TAMISEMI: Gari lililohusika katika ajali ya Naibu Waziri Dugange lilikuwa binafsi na siyo la Serikali


Mbona haina Bima?

 
Ha ha ha wanasema alikuwa anamkwepa bodaboda
 
Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ina utaratibu mzuri kwenye kutoa taarifa tofauti kabisa na Chama Cha Mbowe. Ungekuta sasa karibu kila kada wa CHADEMA kapost anavyojua bila kujali kama chama kina msemaji.
 
We RPC ndio wa kupuuzwa kwa upotoshaji huu, hii taarifa ungemwandikia tu rais.

Kwanini plate namba ya hiyo gari imeondolewa kabla hata gari haijanyanyuliwa. Angalieni picha hapo kwenye tukio hakuna plate number.

RPC na viongozi wako wa kitaifa nyie ni binadamu km huyo mama ambaye mmemficha na kwenda kumzika km mnyama ili kumlinda mpumbavu moja km Dugange. Dugange ni nani nchi hii mpaka serikali itumie nguvu kubwa kupotosha watanzania na kumdhalilisha mtanzania mwingine, yaani huyo mama aliyekuwa naye

Mama Rais wetu watu km hawa ndio watakupa wakati mgumu sana, watu wataichukia serikali yako. Watanzania siyo wajinga wanajua ukweli wote ndio maana walikuwa wa kwanza kutoa taarifa hii mtandaoni.

We rais hushangai taarifa viongozi wako akiwepo huyo RPC walikata kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari mpaka habari ilipojulikana nchi nzima kuwa ni ya kweli na sasa anakuja RPC na taarifa za uwongo za kupotosha na yenye vitisho.

Nchi hii ni ya wananchi na wana akili, Otieno asifikiri anawazidi watanzania akili kisa ana hako kacheo. Km Magufuli alifia madarakani, cheo gani haitapita? Mwe na utu.
 
Sasa why katika hiyo picha mmeng'oa plate number if this is real?
Sahihi kabisa. Hapa kuna utata! Kwa nini hizo namba za usajili hazionekani kwenye gari? Na kamanda hajasema huyo Mheshimiwa alikuwa anatoka wapi! Kiasi cha kuwa peke yake kwenye gari.

Kwa nafasi na hadhi yake, bado maswali ni mengi kuliko majibu.
 
Kikubwa mh.waziri chamoto amekiona na tuna imani amejifunza jambo kupitia hii ajali na hatorudia tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…