Tamaduni 10 za kidini ambazo hazimo kwenye Biblia au Quran

Naona uzao wa Is-hak na Yakuub umetajwa, lakini sijaona uzao wa Ishmael ukitajwa, je Ishmael hakuwa na uzao?
 
Duh, sijawahi kuwaza Kama hili fungu linaweza kutumika halo. Au mkuu umelilazimishia?
 
5: Mchungaji au askofu wa kike. Katika biblia mchungaji ni Mume wa mke mmoja sio mke wa Mume mmoja.
Kuoa ama kuolewa si chochote; Msikilize Yesu anasema nini:

Luka 20:34
Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa;

Luka 20:35
lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi;
 
Duh, sijawahi kuwaza Kama hili fungu linaweza kutumika halo. Au mkuu umelilazimishia?
Hapana sijakurupuka bali nimemuonesha kuwa katika Kristo hakuna maiti kwa maana hatufi bali tuna uzima wa milele.
Yohana 10:10
Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
 
Naona uzao wa Is-hak na Yakuub umetajwa, lakini sijaona uzao wa Ishmael ukitajwa, je Ishmael hakuwa na uzao?
Hoja yako ni ipi hasa? Ismael ametajwa pia kwenye aya nyingine ambazo nikikuwekea pia utahoji kwanini Ishaq na uzao wake haukutajwa kwenye aya hiyo...wote ni Mitume wa Mungu na tunawakubali bila ya kuwabagua.

Uzao wa Ismael ndio ametokea Mtume Muhammad (pbuh)
 
Utajuaje sunna hii au hadithi ile haipingani na quran wakati hilo jambo quran haijalisema?
Mtume ni kiigizo chema means sunnah zake ni halali.


Unaweza kujua kwa sababu unatumia elimu hapa ndo kuna hata hadithi sahili ,hadithi dhaifu ambazo hazisomwi na zimetolewa ni uongo ..Ukileta hadithi inayopinga na Qur an basi ni uongo.





kama sio waislamu kutumia muongozo wa Qur an moja basi mpaka leo uzushi ungekuwa mwingi kila mtu angekuja na story zake za kutunga.

Pia tambua uislamu unataka mtu aelewe kwanza huwezi kumuabudu Mungu ambaye humjui..Ndo maana elimu nyingi ya dini watu wanafundishwa Tawhid kwanza ili umjue Mungu .

Baada ya hapo unafundishwa Qur am sasa baada ya kuamini na umuamini Mungu ,sasa unasoma maneno yake ukiwa na yakini moyoni baada ya kusoma Tawahid.

Mwisho unakuja kusoma sunnah ,hadithi ,tarekhe ,sasa kwa kutumia elimu ya mwanza ndo utakuja kung'amua hizo hadithi ipi sahili ipi dhaifu.

Mtume ni kiigizo chema


kwa nn tunaamini sunnah ?
👇👇👇

Kasome Qur an 33:21 then uje hapa tuendelee...Hapo ndo tumeelekezwa kuwa kiigizo chetu ni nan.
 

Ufafanuzi Kwenye Qur'an

1."Ishmail kuwa Bora kuliko Isaka"

Kama Kichwa Cha Habari Kinavosema "Tamaduni Ambazo hazimo Kwenye Bibilia au Qur'an" Naomba Kuuliza Je Quran imesema Kuwa Isaka Ni Bora Kuzid Ismail mpka Sisi Tukabadili Kinyume.Kila Mtume Ana Nafasi Yake Mwenyezimungu Anajua Nani Ni Mbora Kati Yao.

2."Waislam Kufanya miujiza wakati mtume hakuwahi kufanya muujiza wowote ndani ya quran"

Je, Safari Ya Israa na Miraji Aloifanya mtume Muhammad(S.A.W) Haikuwa Miujiza?Fatilia Jambo Kwanza Kabla Ya Kuja na Hoja.
Waislamu Tunaishi Kwa Kufuata Qur'an
Na Hadithi Sahihi.
Hivyo kuna hadithi nyngi zinazoonyesha Miujiza aloitenda Mtume Muhammad (S.A.W) Mbali Na Muujiza Wa Safari ya Israa Na Miraj Kama
*Muujiza wa Kupasua Mwezi
(Chanzo:Quran 54:1-2, Al-Mīzān, 1391 AH, vol. 19, p. 65.)
*Muujiza wa kutoka Maji katika Vidole vya mtume Muhammad(S.A.W) watu wakanywa Na kutia Udhuu (Chanzo Sahih al-Bukhari 5639)
Miujiza ya mtume Muhammad (S.A.W) Iko Mingi.Pia Muhammad (S.A.W) Mwenyewe Ni Muujiza,Uliza Kwa Nini Aliwekwa Namba Moja Kwenye jarida La Most Influential People In The World

3:"Kuvaa suruali ambazo hazifiki chini.
Zile Suruali fupifupi"

Hakuna Ubaya katika kufanya Hvo kwani Ubaya Ni Kuvaa Nguo Ambavyo Haivuki Magoti
Pia ni Vizuri kwa Muislamu wa kiume kuvaa Nguo fupi isiyovuka Vifundo Vya miguu Kwani Nguo Zinazovuka Vifundo kwa Miguu Zinaweza Beba uchafu Hivo Kuitolea udhu Nguo yako.
Hapo Hakuna Ubaya Hata mtume Hakuvaa Nguo Inayovuka vifundo Vya miguu.

