TAMISEMI rasmi yaamua kuua elimu yetu Darasa 1 mpaka kidato cha 6? Nini kazi ya Wizara ya Elimu,OR na Necta?

TAMISEMI rasmi yaamua kuua elimu yetu Darasa 1 mpaka kidato cha 6? Nini kazi ya Wizara ya Elimu,OR na Necta?

Mi binafsi naomba Mama mheshimiwa Rais Samia anitafutie kitengo chochote angalau niweze kupambana na watu wazima,hisabati wanaelewa watoto wachache bila fimbo ...naadhibu but moyo wangu unajitengenezea chuki hasa nikiwa alone nimejituliza nahisi kama wanaumia tunavyowaadhibu.
 
inabidi tuchukue hatua kali kabisa kama wadau wa elimu
Hapo mimi naona vumbi tu kama si matope. Haiwezekani kuufuata mwongozo wa TAMISEMI halafu tukategemea kupata matokeo. Kuna somo mfano BIOLOGY, huwezi kufundisha mada kwa kuzingatia mpangilio wa mada za muhtasari, kwa sababu kuna baadhi ya mada ambazo mwalimu hutakiwa kuzifundisha kwa kuzingatia majira ya mwaka mfano masika, vuli au kiangazi ili kuongeza ufanisi wa somo kwa sababu ya upatikanaji wa zana halisi za ufundishaji na ujifunzaji. Mfano mada inayohusiana na maua haiwezi kufundishwa mwezi wa saba sababu wakati huo mimea mingi huwa imekauka kutokana na kiangazi. Hivyo mwalimu huirejesha nyuma mada hiyo hadi mwezi wa pili au wa tatu ili kurahisisha upatikanaji wa zana halisi mfano maua ambapo mwalimu hutakiwa kuwatoa nje wanafunzi na kuwapeleka katika mazingira yanayoizunguka shule na kujionea maua halisi, kuyagusa au hata kunusa na hivyo kuwajengea kumbukumbu ya muda mrefu juu ya somo husika. Huu mchezo wa wataalamu kujifungia ofisini na kutunga muongozo huu usiotekelezeka, utaua ama kudhoofisha elimu yetu.
 
Nakuunga mkono ndugu mleta mada,semina hizi,jana zimefanyika hapa tanga, kesho Kuna mtu kanidokeza wilaya ya mkuranga,kwa kweli huwezi kumpangia mtu mpango kazi,wakati kazi anafanya yeye na hujui katika utendaji wake anakumbana na matatizo gani,hapa tamisemi wanakwenda kuua elimu jumla.tuhifadhi bandiko hili wakati mitihani itakapofanyika na matokeo kutoka ndiyo tutabaini ukweli.
Shule nyingi Zina upungufu wa walimu kwa hiyo kuwa sawa katika ufundishaji ni kitu kisichowezekana kabisa,kila eneo Lina changamoto zake.
Ajabu mpaka mitihani yote qamwpanga ifanyike wakati mmoja,ya mid term, terminal,na annual kwa Tanzania Zina. Kitu ambacho ni kigumu kutekelezeka.chukua mfano mwlimu z Ana matatizo ya kiafya,hajafika kazini siku tatu,kw hiyo atakapo Rudi atalazimika kwenda spidi ili kuwa sawia na azimio lake la kazi.
Lengo ni nini?
Wanafunzi wote kufundishwa kilekile kwa siku hiyo hiyo, labda lengo ni kuhakikisha kuwa Mtaala, 'Syllabus' inakamilika, lakini kueleweka na kuelewa ni 'personal skills' za Mwalimu.
Ukiongeza suala la upungufu wa Walimu na hususan Walimu wa Hisabati na Sayansi, huu unaweza kuwa "Mradi wa Wajanja kula hela za Umma".
Hii progaramu imepangiwa Bajeti ya Bilioni ngapi?
 
Habari wanajukwaa,

Mimi nimekuwa mhanga kwelikweli wa elimu yetu hii ya tanzania hasa huku chini.

Juzi TAMISEMI wametoa mwongozo mpya ambao unatakiwa kutumia kufundishia kuanzia darasa la kwanza mpakakidato cha 6, ambapo kila mwalimu anatakiwa kuandaa kalenda la kufundisha na kwamba wanatak kuweka equality kwa wnaafunzi kuwa kwa mwanafunzi aliepo mwanza kama leo Alhamisi kasoma heabu kugawanya basi na mwanafunzi aliyeko Dar awe amesoma hesabu ya kugawanya muda ule ule.

Lengo lao ni kuweka uniformity kwa Tanzania nzima ambapo swala hili kiutendaji ni gumu sana ukizingatia idadi ya walimu waliopo na idadi ya wanafunzi.

Mfano: Kuna shule ipo Kongwa ina walimu watatu ikiwa na wanafunzi 478,je wanafunzi hao wataweza kufundishwa kwa njia hizo?

mwongozo ulivyotoka ni kwamba walimu wanatakiwa kuandaa kila kitu upya ikiwa ni pamoja na azimio la somo ambalo tayari walikuwa wameandaa,je kwa hali hiyo mwalimu mmoja anaefundisha physcs form 1 to f6 ataweza kufanya majukumu yote haya?

katika semina hizo nikiwa kama observer nisiejulikana kuna mdau aliuliza whats this for?

jibu lililotoka ni kwamba wanataka kuhakikisha kwamba,wanafunzi wakimaliza level flani wajiajiri..kuliko kusubiriwa kujiajiri

Kwa taarifa za gizani ni kwamba huu ni mkakati wa mwanamama aliepewa ujasiri kwa kukataa div 5 na GPA Ndalichako.., Waziri mpya kaingia kakuta tayari mambo yalishaiva na mwongozo umeshaandaliwa hivyo ukapelekwa OR kwa utekelezaji.

naendelea...
Unge-share na huo mwongozo.
 
Mi binafsi naomba Mama mheshimiwa Rais Samia anitafutie kitengo chochote angalau niweze kupambana na watu wazima,hisabati wanaelewa watoto wachache bila fimbo ...naadhibu but moyo wangu unajitengenezea chuki hasa nikiwa alone nimejituliza nahisi kama wanaumia tunavyowaadhibu.
khasanet sana madam
 
Tabora ya simiyu au rukwa ya shinyanga?tatizo elimu yetu inakuwa haina usukani unaoeleweka
 
Mwalimu mwenyewe kaajiliwa hajui hata kujiajiri ni nini,then aje amfundishe mwanafunzi kujiajiri!
Skills,atitudes na experience aliyonayo mwalimu ni KWA masomo yake husika suala la kujiajiri ni degree inayojitegemea
 
Back
Top Bottom