Tamko la Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kumtaka Freeman Mbowe kuomba radhi

Yes ni adui wa vyombo vya CCM... !! Vinavyosifu na kiabudu masaa 24 /7

Azory kapotea mwaka wa tatu sasa lakini hatuyaoni matamko ya kulaani toka kwa hawa wasaka tonge.
 
HAWA MAKANJANJA WALISHINDWA KUDAI HAKI YA MWANGOSI KUISHI BADALA YAKE WAKAJIKOMBA KWA SERIKALI WAKATI WA MSIBA PALE JANGWANI!
 
Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
Hivi kumbe kuna DCPC? Ilikuwa wapi miaka yote mitano? Ama ndio imeanzishwa juzi?

"Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari".

Yaani hilo ndio linajulikana leo baada ya TBC kufukuzwa kwa makosa yao wenyewe?
Kitendo cha kukata matangazo mnakikubali lakini kufukuzwa ndio kumewakera?
TBC hawakufukuzwa kwa kutangaza mkutano wa kampeni za CDM, ila hujuma ndio iliyo waponza. Kama lengo nikurusha matangazo mubashara wangerusha halafu wawaachie wananchi waamue mchele ama pumba.
Kama wanakata matangazo haina maana tena kuwepo eneo husika.
Kama ikitokea Mbowe akaomba radhi kwa upuuzi huu, itaanza kampeni yakusitisha harakati za kampeni za uchaguzi na kushinikiza Mbowe ajiuzulu kwanza.
 
Yaani baaada waalani ssheria.kandamizi zinazotungwa na serikali kukandamiza vyombo vya habari

Hiyo ni klabu ya waandishi walevi tu
 
Wapeleke upuuzi huko.

Hakuna mtu atawaomba radhi hao wazee wa bahasha za kaki, hizo njaa zao wazipeleke huko CCM.
Wamewabeba sana miaka yote hawa waandishi.

Habari nyingi za chadema ni za kubumba.

Wana haki kudemand Gastura aombe radhi
 
Ulimwengu wa Wanahabari na Watanzania kwa ujumla ulipigwa na butwaa pale Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Alkaeli Mbowe, alipoamrisha waandishi wa habari wa televisheni ya Taifa (TBC) kuondoka katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za chama hicho, uliofanyika kwenye viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama kwa tuhuma za kwamba wanafikiri wao ni televisheni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika amri yake Mhe. Mbowe alitoa dakika 15. Kwa waandishi hao kuwa wamefunga vyombo vyao na kuondoka katika eneo la mkutano huo kwa madai kwamba TBC ilikuwa imesitisha matangazo ya mkutano huo ambayo awali yalikuwa yakirushwa mubashara.

Mbowe alisema wamechoka kuonewa na kufanywa wapumbavu hivyo aliwapa dakika 15 wawe wameondoka kwenye viwanja vya mkutano.

Kwa vipimo vyovyote vya kimaadili kitendo hicho kilikosa uungwana na hakikubeba misingi ya kiutu hata kama zilikuwepo dalili zozote za kukatishwa kwa matangazo hayo au huko kufanywa wapumbavu kama alivyosema Mhe. Mbowe.

Kitendo kile ambacho kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa siyo tu kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma yao isipokuwa zaidi kilihatarisha usalama wao na vifaa vyao kutokana na mazingira yaliyokuwepo.

Kutokana na hali hiyo ambayo haivumiliki hasa katika kipindi hiki cha kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla.

Tasnia ya habari ni nyenzo muhimu katika upashanaji wa habari hasa nyakati hizi za kampeni za kisiasa na uchaguzi wananchi wanahitaji kujua sera, ilani na mipango ya vyama vya siasa kabla ya kupigakura. Na kwa vyovyote hakuna njia rahisi ya wananchi kuyapata yote hayo kama si kupitia vyombo vya habari ambavyo CHADEMA imeamua kuwadhalilisha.

DCPC inaungana na vyombo, taasisi na watu wote ambao wamekerwa na kitendo kile na inaviasa vyama vingine vyote kujiepusha na mihemuko inayoweza siyo tu kudhalilisha taaluma ya habari lakini pia kuwatia hatarini waandishi wa habari wanapokuwa kazini.

Mwenyekiti DCPC
Irene Mark
01.09.2020
Akwahiyo hao wanasema waombwe radhi walifurahia hujuma za tbc?. Na wanalipwa kwa Kodi za watanzania wote. Wacheni unafiki ndio Mana meko anawakandamiza Kila kukicha kwa ujinga wenu.
 
TBC ndio nguli wa habari nchini huwezi kuwatimua kizembezembe vile!
Huu ni upumbavu mkubwa, nguli anaruhusiwa kufanya makosa ya makusudi?

Hiyo club ya wana habari mbona hatujaina
Ikiikemea tbc ilipokuwa inafanya upendeleo kwa ccm?
Hiyo ni club bali ni kilabu ya ulanzi unsotoka iringa wananywea Dar.

Hapo ndipo vyombo vya habari vya tanzania vinadharaulika ndani na nje ya nchi.
Wanawashinda hata wakenya! Shame
 
Kwa hili 'Tamko' lao tu la sasa ni 'Uthibitisho' ulio rasmi kuwa 'Tasnia' nzima ya Waandishi wa Habari nchini Tanzania iko 'Mfukoni' mwa 'Dola' Kuu.
Wangekua na nia njema wangekua wanakemea madhila waaliopata kina Azory Gwanda au wangepigia kelele hii sheria ya vyombo vya habari inavyotumika kukandamiza vyombo vya habari kupitia idara ya habari maelezo chini ya Dr. Abassi.
 
Back
Top Bottom