TAMISEMI rasmi yaamua kuua elimu yetu Darasa 1 mpaka kidato cha 6? Nini kazi ya Wizara ya Elimu,OR na Necta?

Khadija Mtalame

Senior Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
185
Reaction score
715
Habari wanajukwaa,

Mimi nimekuwa mhanga kwelikweli wa elimu yetu hii ya tanzania hasa huku chini.

Juzi TAMISEMI wametoa mwongozo mpya ambao unatakiwa kutumia kufundishia kuanzia darasa la kwanza mpakakidato cha 6, ambapo kila mwalimu anatakiwa kuandaa kalenda la kufundisha na kwamba wanatak kuweka equality kwa wnaafunzi kuwa kwa mwanafunzi aliepo mwanza kama leo Alhamisi kasoma heabu kugawanya basi na mwanafunzi aliyeko Dar awe amesoma hesabu ya kugawanya muda ule ule.

Lengo lao ni kuweka uniformity kwa Tanzania nzima ambapo swala hili kiutendaji ni gumu sana ukizingatia idadi ya walimu waliopo na idadi ya wanafunzi.

Mfano: Kuna shule ipo Kongwa ina walimu watatu ikiwa na wanafunzi 478,je wanafunzi hao wataweza kufundishwa kwa njia hizo?

mwongozo ulivyotoka ni kwamba walimu wanatakiwa kuandaa kila kitu upya ikiwa ni pamoja na azimio la somo ambalo tayari walikuwa wameandaa,je kwa hali hiyo mwalimu mmoja anaefundisha physcs form 1 to f6 ataweza kufanya majukumu yote haya?

katika semina hizo nikiwa kama observer nisiejulikana kuna mdau aliuliza whats this for?

jibu lililotoka ni kwamba wanataka kuhakikisha kwamba,wanafunzi wakimaliza level flani wajiajiri..kuliko kusubiriwa kujiajiri

Kwa taarifa za gizani ni kwamba huu ni mkakati wa mwanamama aliepewa ujasiri kwa kukataa div 5 na GPA Ndalichako.., Waziri mpya kaingia kakuta tayari mambo yalishaiva na mwongozo umeshaandaliwa hivyo ukapelekwa OR kwa utekelezaji.

naendelea...
 
Habari wanajukwaa,

Mimi nimekuwa mhanga kwelikweli wa elimu yetu hii ya tanzania hasa huku chini.

Juzi TAMISEMI wametoa mwongozo mpya ambao unatakiwa kutumia kufundishia kuanzia darasa la kwanza mpakakidato cha 6, ambapo kila mwalimu anatakiwa kuandaa kalenda la kufundisha na kwamba wanatak kuweka equality kwa wnaafunzi kuwa kwa mwanafunzi aliepo mwanza kama leo Alhamisi kasoma heabu kugawanya basi na mwanafunzi aliyeko Dar awe amesoma hesabu ya kugawanya muda ule ule.

Lengo lao ni kuweka uniformity kwa Tanzania nzima ambapo swala hili kiutendaji ni gumu sana ukizingatia idadi ya walimu waliopo na idadi ya wanafunzi.

Mfano: Kuna shule ipo Kongwa ina walimu watatu ikiwa na wanafunzi 478,je wanafunzi hao wataweza kufundishwa kwa njia hizo?

naendelea...
Ajira 6,000 zinakuja

Hahahahahah Hangaya aisee
 
Kulazimisha uniformity wakati mazingira hayaruhusu ni kujidanganya, sijui watafanyaje ili shule zenye walimu wachache ziende sawa na shule nyingine zenye walimu wa kutosha kwa masomo husika.

Hawa wasipokuwa makini ndio wanaidumaza elimu yetu kabisa, kuwasubirisha wenye walimu wa kutosha ili waende sawa na wasio na walimu ni ujinga tu, naona hata hawa wanaoandaa hizo sera nao ni wajinga pia.
 
katika semina hizo nikiwa kama observer nisiejulikana kuna mdau aliuliza whats this for?

jibu lililotoka ni kwamba wanataka kuhakikisha kwamba,wanafunzi wakimaliza level flani wajiajiri..kuliko kusubiriwa kujiajiri
Huo mfumo unatoa skills gan za kumwezesha huyo mwanafunzi kujiajiri?

Kuna mda watu wanajibu kama hana akili timamu upumbavu kabsaa
 
yani nahisi wanaamua kupunguza idadi ya wanafunzi watakaokuwa wanaendelea na masomo yao ya juu
 
Kwahiyo kwa mujibu wa hayo maelekezo ikitokea labda emergency labda ya masomo kuhairishwa kwa shule x kwa siku 1 tayari wanakuwa nje ya muhtasari halafu vipi kuhusu uwezo wa wanafunzi kuelewa somo kwa sababu kuna kipindi mwalimu analazimika kurudia somo hata zaidi ya mara moja kama dakika 40 za kipindi ziliyeyuka bila madogo kudaka chochote
 
Kwahiyo kwa mujibu wa hayo maelekezo ikitokea labda emergency labda ya masomo kuhairishwa kwa shule x kwa siku 1 tayari wanakuwa nje ya muhtasari halafu vipi kuhusu uwezo wa wanafunzi kuelewa somo
hilo hawajangalia kabisa yani,lazima kila siku wanafunzi wasome tu,hakuna michezo wala extra works
 
Nakuunga mkono ndugu mleta mada,semina hizi,jana zimefanyika hapa tanga, kesho Kuna mtu kanidokeza wilaya ya mkuranga,kwa kweli huwezi kumpangia mtu mpango kazi,wakati kazi anafanya yeye na hujui katika utendaji wake anakumbana na matatizo gani,hapa tamisemi wanakwenda kuua elimu jumla.tuhifadhi bandiko hili wakati mitihani itakapofanyika na matokeo kutoka ndiyo tutabaini ukweli.
Shule nyingi Zina upungufu wa walimu kwa hiyo kuwa sawa katika ufundishaji ni kitu kisichowezekana kabisa,kila eneo Lina changamoto zake.
Ajabu mpaka mitihani yote qamwpanga ifanyike wakati mmoja,ya mid term, terminal,na annual kwa Tanzania Zina. Kitu ambacho ni kigumu kutekelezeka.chukua mfano mwlimu z Ana matatizo ya kiafya,hajafika kazini siku tatu,kw hiyo atakapo Rudi atalazimika kwenda spidi ili kuwa sawia na azimio lake la kazi.
 
inauma na inafikirisha sana wameona walimu ni watu wa kupangiwa na kuagizwa bila kushirikishwa chochote ,pia nasikia hii ni outcome ya NDALICHAKO
 
Back
Top Bottom