4."Wanawake na wanaume kuchangamana wakati wa ibada ya hijja kwenye kaaba (ibada ya heshima kabisa) wakati huku misikitini hawachangamani"

Kila Ibada Na Taratibu Zake,Ibada Ya Swala Hairuhisiwi Kuchangamana Na Wanawake Lakini Ibada Za Hijja Huchangamana.Hapa Ni ibada Mbili tofauti Ibada ya Hijja Macca na Ibada ya Swala msikitini.

5."Wanawake kuwa maimam na kuongoza ibada zanye mchanganyiko wa jinsia zote"

Hii Kitu Katika Uislamu Haipo.Kama Uliona Basi Huenda Sio Waislamu Kwani Hawajafata Maamlisho Ya Quran na Hadith sahihi za Mtume Muhammad(S.A.W).Au Huenda Ni Shia,Dhehebu Linalodai Na Wao ni Waislamu Hali Ya Kuwa Hawaikubal Shahada.

NB:Fatilia Jambo Kwanza Kabla Ya Kuandika Thread,Pia Sio Vizuri Kuandika Sensitive Thread Mfano Thread Za dini Kama Huna Elimu Juu Ya Dini au Mada Husika
 
1: Waislam wanafundisha ismail kuwa ndiye aliyerithi na kuendeleza kizazi cha ibrahim. Huu ndio msingi wa ubora wa mmoja baada ya mwingine. Lakini ukweli Quran na Biblia havimpi hizo sifa, bali Isihaka na uzao wake ndio unazungumzwa zaidi kuliko huyo Ishmail.


2: Mada haihitaji hadithi ilikuwa na mipaka ya kiquran na biblia. Naomba ukiri quran hakuna ushahidi wa miujiza ya Mtume isipokuwa kwenye hadithi sahihi zilizoandikwa miaka zaidi ya mia baada ya muhusika kufa.
Unaweza kuwaka list ya hadith sahihi?

3:Umetoa ushauri hukatoa aya. Hii inathibitisha kuvuka au kutokuvuka sio suala la kidini au lakiquran. Hakuna haja ya kuhukumiana kwa hilo.

4: Maelezo hayana aya, kupinga au kuunga mkono hoja yangu.

5: Hujaweka Aya inayosema hichokitu hakipo.

N.B asante kwa mchango mkuu. Kama kuna nyongeza zaidi uwanja uko wazi.
 
Kichwa cha habari ya majibu yote kimeanza vizuri. Ufafanuzi wa kwenye quran. Lakinj contents haina aya hata moja ya quran.

Nadhani hujanitendea haki.
 
Unaweza kunipa list ya hadith sahihi, dhaifu na potoshi

Angalau link nizifuatilie zaidi.
 
Kwa hiyo Ni dhambi mchungaji kuoa au kuolewa. Au suala la kuolewa na kuolewa haliwahusu wakristo.

Mkuu inawezekana sijakuelewa au wewe ndio hujamuelewa Yesu. Maana Petro alikuwa na mke na hakumwambia amuache ili asijeakaukosa ulimwengu mpya bali alimponya kabisa mama mkwe wake.
 
Aya hazina uhusiano na maombi kwa maiti.
Amwaminiye Yesu maana yake amhana dhambi. Na akitenda dhambi anatubu yanaisha. Akifa na dhambi huo uzima wa milele haumuhusu.
 
Mimi nadhan hukuusoma vizuri au hujasoma kabisa uislamu., katika uislamu hakuna Ibada yoyote itekelezwayo na waislam bila ya mafundisho kutoka katika Quran na khadith za Mtume S.A.W

Kwa mfano kama uligundua wanawake hawawezi kuwa maimamu basi ipo katika mafundisho ya Quran.,

Hii mada hapa si mahala pake, hizi ni mada zinahitaji kujadiliwa na watu wenye elimu hapa sana sana watu wanaweza kuongea visivyo kusemea katika dini wasioifahamu bora ungeacha tu
 
Hii aya inathibitisha hoja ya kwenye mada kuwa katika quran hakuna muujiza. Wala mtume hakufanya. Na tena inaonekana imekatazwa kabisa .

Waislam wanaofanya miujiza wanafanya kwa mapokeo tu.
 
Wewe ndio utulize kichwa usome hiyo aya vizuri!! Ujue kwanza ni sababu gani ilifanya Mungu alete miujiza kwa Mitume wake na nini kiliwapata watu mara baada ya kuikanusha hiyo miujiza (ishara).
Kama yalivyomaagizo mengine ya Mungu, kuna waliobadilishwa na miujizs na kunawaliodhihaki.

Hata sasa kiyama kunwawanaoamini na kunaodhihaki.

Sijaelewa hoja yako hapo.
 
Asante. Ni mafundisho ya Sunnah ila sio quran. Hapo nimekuelewa mkuu. Na kwa mujibu wa mada, hayo ni mafundisho nje ya kitabu kisicho na shaka.
 
wakuu nawashukuru. Ninawapongeza zaidi ndugu zangu wa umma wa waislam kujitahidi kujenga hoja.

Kwa upande wangu nimetosheka na majibu. Na ninaweza kuomba mada ifungwe. Kama kuna mtu bado anadukuduku badi anaweza kuendelea ila kwangu nimefurahi na kuna vitu nimejifunza.

Wabheja sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…