TAMISEMI: Zipo Shule ambazo Wanafunzi hawajawahi kuwaona Walimu wa Physics na Hesabu

TAMISEMI: Zipo Shule ambazo Wanafunzi hawajawahi kuwaona Walimu wa Physics na Hesabu

Walikuwa busy kuajiri UV CCM ambao hawajasoma science ...hii nchi ilorogwa sio bute
 
Huwa sielewi CCM huwa wanapata wapi uhalali wa kuomba kuendelea kuongoza hii nchi na wanaowaunga mkono sijui huwa ni vipofu na viziwi!
Ahsante sana ndugu kwa kufunguka ya moyoni.
CCM wanajua fika kuwa asilimia kubwa ya raia wa Tanzania ni wajinga, hivyo ujinga ndio mtaji wao!
Wanaowaunga mkono 99.95% ni hawa wananchi wajinga wenye umaskini wa fikra na 0.05% ni wanufaika wa CCM ambao ni familia za viongozi wa CCM, wafanyabiashara wakubwa, baadhi ya watumishi wa serekali. Hakuna kipofu wala kiziwi bali kuna mjinga na mnufaika!
 
Ukweli ni kwamba hata kama CCM ikitoka madarakani, kitabadilika chama tu, nyuso za watawala zitakuwa zile zile.

Hao watu waliopo CCM siku ikiondoka madarakani, na wao wanahamia chama chenye madaraka.

Wanasema palipo na mzoga ndipo wakutanikiapo tai. Ndio maana wanaokosa nafasi CCM wanajiunga CHADEMA na siyo NLD ya Makaidi.

Wao wanasiasa siyo masikini, wanakula bata na maisha yao ni mazuri. Wanaishi, ila wewe wanakuaminisha kuishi vizuri ni mpaka siku CCM ikitoka madarakani🙄
Mifumo ndio inayoongoza nchi na wala sio chama. Nchi yetu ni ya vyama vingi na ina mifumo mibovu hivyo ni wazi kabisa ulivyosema yeyote atakaepata nafasi anaweza kuitumia hii mifumo iliopo kuendeleza madudu. Mifumo iliopo ni ya kuilinda CCM isitoke madarakani na sio ya kuiendeleza nchi tatizo liko hapo, mkuu wewe unashaurije?
 
Mfumo bora utajengwa na mwananchi mwenyewe.

Aidha kupitia maandamano/machafuko kama ilivyotokea Kenya na Zanzibar au kupitia mgongano wa fikra.

Mfano ingetokea bunge likawa na upinzani 51%+ hata kama Rais awe CCM, automatic mfumo ungebadilika. Ingawa hili ni gumu hapa kwetu kwasababu mwenye madaraka ana rundo la incentives za kutoa rushwa ( vyeo na pesa ) na hivyo anaweza kugawanya watu.

Huo mfumo uliopo hakuna chama au mwanasiasa asiyeupenda.

Ni lazima wananchi watafute namna ya kuwafanya wanasiasa wawaheshimu.
 
Naongelea uwepo wa Jobless walimu wa Physics na Mathematics mtaani.

Na nikaongezea uwepo wa wataalamu wa Afya ( nikiwemo mimi ) Jobless mtaani tangu 2016.

Una kingine ?

Waambie walimu 6 kati ya hao wengi waje hapa Namanyere, wilaya ya Nkasi mkoa wa Rukwa waingie kwenye ajira moja kwa moja

Hukumsikia waziri akisisitiza hilo?
 
Kauli imekaa kisiasa, anyooke tu walimu hawapo uhaba ni mkubwa, kinachoendelea ni kuzidi tu kumwaga idadi kubwa ya wanafunzi shule za sekondari wasiojua hata kuandika....sijui hiyo miaka 7 ya msingi ilikuaje.
Elimu ya hii nchi ina mazingaombwe mengi sana.
 
Waambie walimu 6 kati ya hao wengi waje hapa Namanyere, wilaya ya Nkasi mkoa wa Rukwa waingie kwenye ajira moja kwa moja

Hukumsikia waziri akisisitiza hilo?
Waziri yupi kasisitiza ?

Kuna majina ya walimu 80,000 mpaka sasa yako huko TAMISEMI au anataka yapi?

Tena hao ni ukiondoa graduates wa 2020 walioambiwa wasiombe.
 
Mfumo bora utajengwa na mwananchi mwenyewe.

Aidha kupitia maandamano/machafuko kama ilivyotokea Kenya na Zanzibar au kupitia mgongano wa fikra.

