DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Amekadiria itakuwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuandikisha kwenyewe unataja jina na mwaka, hiyo teknolojia imetoka wapi?Kujumlisha kiteknolojia kunachukua dakika ngapi?
Hata 10m hawafiki.Amekadiria itakuwa
10 million hawawezi kufikaHata 10m hawafiki.
Waziri anafikiri kila mtu ni mjinga ,kuna demu wangu ni mtendaji mpaka sasa yupo ofisini anawasubiri waandikishaji wampelekee idadi ya leoZoezi lilikuwa manual, na limefungwa jioni hii hii, wamekusanyaje matokeo yote na kupata idadi hiyo? Bado kuna wajinga wa hivyo?
Zoezi lilikuwa manual, na limefungwa jioni hii hii, wamekusanyaje matokeo yote na kupata idadi hiyo? Bado kuna wajinga wa hivyo?
Kabisa, maana hata kesho bado angeleta idadi ya uongo, sasa alikuwa na haja gani ya kuitaja leo? Hii tabia ya kutangaza idadi ya uongo ya wapiga kura nilianza kuiona kwa uwazi wakati wa Magufuli, kwa sasa naona ndio imekuwa fashion.Yaani hata mimi nashangaa hapa. Alaf kwa nini watangaze takwimu harakaharaka, wanataka ku justify nini?
Waliandikisha kiteknolojia?Kujumlisha kiteknolojia kunachukua dakika ngapi?
Mkwe mpishi wa takwimuWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kufikia Oktoba 19, 2024, Jumla ya watanzania wenye sifa Milioni 26,769,995 sawa na asilimia 81% wamejiandikisha kwenye daftari la Mpigakura, tayari kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Waziri Mchengerwa ametoa takwimu hizo leo Jumapili Oktoba 20, 2024 akiwa Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, akiitaja Mikoa ya Tanga, Pwani, Mwanza, Dar Es salaam na Dodoma kuwa Vinara katika uandikishaji huo.
Mhe. Mchengerwa kando ya Kutangaza kutoongezwa kwa siku za kujiandikisha, amewashukuru watanzania wote waliotumia haki yao Kikatiba katika kujiandikisha kwenye Daftari hilo, akiwataka pia wale wote wenye sifa za kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeza kwa wingi kuanzia Oktoba 26, 2024 ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali kwenye serikali za Mitaa.
Mhe. Mchengerwa kadhalika ametoa wito kwa wasimamizi wa Uchaguzi na wadau wote wa Uchaguzi kuendelea kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia Uchaguzi huo, akihimiza pia suala la usimamizi na utekelezaji wa falsafa ya 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha haki, usawa na Uhuru wa kuchagua unatamalaki kwenye Uchaguzi huo wa baadae mwaka huu.