaelewani.
3: Maombezi kwa maiti ili isamehewe dhambi alizofanya akiwa hai.
4: Sabato ya Jumapili.
5: Mchungaji au askofu wa kike. Katika biblia mchungaji ni Mume wa mke mmoja sio mke wa Mume mmoja.
HAYAMO KWENYE QURAN
1: Ishmail kuwa Bora kuliko Isaka.
2: Waislam Kufanya miujiza wakati mtume hakuwahi kufanya muujiza wowote ndani ya quran.
3:Kuvaa suruali ambazo hazifiki chini.
Zile Suruali fupifupi.
4: Wanawake na wanaume kuchangamana wakati wa ibada ya hijja kwenye kaaba (ibada ya heshima kabisa) wakati huku misikitini hawachangamani.
5: Wanawake kuwa maimam na kuongoza ibada zanye mchanganyiko wa jinsia zote.
Nini maoni yako.
Ufafanuzi Kwenye Qur'an
1."Ishmail kuwa Bora kuliko Isaka"
Kama Kichwa Cha Habari Kinavosema "Tamaduni Ambazo hazimo Kwenye Bibilia au Qur'an" Naomba Kuuliza Je Quran imesema Kuwa Isaka Ni Bora Kuzid Ismail mpka Sisi Tukabadili Kinyume.Kila Mtume Ana Nafasi Yake Mwenyezimungu Anajua Nani Ni Mbora Kati Yao.
2."Waislam Kufanya miujiza wakati mtume hakuwahi kufanya muujiza wowote ndani ya quran"
Je, Safari Ya Israa na Miraji Aloifanya mtume Muhammad(S.A.W) Haikuwa Miujiza?Fatilia Jambo Kwanza Kabla Ya Kuja na Hoja.
Waislamu Tunaishi Kwa Kufuata Qur'an
Na Hadithi Sahihi.
Hivyo kuna hadithi nyngi zinazoonyesha Miujiza aloitenda Mtume Muhammad (S.A.W) Mbali Na Muujiza Wa Safari ya Israa Na Miraj Kama
*Muujiza wa Kupasua Mwezi
(Chanzo:Quran 54:1-2, Al-Mīzān, 1391 AH, vol. 19, p. 65.)
*Muujiza wa kutoka Maji katika Vidole vya mtume Muhammad(S.A.W) watu wakanywa Na kutia Udhuu (Chanzo Sahih al-Bukhari 5639)
Miujiza ya mtume Muhammad (S.A.W) Iko Mingi.Pia Muhammad (S.A.W) Mwenyewe Ni Muujiza,Uliza Kwa Nini Aliwekwa Namba Moja Kwenye jarida La Most Influential People In The World
3:"Kuvaa suruali ambazo hazifiki chini.
Zile Suruali fupifupi"
Hakuna Ubaya katika kufanya Hvo kwani Ubaya Ni Kuvaa Nguo Ambavyo Haivuki Magoti
Pia ni Vizuri kwa Muislamu wa kiume kuvaa Nguo fupi isiyovuka Vifundo Vya miguu Kwani Nguo Zinazovuka Vifundo kwa Miguu Zinaweza Beba uchafu Hivo Kuitolea udhu Nguo yako.
Hapo Hakuna Ubaya Hata mtume Hakuvaa Nguo Inayovuka vifundo Vya miguu.
4."Wanawake na wanaume kuchangamana wakati wa ibada ya hijja kwenye kaaba (ibada ya heshima kabisa) wakati huku misikitini hawachangamani"
Kila Ibada Na Taratibu Zake,Ibada Ya Swala Hairuhisiwi Kuchangamana Na Wanawake Lakini Ibada Za Hijja Huchangamana.Hapa Ni ibada Mbili tofauti Ibada ya Hijja Macca na Ibada ya Swala msikitini.
5."Wanawake kuwa maimam na kuongoza ibada zanye mchanganyiko wa jinsia zote"
Hii Kitu Katika Uislamu Haipo.Kama Uliona Basi Huenda Sio Waislamu Kwani Hawajafata Maamlisho Ya Quran na Hadith sahihi za Mtume Muhammad(S.A.W).Au Huenda Ni Shia,Dhehebu Linalodai Na Wao ni Waislamu Hali Ya Kuwa Hawaikubal Shahada.
NB:Fatilia Jambo Kwanza Kabla Ya Kuandika Thread,Pia Sio Vizuri Kuandika Sensitive Thread Mfano Thread Za dini Kama Huna Elimu Juu Ya Dini au Mada Husika