Mfano ingetokea bunge likawa na upinzani 51%+ hata kama Rais awe CCM, automatic mfumo ungebadilika. Ingawa hili ni gumu hapa kwetu kwasababu mwenye madaraka ana rundo la incentives za kutoa rushwa ( vyeo na pesa ) na hivyo anaweza kugawanya watu.

Huo mfumo uliopo hakuna chama au mwanasiasa asiyeupenda.

Ni lazima wananchi watafute namna ya kuwafanya wanasiasa wawaheshimu.
Pamoja na vurugu zilizofanyika Kenya na Znz bado hawana mifumo bora
Bunge likiwa na 51% au zaidi ya wapinzani rais hawezi kuunda serekali.
Mfumo uliopo haupendwi na wapinzani kwakuwa unawanyima haki ya kushinda uchaguzi mkuu.
Wananchi hatuwezi kujenga mifumo imara ila tunaweza kushawishi, watakaojenga mifumo imara ni wanasiasa hasa walio madarakani ambao watakubali kulitumikia Taifa na sio matumbo yao. Tunawapataje hawa wanasiasa watakaolitumikia Taifa? Tutawatambuaje wanapoomba kuchaguliwa? Tunaweza kujua huyu ndio huyu sio?
Ni mawazo yangu tu Mkuu
 
Binafsi naamini kila kitu ni hatua, Kenya na Zanzibar hawana mifumo hiyo lakini wako mbele yetu.

Ni ngumu kujenga mfumo kwa ushawishi wa kura hasa kwenye nchi masikini na yenye ujinga mwingi kama yetu.
 
Zanzibar sio nchi kamili wanajitawala kwa kiwango kidogo tu, Ni kweli Kenya wapo mbele yetu
Umelenga penyewe, bila kufuta huu ujinga, tutakuwa tunapigia mbuzi tarumbeta. Tunafutaje huu ujinga ndugu yangu?
 
Huwa sielewi CCM huwa wanapata wapi uhalali wa kuomba kuendelea kuongoza hii nchi na wanaowaunga mkono sijui huwa ni vipofu na viziwi!
Lakini kumbuka ccm walikimbia uchaguzi mwaka jana na wakaamua kujitangaza washindi kwa mtutu wa bunduki hivyo kutawala pasipo uhalali.
 
Zanzibar sio nchi kamili wanajitawala kwa kiwango kidogo tu, Ni kweli Kenya wapo mbele yetu
Umelenga penyewe, bila kufuta huu ujinga, tutakuwa tunapigia mbuzi tarumbeta. Tunafutaje huu ujinga ndugu yangu?
Kwa kuendelea kufanya harakati. Siasa za 1995 wakati vyama vingi vinaanza siyo siasa za sasa hivi.

Mambo yanabadilika taratibu muhimu ni HATUA.
 
UFUMBUZI WA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA WALIMU WA SAYANSI, TAMISEMI WATOA UFAFANUZI
Katika Ajira mpya 6949 Za Walimu zilizotangazwa hivi karibu tumetangaza ajira Walimu wa Sayansi wa kutosha na tutawapeleka walimu hao kwenye shule zote ambazo hazina walimu wa hesabu, physics na Kemia. Changamoto hii haitakuwepo tena kupitia Ajira mpya tulizotangaza
 
kama hamna graduate wa hesabu na fizikia bora wachukue enginer wakafundishe naona wako vzur katika hy masomo kuliko kuangaika mtaani bila ajira za kueleweka
 
Serikali yetu bana, kwenye mambo ya msingi/maendeleo utasikia pesa hakuna....vitu visivyo na tija kwa Taifa mpunga upo, leo wakisema posho zao zitoke kuwa laki 2 iwe milioni pesa itapatikana na watajilipa
[emoji16][emoji16]wawakilishi wa wananchi[emoji119]
 
Waziri Ummy Mwalimu amesema kuna Shule takriban 1,000 za Sekondari ambazo Wanafunzi hawajawahi kukutana na Mwalimu wa somo la Physics uso kwa uso.

Akiwa Bungeni leo, pia amesema zipo Shule zipatazo 400 ambazo Wanafunzi wa Sekondari hawajawahi kuona Mwalimu wa Hesabu akiingia Darasani.

Ametoa maelezo hayo baada ya Wabunge kuhoji ni lini Serikali itapeleka Walimu wa Sayansi katika Shule akikiri kuwepo Uhaba.

Idadi ya watoto inaongezeka kila mwaka shule na walimu ni kulenga kwa manati unategemea tatizo litakwisha?
 
Back
Top Bottom