Habari wanajukwaa,
Mimi nimekuwa mhanga kwelikweli wa elimu yetu hii ya tanzania hasa huku chini.
Juzi TAMISEMI wametoa mwongozo mpya ambao unatakiwa kutumia kufundishia kuanzia darasa la kwanza mpakakidato cha 6, ambapo kila mwalimu anatakiwa kuandaa kalenda la kufundisha na kwamba wanatak kuweka equality kwa wnaafunzi kuwa kwa mwanafunzi aliepo mwanza kama leo Alhamisi kasoma heabu kugawanya basi na mwanafunzi aliyeko Dar awe amesoma hesabu ya kugawanya muda ule ule.
Lengo lao ni kuweka uniformity kwa Tanzania nzima ambapo swala hili kiutendaji ni gumu sana ukizingatia idadi ya walimu waliopo na idadi ya wanafunzi.
Mfano: Kuna shule ipo Kongwa ina walimu watatu ikiwa na wanafunzi 478,je wanafunzi hao wataweza kufundishwa kwa njia hizo?
mwongozo ulivyotoka ni kwamba walimu wanatakiwa kuandaa kila kitu upya ikiwa ni pamoja na azimio la somo ambalo tayari walikuwa wameandaa,je kwa hali hiyo mwalimu mmoja anaefundisha physcs form 1 to f6 ataweza kufanya majukumu yote haya?
katika semina hizo nikiwa kama observer nisiejulikana kuna mdau aliuliza whats this for?
jibu lililotoka ni kwamba wanataka kuhakikisha kwamba,wanafunzi wakimaliza level flani wajiajiri..kuliko kusubiriwa kujiajiri
Kwa taarifa za gizani ni kwamba huu ni mkakati wa mwanamama aliepewa ujasiri kwa kukataa div 5 na GPA Ndalichako.., Waziri mpya kaingia kakuta tayari mambo yalishaiva na mwongozo umeshaandaliwa hivyo ukapelekwa OR kwa utekelezaji.
naendelea...