TAMISEMI: Zipo Shule ambazo Wanafunzi hawajawahi kuwaona Walimu wa Physics na Hesabu

TAMISEMI: Zipo Shule ambazo Wanafunzi hawajawahi kuwaona Walimu wa Physics na Hesabu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri Ummy Mwalimu amesema kuna Shule takriban 1,000 za Sekondari ambazo Wanafunzi hawajawahi kukutana na Mwalimu wa somo la Physics uso kwa uso.

Akiwa Bungeni leo, pia amesema zipo Shule zipatazo 400 ambazo Wanafunzi wa Sekondari hawajawahi kuona Mwalimu wa Hesabu akiingia Darasani.

Ametoa maelezo hayo baada ya Wabunge kuhoji ni lini Serikali itapeleka Walimu wa Sayansi katika Shule akikiri kuwepo Uhaba.

Huwa sielewi CCM huwa wanapata wapi uhalali wa kuomba kuendelea kuongoza hii nchi na wanaowaunga mkono sijui huwa ni vipofu na viziwi!
Kweni unadhani ni chama gani kikiongoza ndiyo kutafanya nchi kua kama Ulaya ghafla? Watu hua mna upuuzi tu,mimi sina chama lakini najua hulka za waTanzania. Kila atakaye ongoza nchi atalaumiwa tu au kila chama kitalaumiwa tu maana watu huishi kwa matamanio ambayo mtu mwingine hawezi kuyatekeleza kwa wakati mmoja.

Na kitu hua naona pia watu wengi wa sasa ni vitoto vya kuzaliwa 1990 kuja sasa, havijui nchi imetoka wapi na sasa tuko wapi.
 
Serikali yetu bana, kwenye mambo ya msingi/maendeleo utasikia pesa hakuna. Vitu visivyo na tija kwa Taifa mpunga upo, leo wakisema posho zao zitoke kuwa laki 2 iwe milioni pesa itapatikana na watajilipa
Mambo yao hayawezi kukwama.

Kuhusu ajira utawasikia, tatizo la ajira liko dunia nzima.

Hapo ndio utashangaa na huko duniani nafasi za kazi zipo ila pesa za kuajiri watu ndio zinakosekana kama hapa kwetu?
 
Watafute vyanzo .....mapato waajiri walimu wapya sayansi zaidi
 
Kweni unadhani ni chama gani kikiongoza ndiyo kutafanya nchi kua kama Ulaya ghafla?watu hua mna upuuzi tu,mimi sina chama lakini najua hulka za waTanzania...kila atakaye ongoza nchi atalaumiwa tu au kila chama kitalaumiwa tu maana watu huishi kwa matamanio ambayo mtu mwingine hawezi kuyatekeleza kwa wakati mmoja.

Na kitu hua naona pia watu wengi wa sasa ni vitoto vya kuzaliwa 1990 kuja sasa,havijui nchi imetoka wapi na sasa tuko wapi
Ukweli ni kwamba hata kama CCM ikitoka madarakani, kitabadilika chama tu, nyuso za watawala zitakuwa zile zile.

Hao watu waliopo CCM siku ikiondoka madarakani, na watu hao hao unaowaona CCM sasa hivi watahamia chama chenye madaraka.

Wanasema palipo na mzoga ndipo wakutanikiapo tai. Ndio maana wanaokosa nafasi CCM wanajiunga CHADEMA na siyo NLD ya Makaidi.

Wao wanasiasa siyo masikini, wanakula bata na maisha yao ni mazuri. Wanaishi, ila wewe wanakuaminisha kuishi vizuri ni mpaka siku CCM ikitoka madarakani🙄
 
Kweni unadhani ni chama gani kikiongoza ndiyo kutafanya nchi kua kama Ulaya ghafla?watu hua mna upuuzi tu,mimi sina chama lakini najua hulka za waTanzania...kila atakaye ongoza nchi atalaumiwa tu au kila chama kitalaumiwa tu maana watu huishi kwa matamanio ambayo mtu mwingine hawezi kuyatekeleza kwa wakati mmoja.

Na kitu hua naona pia watu wengi wa sasa ni vitoto vya kuzaliwa 1990 kuja sasa,havijui nchi imetoka wapi na sasa tuko wapi
Unaonekana umeridhika sana, that's good for you, kwa wenzako CCM imefeli; miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru bado tunapigana na wale maadui watatu (ujinga - ukosefu wa walimu wa sayansi, maradhi, na umasikini).
 
Ukifikiria kuwa ni serikali hii hii iliyonunua midege lukuki kwa cash ambayo sasa inaleta hasara kwa atcl ....na pia kujenga airport kule chattle.....unapata kizunguzungu! Ndio sababu hata "mabeberu" wanatudharau sana.
 
Waziri Ummy Mwalimu amesema kuna Shule takriban 1,000 za Sekondari ambazo Wanafunzi hawajawahi kukutana na Mwalimu wa somo la Physics uso kwa uso

Akiwa Bungeni leo, pia amesema zipo Shule zipatazo 400 ambazo Wanafunzi wa Sekondari hawajawahi kuona Mwalimu wa Hesabu akiingia Darasani

Ametoa maelezo hayo baada ya Wabunge kuhoji ni lini Serikali itapeleka Walimu wa Sayansi katika Shule akikiri kuwepo Uhaba
Mh, hata wakati unasoma Physics na hesabu ilikusumbua na hukuwa na mwalimu na matokeo yake hukufaulu. Ila kwa Sasa walimu hao wapi mitaani wanaohitaji ajira
 
Waziri Ummy Mwalimu amesema kuna Shule takriban 1,000 za Sekondari ambazo Wanafunzi hawajawahi kukutana na Mwalimu wa somo la Physics uso kwa uso

Akiwa Bungeni leo, pia amesema zipo Shule zipatazo 400 ambazo Wanafunzi wa Sekondari hawajawahi kuona Mwalimu wa Hesabu akiingia Darasani

Ametoa maelezo hayo baada ya Wabunge kuhoji ni lini Serikali itapeleka Walimu wa Sayansi katika Shule akikiri kuwepo Uhaba
Shujaa alikuwa anafanya nini sasa?
 
Zama zimebadilika kweli...! Sisi enzi zetu ilikua shule hazikosi walimu ya physics na mathematics, na hata kama hawakua waajiriwa wa serikali lakini shule ziliweza kuwaajiri walimu hao. Mtaani kukawa hamna waalimu wanademka demka..!

Leo hii shule hazina walimu eti..! Na mtaani waalimu wapo tu kibao na serikali haiwezi kuwaajiri. Tunaona nafasi 600 za walimu zimetolewa walioomba 120K...! Tanzania yangu ya Viwanda.
 
kuna mambo ya aibu Nchi hii!!!??
 
Walimu wa science wachache sana miaka yote.
Tamisemi na wizara ya elimu watafute njia sahihi ya kuondoa hili tatizo
 
Back
Top Bottom