LGE2024 TAMISEMI: Wananchi 26,769,995 wamejiandikisha katika Daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi kufikia Oktoba 19, 2024

LGE2024 TAMISEMI: Wananchi 26,769,995 wamejiandikisha katika Daftari la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi kufikia Oktoba 19, 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Waongo hawa, ni data za kupika hizi....

Watu wanatumia njia za karne ya 14 kuandikisha halafu eti wanatoa data hata kabla zoezi halijaisha....

NEC wenyewe waliokuwa na mifumo ya kielekroniki kuandikisha/kuboresha daftari la wapiga kura zoezi lililoisha karibu mwezi umepita mpaka sasa hawajatoa takwimu za waliandikisha kwa jumla yake nchi nzima...

Hawa wanaoandikisha manually kwa kutumia madaftari ya MSOMI wamewezaje kutoa data za. nchi nzima hata kabla zoezi lenyewe halijaisha kama sio data za kupika tu hizi..?

Wasitiletee balaa hawa maana safari hii ujinga na upumbavu wao wa mwaka 2019 hautafanikiwa...!!
 
Yaani hata mimi nashangaa hapa. Alaf kwa nini watangaze takwimu harakaharaka, wanataka ku justify nini?
Kabisa, maana hata kesho bado angeleta idadi ya uongo, sasa alikuwa na haja gani ya kuitaja leo? Hii tabia ya kutangaza idadi ya uongo ya wapiga kura nilianza kuiona kwa uwazi wakati wa Magufuli, kwa sasa naona ndio imekuwa fashion.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema kufikia Oktoba 19, 2024, Jumla ya watanzania wenye sifa Milioni 26,769,995 sawa na asilimia 81% wamejiandikisha kwenye daftari la Mpigakura, tayari kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Waziri Mchengerwa ametoa takwimu hizo leo Jumapili Oktoba 20, 2024 akiwa Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, akiitaja Mikoa ya Tanga, Pwani, Mwanza, Dar Es salaam na Dodoma kuwa Vinara katika uandikishaji huo.

Mhe. Mchengerwa kando ya Kutangaza kutoongezwa kwa siku za kujiandikisha, amewashukuru watanzania wote waliotumia haki yao Kikatiba katika kujiandikisha kwenye Daftari hilo, akiwataka pia wale wote wenye sifa za kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi kujitokeza kwa wingi kuanzia Oktoba 26, 2024 ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali kwenye serikali za Mitaa.

Mhe. Mchengerwa kadhalika ametoa wito kwa wasimamizi wa Uchaguzi na wadau wote wa Uchaguzi kuendelea kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia Uchaguzi huo, akihimiza pia suala la usimamizi na utekelezaji wa falsafa ya 4R za Rais Samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha haki, usawa na Uhuru wa kuchagua unatamalaki kwenye Uchaguzi huo wa baadae mwaka huu.
Mkwe mpishi wa takwimu
 
Back
Top Bottom