Uchaguzi 2020 Tamko la chama cha Julius Malema wa EFF juu ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Tamko la chama cha Julius Malema wa EFF juu ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

CCM imetuaibisha sana sana tunaona aibu hata kuitwa watanzania sababu ya aibu ya CCM, mmefanikiwa kuwafanya masikini watanzania sasa mmefanikiwa kuharibu hata image ya nchi kimataifa. Hivi Rais anayechaguliwa kwa wizi anafanya kazi gani na nani atamuamini. Kila anapoomekana watakuwa wanaona wamekutana na mwizi, yaani sasa hivi ikionekana sura yako mtu unakumbuka wizi was kura jamani hii ni aibu kubwa sana
Utabaki unalia lia kwa miaka mingine mitano. Pole.
 
Kidogo kidogo dunia nzima inakuja tanzania kuishinikiza serikali irudie uchaguzi huru na wa haki ikiwa na katiba mpya, si hii katiba ambayo wanaikanyaga wenye mamlaka halafu raia anaelipa kodi hio katiba haimlindi mbele ya vyombo vya serikali. we have to do something.
Mkuu pamoja na mapunguvu mengi kwenye Katiba ya sasa bado ccm wameisigina.

Kuna mtoto wa miaka kumi hivi wakati akiangalia DW kwenye sim yangu alisikitika sana. Akasema huenda Rais Magufuli alipass kwa kuibaia mitihani ya wenzake. Nikamuambia alikuwa Mwalimu wa Chemistry. Akasema alikuwa anaiba mitihani shuleni na kuwaletea watoto wake nyumbani. Wakifanya mtihani watoto wake wanaonekana wana akili sana kumbe baba yao kaiba mitihani ya waalimu wengine na kuwapa.

Aibu sana.
 
Kama prezidaa asingekuwa na Elimu angekuwa mwananchi wa kawaida halafu angetumia hizo akili anazotumia kuendesha nchi kwenye huo ukawaida wa maisha ya kila siku angekuwa na maisha magumu sana, NGUVU NYINGI NA MIHEMKO, INASAIDIA UKIWA NA CHEO AU PESA, na ni vile wataogopa kukunyoshea kidole kwa sababu ya hivyo viwili bt to me this guy mmmmmmmmmmmh Hapana kwa Kweli SIBARIKIWI NAE KABISA.
 
Ni kweli kuwa CCM ni chama kikongwe Afrika. Kitendo cha vijana wadogo akina Malema na wenzake akina Mbuyiseni Ndlozi kwa kushirikiana na wenzao akina Mnyika na Zitto kutaka kupambana na vyama vikongwe ni utovu wa nidhamu.

Angalia tamko lao kuhusu uchaguzi wa Tanzania lilivyojaa kibri.
View attachment 1618635View attachment 1618636
Mkuu, mbona hakuna kibri hapo? Wanaeleza ukweli mtupu na ushauri wao ni kuntu
 
Kuna issue ya vyeti feki waliachishwa kazi no matter how long time waliajiriwa,hoja ikawa walijipatia ajira kwa udanganyifu.Kuna tofauti gani na ushindi huu hata asiyekuwa na elimu kubwa anaona kuna magumashi yalifanyika? Uzalendo gani huu? Mwaka 1998 ulifanyika uvujishaji mtihani wa taifa kidato cha nne kwa kiwango cha kutisha.Siku ya pili baada ya kufanyika mtihani ule,ilibidi ufutwe tu maana wanafunzi wangefaulu kimagumashi na kutunukiwa vyeti. Ilibidi mtihani ule urudiwe miezi miwili mbeleni huku kukiwa na ulinzi mkali.Sasa kwa mkhutadha wa matokeo ya uchaguzi huu unahalalisha udanganyifu hata kwenye mambo mengine nyeti katika jamii kama wizi wa mitihani,maana itakuwa ni utamuduni ili ushinde huna budi kufanya udanganyifu.Kuna tabia za kuigana mbinu za kupata ushindi wa kishindo,hata wengine wataiga katika nchi zao.Ushindi huu haukubaliki utapingwa popote duniani na wapenda haki
 
Yaani wanaongea as if kuna mauaji yanatokea mitaani hovyo hovyo wakati huku hali ni shwari na wanachotaka ni turuhusu maandamano halafu watu wakifa watulaumu tena, stupid!
 
Tell Mr. Malema that in Tanzania we have confused guys like himself. Let Malema hear from the people of Tanzania who voted and not otherwise.
 
Wana hoja nzito, wewe tulia ikuingie wala usijidai kurusha ngumi gala wewe.
 
Yaani Magufuli anawaogopa na kuwazimia internet 16% ya watu ambao hawakumpigia kura na kuwaumiza wote including 84% ya Watanzania waliompigia kura? Makes no sense at all.

Kwanini mwaka 2020 na sio 2015? It seems TISS walimwambia mapema kabisa kwamba huwezi kushinda na njia pekee ni kupora mchana kweupe
Kila mtu anajua asingeweza kushinda!
 
Naiona Zimbabwe mpya ngoja washangilie upuuzi.

Hata Mugabe alishangiliwa lakini mwisho wa siku Jeshi likasema hapana Mzee kaa pembeni.
 
Ni kweli kuwa CCM ni chama kikongwe Afrika. Kitendo cha vijana wadogo akina Malema na wenzake akina Mbuyiseni Ndlozi kwa kushirikiana na wenzao akina Mnyika na Zitto kutaka kupambana na vyama vikongwe ni utovu wa nidhamu.

Angalia tamko lao kuhusu uchaguzi wa Tanzania lilivyojaa kibri.
View attachment 1618635View attachment 1618636
Sio kiburi ni mtazamo wa vijana wengi!, sio kila kijana anachozungumza ni kibr HAPANA!, Unachotakiwa kufanya ni kujenga hoja ya kupinga walichokisema sio ukimbilie kusema ni kibri.
 
Back
Top Bottom