Niliandika leo asubuhi kwenye page yangu juu ya upofu wa weledi wa waandishi wa habari baada ya kusoma Tamko la Kaimu Mwenyekiti. Nisijue kuwa haya mambo nikiyowahi kuyashuhudia wakati nafanya kazi na wakina Rostam Aziz, ma spin doctors wa wakati huo, bado yako japo kwa kiwango cha hali ya level ya zero kabisa. Nianze kwa kuungana bq wale waliokwisha uliza hili swala linawahusuje Press Clubs? Irene Mark katumwa na nani kuchafua Press Clubs, zilizojengwa kwa weledi mkubwa na wahenga wakina Karsan kwa lengo la primarily, kutetea maslahi ya waandishi na weledi wa uandishi wa habari Tanzania, wakipigania maslahi na press freedom. Naomba kusaidiwa kwamba Wanachama wa Press Clubs wengi ni waajiriwa wa vyombo binafsi, qmbavyo vyote vimeathiriwa na mfumo mpya wa kunyumwa matangazo, ambayo no chanzo kikubwa cha kipato, na hivi sasa, vingi vineshindwa kujiendesha na wafanyakazi wake wanaishi kwa kuombaomba kwa kukosa mishahara, ni bahati kama Mwenyejiti wa Jukwaa hili si mmoja wa hao. Kwa upande mwingine watendaji wa vyombo vya umma wana neema ya vyombo vyao kuwa ndio wafaidika wakubwa wa matangazo ya serikali, na pili kwa zama hizi ninavyosikia, hata mishahara yao inatoka serikali kuu. Hawa ndio waliolalamikiwa na Chadema wiki iliyopita, na leo hii ACT wamelirudia hilo. Hivi kwa wana Club ya DSM, hamuoni kwamba tatizo lililosemwa linawahusu TBC kama chombo, na kwa weledi ule ule wa kiuandishi lalamiko hilo lingetolewa na vyombo vyenu kwa kuwa tayari waandishi wa habari tena mahiri wamekosoa maana wanajua live ya namna ile haipo kwenye Journalism. Ni vema waandishi wq habari wakajikita kwenye mambo ya msingi hasa weledi katika kazi zao hasa hawa wa vyombo vya habari binafsi ili kuweza kuvutia wasomaji na kuwawezesha waajiri wao kupata hela za kuwalipeni mishahara.