TAMISEMI rasmi yaamua kuua elimu yetu Darasa 1 mpaka kidato cha 6? Nini kazi ya Wizara ya Elimu,OR na Necta?

Mi binafsi naomba Mama mheshimiwa Rais Samia anitafutie kitengo chochote angalau niweze kupambana na watu wazima,hisabati wanaelewa watoto wachache bila fimbo ...naadhibu but moyo wangu unajitengenezea chuki hasa nikiwa alone nimejituliza nahisi kama wanaumia tunavyowaadhibu.
 
inabidi tuchukue hatua kali kabisa kama wadau wa elimu
Hapo mimi naona vumbi tu kama si matope. Haiwezekani kuufuata mwongozo wa TAMISEMI halafu tukategemea kupata matokeo. Kuna somo mfano BIOLOGY, huwezi kufundisha mada kwa kuzingatia mpangilio wa mada za muhtasari, kwa sababu kuna baadhi ya mada ambazo mwalimu hutakiwa kuzifundisha kwa kuzingatia majira ya mwaka mfano masika, vuli au kiangazi ili kuongeza ufanisi wa somo kwa sababu ya upatikanaji wa zana halisi za ufundishaji na ujifunzaji. Mfano mada inayohusiana na maua haiwezi kufundishwa mwezi wa saba sababu wakati huo mimea mingi huwa imekauka kutokana na kiangazi. Hivyo mwalimu huirejesha nyuma mada hiyo hadi mwezi wa pili au wa tatu ili kurahisisha upatikanaji wa zana halisi mfano maua ambapo mwalimu hutakiwa kuwatoa nje wanafunzi na kuwapeleka katika mazingira yanayoizunguka shule na kujionea maua halisi, kuyagusa au hata kunusa na hivyo kuwajengea kumbukumbu ya muda mrefu juu ya somo husika. Huu mchezo wa wataalamu kujifungia ofisini na kutunga muongozo huu usiotekelezeka, utaua ama kudhoofisha elimu yetu.
 
Lengo ni nini?
Wanafunzi wote kufundishwa kilekile kwa siku hiyo hiyo, labda lengo ni kuhakikisha kuwa Mtaala, 'Syllabus' inakamilika, lakini kueleweka na kuelewa ni 'personal skills' za Mwalimu.
Ukiongeza suala la upungufu wa Walimu na hususan Walimu wa Hisabati na Sayansi, huu unaweza kuwa "Mradi wa Wajanja kula hela za Umma".
Hii progaramu imepangiwa Bajeti ya Bilioni ngapi?
 
Unge-share na huo mwongozo.
 
khasanet sana madam
 
Tabora ya simiyu au rukwa ya shinyanga?tatizo elimu yetu inakuwa haina usukani unaoeleweka
 
Mwalimu mwenyewe kaajiliwa hajui hata kujiajiri ni nini,then aje amfundishe mwanafunzi kujiajiri!
Skills,atitudes na experience aliyonayo mwalimu ni KWA masomo yake husika suala la kujiajiri ni degree inayojitegemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…