TAMISEMI: Zipo Shule ambazo Wanafunzi hawajawahi kuwaona Walimu wa Physics na Hesabu

Haya ndio maajabu ya elimu ya bongo

Tunaambiwa shule hazina walimu wa sayansi ingawa walimu hao wamejaa tele mtaani

Tukiwambia kwanini msiajiri waliopo mtaani wanasema pesa hakuna lakini kwenye vikao wanalipana posho na perdiem za kufa mtu

Huko mashuleni ndo kituko zaidi. Wanafunzi wanasoma sayansi bila walimu na ufaulu unaongezeka kila mwaka alafu tukisema necta wanachakachua matokeo kuwaridhisha wazazi na wanafunzi wanabisha.

Maajabu hayatakaa yakaisha nchi hii
 
Wewe sijui huwa unabisha kitu gani aisee!

Kwahiyo hilo lundo la walimu 80,000 walimu walioomba ajira 6,000 unadhani wote ni Arts au wanafundisha shule binafsi ?

Halafu unazungumzia shule binafsi zipi, hizo zilizopitiwa na wimbi la CORONA ?

CCM mna shule zenu za Jumuiya ya Wazazi zilizokuwa chini ya Bulembo sasa hivi ziko wapi, zimeajiri walimu wangapi ?

Afya tu yenye uhaba mkubwa wa watumishi, waombaji 31,000 wameomba ajira 2,700 na wenyewe wako sekta binafsi?
 
Saa nyingine kubishana na MATAGA a.k.a. sukumagang ni kupoteza muda tuuu!
 
Ingekuwa nchi nyingine serikali ingeshitakiwa na viongozi kuondolewa, haiwezekani wabunge kujipangia posho kubwa wakati wanafunzi wanakosa walimu wa kuwafundisha ilibidi tuagize walimu hata kutoka nje ya nchi ikiwa hatuna walimu wa kutosha.
 
😂😂😂😂😂
Watawaona vipi hao waalimu na hawajawaajiri? Hao wanafunzi waje wawaone huku hao walimu tunauza nao karanga stendi.
 
Elimu bure nayo kwa kiasi chake imechangia upuuzi huu, mi nakumbuka wakati nasoma shule yetu ilikuwa na mwalimu mmoja mwajiliwa yaani headmaster ila kilichofanyika tulikuwa tunachanga hela ya taaluma ambayo kwa mwaka haikuwa kubwa na hela hyo ilitumika kuwaajiri form four leaver na six leaver wakatufundishe kiukweli mpaka namaliza form four nilikuwa nafundishwa na leavers hao,ila sa hivi kituko graduates wamejazana mtaani na shuleni walimu hawatoshi,na shule haziwezi kuwaajiri kwa maana elimu bure hata chaki ni za bajeti
 
Elimu ya Tanzania kwa sasa imo kwenye majaribu mengi sana, ni tofauti kubwa na tulivyosoma sisi miaka ya 90 ambapo wewe mwanafunzi ndiyo unamkimbia Mwalimu...
Yaani nisote mtaani miaka sita alafu ndo nipate uo ualimu nijisumbue na mapindi uwiii
 
Yaani kipindi za mwendazake matokeo yanashuka vipi ani?kwa vyovyote vile ilibid yapande tu
 
Tatizo siyo elimu bure. Janga lilikuwa na kibwengo mpenda sifa.

Sasa hivi hata mzazi akiambiwa achangie elfu 20 kwa mwaka kwaajili ya walimu wa part time haelewi.

Yaani ni bora watoto wake wasisome kuliko yeye kulipia hiyo 20,000.

Mafanikio ya wanafunzi wa Saint Kayumba mara nyingi ni Self struggle.
 
Mfano niliotoa unahusu walimu wa sayansi.

Kama mimi nafahamu wawili, nchi nzima lazima wako wengine wengi mtaani.
 
Nimesoma kwenye gazeti la jana, kuna mpango wa kujenga shule za sekondari kwa ajili ya sayansi kwa ajili ya wasichana kila mkoa? tungeimarisha zilizopo na kuzipatia walimu na vitendea kazi kwanza 😎
 
Kikwete na udhaifu wake, alijaribu, aka introduce ile fast track wakapatikana, na wakaajiriwa wakapunguza uhaba,
Sasa ni aibu kukiri kuna shule 1,000 kisha tunajiita Tanzania ya viwanda labda vi-wonder.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Ni kweli maendeleo hayaji haraka pasipo na mission, vision na action.

Wewe umejipambanua kuwa ni wa 1990 kurudi nyuma, unajua nchi ilipotoka hadi hapa ilipo.

Je kwa miaka yote hii ya Uhuru chini ya CCM tunastahili/tulistahili kuwa hapa?
 
Walimu wa science wachache sana miaka yote.
Tamisemi na wizara ya elimu watafute njia sahihi ya kuondoa hili tatizo
Njia sahihi ni kutambua uwepo wa shule ambazo hazifundishi masomo ya sayansi na hisabati ili uandaliwe mtaala mahsusi wa kufundishia.
Na ikionekana wapo wanafunzi walifanya vizuri katika masomo ya sayansi na hisabati wapelekwe kwenye shule zinazofundisha masomo hayo.
Hata hivyo iko haja ya kuiondoa sekta ya Elimu katika Tamisemi ili Wizara Mama ya Elimu itimize majukumu yake moja kwa moja.
Yawezekana kuna Conflict of Interest kati ya Wizara hizi mbili kiasi ya kushindwa kubaini nani wa kulaumiwa pale tatizo/changamoto zinapojitokeza.
 

Unaongelea uhaba waajira au walimu wa science?
 
Unaongelea uhaba waajira au walimu wa science?
Naongelea uwepo wa Jobless walimu wa Physics na Mathematics mtaani.

Na nikaongezea uwepo wa wataalamu wa Afya ( nikiwemo mimi ) Jobless mtaani tangu 2016.

Una kingine ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…